AFRICA YETU: Mjumbe wa AU asema huenda Kony anaumwa

Joseph Kony, kiongozi wa kundi la waasi wa Uganda.(LRA)
Joseph Kony, kiongozi wa kundi la waasi wa Uganda.(LRA)
 
 
Mjumbe maalumu wa Umoja wa Afrika amesema mbabe wa kivita  kutoka Uganda Joseph Kony  huenda  akawa mgonjwa sana na anatafuta hifadhi kwa wapiganaji wake wa kundi la Lord’s Resistance Army.

Fransisco Madeira mjumbe maalum wa Umoja wa Afrika anayehusika na swala la kundi la waasi wa Uganda- LRA, alisema Jumatano  kwamba kiongozi wa Jamhuri ya Afrika Kati amewasiliana na Kony na anajaribu kufanya mashauriano naye ili kujisalimisha kwake.

Lakini Madeira anasema inawezekana Kony anaidanganya serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati ili inapofanya majadiliano, apate muda wa kufanya  mkakati  wa kuhamisha wapiganaji wake.

Mjumbe huyo hakutoa maelezo zaidi kuhusu kuugua kwa Kony.

Related Posts