Flamingo huwa na tabia ya kuhama kufuatana na mazingira wanayohitaji.
Moja ya vituo vyao ni kwenye hifadhi ya Arusha hususan kwenye maziwa ya
Momella. Kwakuwa maji ya Ziwa hili ni Alkaline, maji haya yanawavutia
algae ambao ni chakula kikuu cha Flamingo.
Ziwa la Momella (Kubwa) lipo kwenye mpaka wa Hifadhi ya Taifa na Kijiji
cha Maji ya Chai. Uzio unaouona ndio alama ya mpaka na vibanda
vinavyoonekana kwa pembeni ni nyumba za wanakijiji ambazo zipo nje ya
hifadhi.