YALIYOJILI MPAKA MPIRA UNAMALIZIKA: YANGA YATOSHANA NGUVU NA WAJELAJELA



KATIKA VIWANJA VYA SOKOINE TENA YANGA WAIBUKA NA SALE TENA

YANGA leo imecheza na timu ya Prison ya jijini  Mbeya katika viwanja vya sokoine na kutoa sale katika ya 1-1 hadi mpira unamalizika uwanjani hapo.

Mpira huo uliochezwa  ukiwa na mashabiki wengi wa timu ngeni ya Yanga huku wenyeji wakiwa na mashabiki wachache yanga ndio walio tangulia kuwachapa wenyeji wao.

Katika dakika ya 43 kupitia Jelson Tengete alifanikiwa kuipatia timu yake goli la kwanza na kuwaibua mashabiki wa timu hiyo ambayo ilikuwa na mashabiki wakutosha karibu nusu ya uwanja.

Hadi kipindi cha kwanza kina malizika timu zote zinaenda mapumziko Yanga iliingia ikiwa na furaha ya goli moja.

Mpira ulianza kwa kasi katika kipindi cha pili ambapo timu ya Prison iliingia na kasi mpya na kuhakikisha ina sawazisha goli lake.

Prison kupitia Peter Michael ambaye alipokeampira usio rasimi katika piganikupike iliytotokea katika goli la Yanga kwa kutupia mpra wa kichwa katika nyavu za wapinzani wake.

Mpira mpaka unamalizika katika uwanja wa sokoine Yanga 1 na Prison 1 huku hali ya usalama ikiwa imeimarishwa vua kutosha uwanjani hapo.

Yanga wametoka na sale ya pili katika uwanja huo baada ya sale ya kwa nza kutoa na timu ya Mbeya City kwa goli 1-1 siku ya jumamosi ya tarehe 14 Septemba ikiwa ni mara ya kwanza kwa timu hiyo kuingia mkoani Mbeya katika msimu huu ambapo Mbeya inatimu mbili katika ligi kuu ya Tanzania.