ALIANZA SUGU KUZUNGUMZA NA WANANCHI |
DR. SLAA AKIZUNGUNZA NA WANAMBEYA NA KUINYESHAUTHIBITISHO WA RIPOTI YA UFISADI W TANZANIA |
KATIBU mkuu wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),
Willbrod Slaa, amemuomba Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kito pitiosha
mswada wa katiba Mpya na urudishwe bungeni kwaajili ya kujadiliwa upya.
Aliyasema hayo jana katika mkutano wa hazara mkoani Mbeya
uliofanyika katika viwanja vya Ruanda Nzovwe wakiwa na lengo la kueleza kilichotokea
Juzi Bungeni kuwa ni ukiukwaji wa sheria na 76 ambapo ilitakiwa kuahilisha kwa
muda bunge.
Slaa alisema kuwa kutokana na vurugu hizo zilizo sababishwa
Chadema kuto jadili mswada huo na kupitisha kisha kupitishwa na chama cha mapinduzi
(CCM) kwa ubabe wakiongozwa na Naibu Spika wa Bunge Job Ndugai.
Alisema hawako tayari kukubaliana na mswada huo endapo Rais
atakuwaamepitisha na kutojali mawazo ya kambi ya upinzani wakati wametumwa nawananchi
kunda kutetea haki zao.
Katibu huyo aliongeza kuwa Jaji Walioba ametumia busara
kusikiliza mawazo ya wananchi juu ya katiba Mpya na kuyaweka maoni yao katikakatiba
hiyo ili iweze kuwa msaada kwa maisha ya watanzani wa leo na vizazi vijavyo.
“Katiba mpya haina matatizo kwa kuwa Jaji Walioba alichukua asilimia kubwa ya maoni ya wananchi
na kuyaingiza katika Rasimu ya katiba mpya ambayo itakuwa muongozo kwa maisha
ya watanzania, Serkali ya Tanzania, kwa miaka 100 ijayo” alisema Slaa.
Alisema viongozi wa CCM wamekuwa wakiipinga Rasimu hii kwa
kuwa inasema ukweli na inaitia kitanzi serikali iliyopo madarakani na kukiua
chama cha mapinduzi kulingana na mfumo uliopo.
Aliongeza kuwa wabunge wa Vyamna pinzani bungeni hawapo
tayari kuona Rais anapitisha mswada huo ambao utakuwa na madhala kwa wananchi watanzania
waliokuwa wamezoea amani na utulivu kuingia katika vurugu.
Kwa upande wake mbunge wa Mbeya mjini kupitia Chadema Joseph
Mbilinyi (maarufu Sugu) alisema kuwa kitendo cha Kutolewa nje Mwenyekiti wao ndicho
kilicho sababisha vurugu bungeni nay eye kutolewa nje kwa kubebwa na jeshi la
askari Polisi.
Sugu alisema hana visa na serikali wala Jeshi la Polisi yeye
anawachukia viongozi wababe pale bungeni kama Job Ndugai ambaye alimuitia
Asikari Polisi kwaajili ya kumtoa nje na kumuaibisha mbele ya wapiga kula wake
na taifa kwa ujumla.
Alisema kuwa mapambano yataendelea hatakubali kuona wananchiwakitendewa
vibaya na wabunge wa CCM wakati naeyupo Bungeni kwaajili ya kutetea wananchi
wasio kuwa na sauti waliomtuma kuwatetea.
Mbunge huyo alisema kuwa katiba ni mali ya nchi na sio mali
ya chama chochote cha siasa na hivyo inatengenezwa kwaajili ya maslahi ya wananchi
wa itikadi zote na sio kama inavyo taka kutengenezwa kwaajili ya CCM.
Aliongeza kuwa kama serikali ina polisi wengi iwapeleke
kuwakamata watu wanaojihusisha na madawa ya kulevya katika viwanja vyandege na mabadali
na sio kuwakamata wabunge wanao tetea wananchi bungeni.
Mwisho