MECHI ya kwanza ya Mbeya City kucheza na klabu kikubwa hapa Tanzania na klabu bingwa mtetezi wa kombe la ligi kuu ya Vodacom Tanzania Yanga imetoa sale ya 1-1.
Mbeya City hii ni sale ya pili kati ya mechi zake tatu ilizo zicheza nyumbani tangu iingie katika ligi kuu baada ya kupanda daraja mwaka jana.
Katika mechi ya kwanza Augosti 24 mwaka huu (2013) Mbeya City ili cheza na timu ya Kagera Sugar ambapo si Mbeya City wala Kagera iliyo fanikiwa kutikisa nyavu za mwingine.
Mchezo huo ambao uliinua mashabiki wa timu ya Mbeya City licha ya kuwakosakosa mahasimu wao timu ya Kagera sugar.
Kupitia mchezo huo Mbeya city ilijizolea mashabiki kwani wengi wao walitaka kuiona mchezo wake mikiwa katika ligi kuu na walilizika na mchezowao.
Mbeya City katika mechi yake ya pili ndo iliongeza mashabiki na kuwavuta wale walikuwa na Usimba - simba na Uyanga - yanga ambao wamekuwa wapenzi na mashabiki halisi.
Mechi hiyo ambayo ilikuwa na upinzani mkubwa na ilichezwa Augost 28 mwaka huu katika uwanja wa Sokoine ambapo Mbeya City walikuwa wenyeji wa Timu ya Ruvu Shooting ambao waliwachapa goli 2-1 wakijivunia uwanja wa nyumbani.
Hapo Mbeya city iliyo chini ya kocha mahili Juma Mwambusi ambayw aliipandisha timu hiyo ka umahiliwake katika ufundishaji wa mchezo huo unaopendwa na wengi ilipo ongeza mashabiki.
Timu hiyo inayo onyesha utundu na umahili wake katika soka ikiwa na wachezaji vijana na wengi wao wakiwa ni kutoka jijini Mbeya.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)