KAMATI ya uchaguzi ya Chama Cha waandishi wa Habari Mkoani
Mbeya imewatanzaza wagombea katika nafasi mbalimbali wanao wania uongozi katika
chama hicho.
Majina hayo yametangazwa jana na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Ulimboka
Mwakilili mbele ya waandishi wa habari katika nafasi mbalimbali za uongozi.
Aliyataja majina hayo kuwa ni kuwa waliogombea nafasi ya
Uwenyekiti wa Klabu Partrick Kosima, Uswege Luhanga wakati makamu Mwenyekili
ikiwa inagomewa na mtu mmoja Modestusi Nkulu.
Alimtaja anaye chukua nafasi ya ukatibu kuwa ni Emmanuel Lengwa
wakati nafasi ya utuza hazina ikiwa inagomaniwa na watu wawili ambao ni Brand
Nelson na Ainess Thobias huku nafasi ya ujumbe kamati kuu ikiwa inanyang’anyiwa
Furaha Eliab na Jackson Numbi.
Alisema kuwa kuna nafasi ambazo hakuna mtu aliyechukua fomu
za na kuwa ziko wazi na zitatolewa na mkutano mkuu wa uchaguzi juu ya nafasi
hizo.
Alizitaja nafasi ambazo ziko wazi na hazijachukuliwa na mtu
yeyote ni nafasi ya Uwenyekiti wa nidhamu na maadili huku nafasi wagombea
wakiwa hawajatosha kama nafasi ya Ujumbe.
Mwakilili alisema kuwa wametoa muda kwa watu walio na
wasiwasi wa wagombea au mgombea kama anahitaji mabadiliko au hajatendewa haki.
Alisema kwa wagombea wananafasi hadi siku ya Mei 23 huku
wanachama ambao wanawasiwasi wanaruhusiwa mpaka siku ya leo kutoa maoni yao.