WANAO ZUNGUKA BONGE LA MTO SONGWE KUNUFAIKA NALO


WAKAZI wa wilaya za Ileje na Kyela wanaolizunguka bonde la Mto Songwe lililo katika Mpaka wa Tanzania na Malawi wanatarajiwa kunufaika na bonde hilo kupitia mradi wa uboreshaji wa Bonde la mto huo unao fanywa kwa ushirikiani wa Nchi hizo Mbili.

Akiwasilisha taarifa kuhusiana na mradi huo wa uboreshaji wa bonde la Mto Songwe, Eng. Gabriel kalinga katika baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Ileje, alisema kuwa wakazi wa wilaya lilimopita Bonde la Mto huo watanufaika kutokana an uboreshaji wa Bonde hilo.

Alisema mradi huo unaotekelezwa kwa kuzihusisha nchi Mbili za Tanzania na Malawi utawanufaisha wakazi wa pande zote mbili kwa kuwa utaweza kuzalisha umeme kutokana na uboreshwaji wake.
Mradi huo unao ghalimu Euro million 400 ulianzishwa kwa lengo la kudhibidi uhalibifu ambao unatokana na mafuriko baada ya Mto huo kuhama kutoka katika njia zake na kuhamisha mpaka unao tendanisha nchi.

“Ili kudhibidi madhara ya mto nchi hizo mbili zilikaa na kujadili kutengeneza mabwa matatu ambayo yataweza kuzuia madhara na kuleta faida kwa wakazi wanao lisunguka bode hili”. alisema Eng. Kalinga
Alisema mabwawa hayo wataweza kuzalisha umeme wa kilowatt 340 ambazo zitaingizwa katika mkondo wa taifa na kusambazwa katika vijiji ninavyo zunguka Bonde hilo la mto Songwe hasa katika wilaya ya Ileje.

Alitaja maeneo ambayo mradi huo utayajenga mabwawa matatu kuwa ni katika Kata ya Bupigu, Malangali kwa upande wa Wilaya ya Ileje na Wilaya ya Kyela ni eneo la Ngana Nduka ili kuzuia madhara na kuleta faida kwa wakazi wanao lisunguka bode hilo.

Naye mkurugenzi wa wilaya ya Ileje Sylvia Siriwa alisema kuwa mradi huo utakuwa kivutio kikubwa kwa katika inchi hiyo na utasaidia wakazi walio karibu na mradi huo kupata umeme na maji safi kwa ajili ya matumizi ya binadamu.

Alisema kuwa faida nyingine itakayo tokana na mradi huo ni kuweza kuimarisha zaidi umoja kwa nchi hizo mbili kwa kuwa watakuwa wakitumia wote bonde hilo na kujinufaisha kwa ajili ya kilimo hucho.

 Kwa upande wa wajumbe wa baraza hili la madiwani walikuwa na wasiwasi wa kuto nufaika na mradi huo ambao utajegwa na katika maeneo ya kata zao kama ulivyo kuwa mradi wa mgodi wa makaa ya mawe ambao uliasisiwa na wilaya Tatu za Kyela, Rungwe, na Ileje  na wilaya yao kuto nufaishwa na mradi huo.