WAFANYABIASHARA WASHAURIWA NA CRDB-MOMBA


Meneja wa CRDB tawi la Mbozi akiwa katika mahojiano na waandishi wa habari mara baada ya kuzungumza na wafanya biashara wa Mji Mdogo wa Tunduma hivi karibuni kuhusiana na faida za Bima katika biashara zao




WAFANYABIASHARA Nchini wametakiwa kufungua Bima katika biashara zao ili kujikinga na majanga mbalimbali yanayo weza kuwarudisha nyuma kibiashara.

Wito huo umetolewa mwishoni mwa wiki katika Mji mdogo wa Tunduma Wilayani Momba na Meneja wa benki ya CRDB tawi la Mbozi Mkoani Mbeya, Cornelius Msigwa, wakati wa hafla fupi ya kutoa elimu wafanyabiashara wa wa mji ndogo wa Tunduna na wamiliki wa bima wa Benki hiyo.

Msigwa alisema kuwa wafanya biashara wakikata bima za urizi wa biashara zao zitakuwa salama hata watakapopatwa na majanga mbali mbali na haya ya moto.

Alisema Mfanyabishara aliyekata Bima kwa biasharayake muda mfupi atakapo patwa na janga la Moto, Kuibiwa au kuvamiwa na Majambazi atafidiwa mali zake na benki hiyo kupitia huduma ya Bima inayotolewa Nchi nzima.

Meneja huyo alisema kuwa kuna wafanyabiashara wa Mji Mdogo wa Tunduma Wilayani Momba mkoani hapa wamenufaika na huduma za bima baada ya kuungua kwa maduka yao baada ya janga la moto lililotokea mwaka jana.

Nao wanufaika wa huduma hiyo ya Bima ya biashara alisema kuwa huduma hiyo imewaokoka kutika majanga baada ya maduka yao kuteketea kwa maduka na kuwa wasinge kuwa na huduma hiyo wangekuwa katika wakati mgumu kibiashara.

Mmoja wa wafanya biashara walionufaika na huduma ya Bima baada ya duka lake kuungua, Mhamed Ulaya alisema kuwa alipata fidia yake mapema na kuendelea na biashara yake kama awali bila kuteteleka.

Kwa upande wa afisa uhusiano wa CRDB kitengo cha Bima Nyanda za juu Kusini Neema Boniface alisema kuwa kwa mteja wa Bima ili apate huduma anahitajika kutoa ushirikiano wa kutosha kwa wafuatiliaji wa malipo ya mteja na kuwa na makabrasha muhimu ya manunuzi.

Alisema makabrasha hayo yataisaidia Benki kujua gharama za mteja wabima na anatakiwa kuripoti mapema Katika tawi lolote la Benki hiyo ili hatua za awali zichukuliwe na kufanyiwa malipo kwa haraka.