Mwandishi
Mkuu wa Mbeya yetu Joseph Mwaisango akiwaanasindikizwa na dogo Asajile
huku akielezwa ni jinsi gani walimfahamu mtoto mwenzao Debora kwakweli
watoto hawa wamesema hawaamini kabisa kama Debora hawata mwona tena
MKASA
wa baba kumuua mwanae kwa kumzika akiwa hai kutokana na mgogoro wa ndoa,
umezidi kuibua mapya, baada ya mama mzazi wa marehemu ,Debora Riziki (3),
kusimulia mkasa mzima .
Akizungumza
kwa hisia kali, katika mahojiano maalumu na Mbeya yetu kijijini kwake
Ibula, katika kata ya Kiwira, wilayani Rungwe, Mama mzazi wa Marehemu, Esther
Mwambenja, alisema kabla ya tukio hilo kutokea kulikuwa na viashiria vingi vya
mumewe kufanya ukatili.
Alisema
tukio la mzazi mwenza huyo kumwiba mtoto na kwenda kumfanyia
ukatili huo wa kinyama lilikuwa la pili, baada ya awali kumuiba akiwa na
miaka miwili na miezi mine na alimrudisha kwa maandishi ya serikali ya kijiji.
Alisema
katika tukio la kwanza la mtalaka wake huyo kumuiba mtoto wao huyo, lilitokea
Septemba mwaka 2012, baada ya wiki chache za kumfukuza katika nyumba waliyokuwa
wakiishi katika kitongoji cha Iponjola, kijiji cha Asenga, nyumba iliyotumika
kuzikwa mtoto huyo.
Alitaja
sababu za yeye kufukuzwa ni ugomvi uliotokana na yeye kuhoji sababu za
kuficha fedha kiasi cha sh. 120,000 zilizotokana na wao kwa pamoja
kufanya kazi ya kibarua katika mashamba kijijini hapo na baada ya malipo
kutolewa mtalaka wake huyo alionesha kiasi kidogo cha sh.80,000.
Alisema
ugomvi huo ndio ulisababisha yeye arudishwe kwa wazazi wake, lakini baada
ya muda mfupi mwanaume huyo alimfuata na kumbembeleza ili warudiane na
alipogoma aling’ang’ania aondoke na mtoto .
“Nakumbuka
ilikuwa Novemba mwaka jana baada ya mimi kuondoka nyumbani kwake na kurudi
kuishi hapa nyumbani, siku hiyo tukiwa shambani huyo bwana alikuja hapa
nyumbani na kumkuta mwanangu wa kwanza (Neema Steven ) niliyezaa na mwanaume
mwingine” alisema Mwambenja.
Alisema
baada ya kufika eneo hilo majira ya saa mbili asubuhi alitumia ujanja na
kufanikiwa kumuiba mtoto na kisha kutokomea naye kijijini kwao Asenga, hali
ambayo ilisababisha kutoa taarifa kituo cha polisi Kiwira.
“Unajua
kuwa baada ya kwenda kutoa taarifa polisi walitusaidia kufika kijijini kwao
ambapo serikali ya kijiji ilikubali nimchukue mwanangu kwa kuwekeana mkataba wa
kisheria kwa mujibu wa sheria, kwani alikuwa chini ya miaka saba”.
Aliongeza
kuwa Novemba 15 mwaka 2012 serikali ya kijiji chini ya Mwenyekiti,
Lutengano Mwakyoma na mashahidi watano wakiwemo wazazi na ndugu zake,
walinikabidhi barua ya kuridhia kuondoka na mwanangu, huku ikimuonya mume wangu
kutorudia kosa hili la kumuiba mtoto hadi hapo atakafikisha miaka saba.
Tukio
la pili la kuiba mtoto.
Alisema
tukio hilo lilitokea Novemba 29 mwaka jana 2012, ambapo alifika nyumbani kwao
majira ya saa 12 :00 na kumkuta dada wa marehemu kumchukua mtoto akimdanga kuwa
anaenda kusenya kuni eneo la jirani.
Aliongeza
kuwa baada ya kuona dada wa marehemu anang’ang’ania kwenda wote alimuamuru
arudi nyumbani kuchochea moto kwa kuwa kulikuwa kumeinjikwa mboga na kukubali
kurudi.
“kwa
mujibu wa maelezo ya mwanangu huyu wa kwanza alisema baada kurudi toka ndani,
alikuta baba yake huyo ameondoka na mtoto na tuliporudi na kupokea taarifa hizo
tulichanganyikiwa na kuanza kuhangaika hovyo” alisema mama wa marehemu.
Mwambenja
alisema kuwa baada ya kucha siku ya pili asubuhi yake walienda kutoa taarifa
kituo cha polisi cha Kiwira ili waweze kupata msaada wa kumtafuta, huku
wakionesha barua ya makubaliano ya awali ya yeye kuwa na haki ya kisheria ya
kusimamia malezi ya mwanao hadi afikishe miaka saba.
Alisema
baada ya kutoa taarifa hizo kituoni hapo, askari aliyekuwa zamu siku hiyo
alimtaka kutoa kiasi cha shilingi 50,000 ili fedha hizo wapewe askari mgambo wa
kwenda kijijini kwa mzazi mwenzake huyo, kwani tayari walikuwa na taarifa
kuwa alikuwa amekimbilia huko.
“Kutokana
na hali ngumu ya maisha tulikosa kiasi hicho cha fedha hivyo suala hilo
kubaki bila msaada wa polisi na pia hatukuweza kwenda kwa kijijini kwao”.
Aliongeza
“sababu ya mimi kuwa mzito kuendelea kumfuatilia kijijini kwao kwa mara ya pili
ili kujua kama yupo huko na mtoto ilitokana na hofu niliyoijenga, kwani awali
tukiwa kwenye ugomvi alitamka maneno ya vitisho kuwa endapo nitaendelea
kung’ang’ania kumchukua mtoto pale anapomchukua atakuja kumuua ili tukose
wote”.
Hata
hivyo mama huyo mzazi wa Debora, alisema kuwa baada ya kuona hali hiyo,
aliendelea kuwasiliana na wifi yake , Bupe Mwangoka,ambaye ni dada mkubwa wa
mume wake anayeishi eneo la Isanga Jijini mbeya, ambaye ndiye
alisaidia kwa kiasi kikubwa kubainika kwa unyama aliofanya.
Maisha
kabla ya tukio.
Akielezea
maisha yao kabla ya kutengana na baadae kuamua kufanya ukatili huo, alisema
aliwahi kumtamkia maneno makali wakati akiwa na ujauzito wa miezi nane .
Alisema
baada ya kuibuka ugomvi katika kipindi hicho, mwanaume huyo alimtaka kwenda
kuiuza mimba ile kwa mwanaume mwingine yeyote atakayempenda ili asije akazaa
mtoto ambaye atachanganya damu ya koo hizo mbili.
“Maneno
yale katika kipindi hicho sikuyatilia maanani kwani nilifikiri zilikuwa ni
hasira, lakini leo hii ndio najua maana ya ile kauli ” alisisitiza Mwambenja.
Hata
hivyo alisema inashangaza kwani kuna wakati tukiwa katika maisha ya
kawaida kabla ya yeye kufanya tukio hilo, mara kadhaa alijutia na kuonya juu ya
matukio machafu yaliyojitokeza na kusikika ya watu kuuawa au kuondolewa baadhi
ya viungo vya miili yao.
Aidha,
alieleza mkasa mwingine wa mume wake huyo ni ule wa wao kufukuzwa katika mji wa
Kiwira walikokuwa wakiishi awali kwa kufanya shughuli za umachinga.
Alisema
walitimuliwa na serikali ya mtaa katika mji huo kutokana na mumewe huyo kutuhumiwa
kuiba simu ya mkononi ambapo alipokea kipigo kikali na baadae kufukuzwa.
Kutokana
na hali hiyo, mama wa marehemu Debora alisema yote yaliyotokea amemwachia mungu
na kwamba kama ingekuwa uwezo wake angeamuru naye anyongwe, hivyo mamlaka
husika zitajua cha kufanya.
Kwa
upande wake dada wa marehemu Debora, Neema Stevini(5) ambaye ni mtoto wa
kufikia wa baba mzazi wa marehemu, akisimulia jinsi mdogo wake alivyoibwa ,
alisema kuwa anakumbaka mara ya mwisho ilikuwa jioni majira ya saa 12 jioni.
“Nilitaka
kwenda nao, lakini baba Debora akaniambia nirudi kuchochea moto ndani na
niliporudi nikakuta wameondoka na nilipokimbilia sana siku waona” alisema kwa
masikitiko Neema.
Hata
hivyo uchunguzi wa Mbeya yetu umebaini kuwa marehemu Debora alifariki dunia siku
hiyo ya Novemba 29 mwaka jana, majira ya saa nne usiku baada ya baba yake
kufanikiwa kumuiba kutoka nyumbani kwa mama yake.
Inadaiwa
kuwa baada ya kufanikiwa kumtorosha baba huyo wa marehemu alitembea kwa mguu
umbali wa kilomita 50 kutoka kijiji cha Ibula alikomuiba hadi nyumbani kwake
kijiji cha Isange katika kata ya Isange.
Imeelezwa
kuwa baada ya kufika nyumbani kwake, baba huyo mzazi wa marehemu alichimba
shimo katikati ya sebule na kumchukua mtoto wake huyo akiwa usingizini na kisha
kumfukia akiwa hai.
“Mwanaume
Yule alikuwa katili sana, kwani baada ya kumfukia alichukua meza ya chakula na
kuiweka juu yake huku akiipamba kwa magazeti jambo ambalo lilifanya ndugu zake
wasigundue kirahisi” alisema mpasha habari.
Chanzo
hicho kilisema baada ya kufanya hivyo aliishi kwa wiki moja na baadae
kukimbilia Jijini Mbeya ili watu wasibaini juu kitendo alichofanya na kwamba
kila alipohojiwa na ndugu zake alisema mwanae huyo alimuweka kwa rafiki yake
Jijini Mbeya.
Hata
hivyo baada ya danadana za muda mrefu ndipo dada wa mtuhumiwa huyo aliamua
kutoa taarifa jeshi la polisi na kufanikiwa kumkamata akiwa katika harakati za
kutorokea wilayani Chunya na alipobanwa alifichua siri ya alipo mwanae kwa
kueleza kuwa alimuua na kumfukia ndani kwake.
kwa msaada wa:
na
Venance Matinya
|