WAKULIMA wa
wilayaNI Kyela mkoani Mbeya wamesusia vocha za mbolea ya ruzuku licha ya serikalai
kupunguza kutoka 835,000 kwa mwaka wa 2011/12 hadi vocha 7,973 za pembejeo
zilizofika Wilayani humo kwa mwaka huu zimedoda.
Akizungumzia
suala hilo Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kyela, Abdarah Mfaume
alisema kuwa sababu inayosababisha wakulima kutojitokeza kwa wakati
kujiunga na mpango wa mbolea za ruzuku ni kutokana na uwezo mdogo wa kuchangia
bei za pembejeo.
Alisema kuwa Serikali
inamchangia mkulima sh,50,000, na mkulima mwenyewe kutoa sh, 26,000, lakini
bado muitikio wa wakulima hao kuzichangamkia mbolea hizo ni mdogo na kuwa hadi
sasa vocha bado zipo kwa baadhi ya maeneo.
“Ni kweli mwaka
huu vocha zilifika chache ukilinganisha na mwaka jana wananchi wananchi
hawakujitokeza kuchukua, lakini bado utokaji wa vocha hizo ni wa kusuasua hii
inatokana na wakulima kutojipanga vizuri kwa ajili ya kilimo na ndiyo maana baadhi
yao wameshindwa kuchangia gharama hizo” alisema Mfaume.
Alisema kuwa mbali
ya vocha hizo na mbegu kuwahi kuwafikia na Serikali kupunguza bei yake ya
kununulia lakini mwamko kwa wakulima kuzinunua vocha hizo umekuwa ni mdogo sana
kwa kuwa ziifika chache na bado zimebaki nyingi.
Mkurugenzi huyo
alizitaja changamoto zilizo changia mkulima kutozishangamkia vocha hizo ni
pamoja na ushirikiano mdogo kati ya kamati ya vocha ya kijiji na ya kata jambo
lililopelekea baadhi ya wakulika kuacha kuchukua vocha kutokana na
ucheleweshaji wa kamati hizo.
Aliongeza kuwa
ugeni wa zoezi la kutumia makampuni badala ya mawakala kama ilivyozoeleka ni
moja ya sababu iliyopelekea wakulima kutojitokeza kuchukuwa vocha hizo.
Baadhi ya wakulima
waliozungumza na NIPASHE kwa masharti ya kutotaja majina yao walisema kuwa
tatizo lililopo ni kwamba serikai licha ya kupunguza hata hivyo bado haiendani
na hali haisi ya watanzania kwa sasa.
Walisema kuwa
maisha yamekuwa magumu bei ya vyakula inapanda kwa kasi kubwa hivyo wakulima
wamekuwa wakipata changamoto kubwa pindi zinapofika vocha hizo kutokana na
kukabiliana na mambo mengi ya shule na mambo mengine.
Aidha waliongeza
kuwa ni vyema serikali ikaanzisha utaratibu wa ugawaji mbolea kipindi cha mwezi
Juni au Julay kwa kuwa kipindi hicho ndicho wakulima wanakuwa na chakula kingi
na pesa zinapatikana kuliko kipindi ambacho wengi wanakuwa wamezitumia katika
mambo yao mbali mbali.
MWISHO.