Diwani wa kata ya
Tunduma Ndugu Frank Mwaijoka (Chadema) pamoja na mchungaji wa kanisa la KKT
katika eneo hilo la Tunduma wilayani momba Mkoani mbeya wametakiwa
kujisalimisha kituo cha Polisi Tunduma mara baada ya kuhusika na uchochezi wa
kidini hali ambayo imepelekea kutokea kwa vurugu katika eneo hilo.
Vurugu hizo zimeanza
majira ya saa 3:asubuhi katika eneo hilo la tunduma mara baada ya kundi la watu
wanaodai kuwa wao ni wafuasi wa dini ya kikristo wakidai waruhusiwe kuchinja
mifugo na kuuza katika mabucha yao hali iliyo pelekea kuibuka kwa vurugu hizo.
Akizungumza kuhusiana
na tukio hilko Kamanda wa Polisi Mkoani humo Ndugu Diwani Athumani amesema kuwa
kufuatia kuwepo kwa tukio hilo jumla ya watu zaidi ya 40 tayari wamekwisha
kamatwa .
Amesema mpaka sasa
taarifa walizo zipata kufuatia vurugu hizo zinaeleza kuwa miongoni mwa watu
walichochea vurugu hizo ni diwani wa kata hiyo ya Tunduma Ndugu John mwaijoka
pamoja na Mchungaji wa kanisa la kkt ndugu Neema Mwaipusa ambao kwa pamoja
wametakiwa kujisalimisha kituo cha polisi kwa mahojiano zaidi.
Amesema suala hilo
limegubikwa na siasa kwani tayari viongozi wa serikali akiwemo Mkuu wa
mkoa huo Ndugu Abbas Kandoro amekwisha litolea ufafanuzi Apri 02 mwaka huu
wakiwepo pia viongozi wa dini .
Amesema kwa asilimia
kubwa mgogoro huo juu ya nani achinje umeingiliwa na mambo ya kisiasa kwani
hata baadhi ya wananchi wa maeneo hayo wamekuwa wakilalamika juu ya kutokea kwa
vurugu hizo.
Amesema shughuli za
kibiashara katika eneo hilo zimeshindwa kufanyika katika eneo hilo hivyo kufanya
wananchi kupata adha hasa kwa nchi jirani ya Zambia ambao kwa asilimia kubwa
wanategema kupata mahitaji kutoka mpakani mwa Tanzania.
Hata hivyo Diwani
amesema kuwa katika vurugu hizo askari mmoja pamoja na mwananchi wamejeruhiwa kwa kupigwa mawe ambapo tayari
wamekwisha fikishwa kituo cha polisi.
Kufuati hali hiyo
Kamanda huyo wa Polisi amesema kwa sasa hali imelejea katika hali yake ya
kawaida hivyo amewataka wananchi wa maeneo hayo kuwa watulivu wakati jeshi
hiulo la Polisi likiendela na msako wa kuwatafuta wahalifu wengine.
|