PINDA KUTUA MBEYA MEY 10 NA 11 KUANZA ZIARA



WAZIRI mkuu wa Tanzania Mh. Mizego Peter Pinda ana tarajia kufanya ziara mkoani hapa pamoja na kuwasha mwenge wa uhuru na kuzindua kampeni za sense ya watu na makazi.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, mkuu wa mkoa wa Mbeya, Abas Kandoro  amesema waziri mkuu ataingia mkoani hapa Mei 11 na atawasha mwenge wa uhuru katika uwanja wa sokoine.

Amesema mbali na kuwasha mwenge wakati huo huo atazindua kampeni za sensa ya watu na makazi pia atatembelea sehemu mbalimbali katika mkoa wa Mbeya.

Kandoro ametaja sehemu ambazo Mh Pinda atatembelea ni pamoja na kilicho kuwa kiwanda cha nyama, kiwanda cha marumaru cha Marmo na hatimaye katika kituo cha utafiti wa kilimo Uyole.

Aidha mkuu wa mkoa wa Mbeya amewataka wananchi kujitokeza kwa vingi katika uwanja wa sokoine katika uwashaji wa Mwenge wa uhuru na uzinduzi wa kampeni za sensa ya watu na makazi.

Awali mkuu wa mkoa amewataka viongozi wenye nyadhifa mbalimbali kama wanajiudhuru wasijiudhuru kwa kumchafua kiongozi mwenzake.

Ameyaema hayo baada ya kujiudhuru kwa mkuu wa wilaya ya Mbozi, Gabriel Kimoro, wakati akitolea ufafanuzi kuhusu barua ya kujiudhuru kwa kiongozi huyo.