WAZEE WACHANGIWA TAMASHA LA PASAKAMBEYA

  • NI KWAAJILI YA KUJENGA KITUO CHAO

  • MABENI YA KULALA WAZEE 36 YATAANZA KUJENGWA KUNZA

ZAIDI ya shilingi milioni 20 zimekusanywa katika tamasha la pasaka lililo ambatana na harambee ya kuchangia ujenzi wa kituo cha kulelea wazee mkoani Mbeya.

Tamasha hilo ambalo lilifanyika juzi katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya na kupambwa na kwaya pamoja na wasanii wa nyimbo za injili, Jenifa Mgendi, Masa MwaipajaKwaya ya Kijitonyama Upendo Group kutoka Dar es salaam na kwa ya za mkoani kutoka katika makanisa mbalimbali mkoani hapa.

Mmoja kati ya waandaaji alisema, wamekusanya shilingi millioni 20,610,000 taslimu ambazo zilichangwa na watu waliohuzulia katika tamasha hilo.

Wakiwa na lengo la kukusanya shilingi milioni 150 ili kukamilisha ujenzi wa kituo cha wazee waiojiweza na na zahanati ambayo watatibiwa bure.

Akizungunza katika tamasha hilo meneja wa Bomba fm, Fred Helbeti alisema, katika kituo hicho wata jenga bweni la wazee na zahanati ya ambayo wazee watatibiwa hapo hapo bure na bila foleni ya kuwachocha

Hebeti alisema, bweni litakalo jengwa katika kituo hicho lita kuwa na uwezo wa kulala wazee 36 ikiwa ni mwanzo tu.

Mbali matamasha hilo, wataendelea kuandaa matamasha mengi huko mawilayani ili kuwawezesha ambao hawa kufika katika tamasha hilo lililofanyika jijini Mbeya na walitamani kuchangia.

Alisema, wameamua kuanzisha tamasha hilo ni baada ya kuona matamasha mengi yamekuwa wakilenga katika kuchangia yatima na watu wenye ulemavu.

Aliongeza kuwa, wamekuwa wakijitolea katika kutoa misaada mbalimbali ya kijamii ikiwemo kwenda kuwaona watoto yatima na watoto waishio katika mazingila magumu.