WAKRISTO WAASWA MKOANI MBEYA NA TANZANIA KWA UJUMLA


YESU KRISTO AKIWA KATIKA MATESO MAKALI MSARABANI
WAKRISTO nchini wametakiwa kutumia kipindi hiki cha kwalesma kudumisha amani na upendo miongoni mwao kwa kuwasaidia wale wasiojiweza na pia kuwatembelea wale waishio katika mazingira magumu na kuweza kuwafariji ili na wao wasiweze kujisikia upweke.



Akihbiri katika ibada ya IJUMAA kuu Askofu wa kanisa katoliki Jimbo la Mbeya Mjini EVARIST CHENGULA amesema kuwa wakati umefika sasa wa wakristo kupendana na pia kuomba amani katika nchi yetu ili matukio mbali mbali yasiweze kutokea.

Askofu Chengula ameongeza kuwa kumekuwepo na matukio mbalimbali ya uvunjifu wa amani katika nchi yetu likiwemo la maandamano yasiyokwisha hivyo wakristo hawana budi kutumia muda huu kupiga magoti na kuomba ili matukio kama haya yasiweze kuendelea kutokea .
GOLIGOTA SEHEMU YESU ALIPO PATA MATESO

Aidha ameongeza kusema kuwa wanasiasa wanatakiwa kuondoa chuki zilizopo kati yao na waangalie amani iliyopo na pia waweze kupendana wao kwa wao ili kuweza kuanya kazi kwa utulivu na si kwa malumbano.

Wakati huohuo katika kanisa la Evanjelist Asembliss of GOD, waumini wametakiwa  kuishi kwa kufuata maadili ya kikristo ili waendane na maisha aliyo ishi bwana Yesu akiwa duniani katika kutafuta kuleta kweli kwa walio potea .
 

Akihubiri katika kanisa la Evanjelist Asembliss of GOD, Mchungaji Mwalongo amewataka waumini hao kutotishika na mambo ya dunia hii kwani kifo cha yesu msalabani kilifungua ukurasa mpya katika maisha ya waaminio kwa roho na kweli


Pia katika ibada iliyoendeshwa na Mwenyekiti wa wilaya ya Mbeya wa kanisa la Moraviani Tanzania  Mchungaji  Swila ametoa pole na pongezi  kwa ujenzi  wa kanisa la moraviani katika ziara yake  ya kutembelea kanisa hilo ijumaa kuu

Katika ibada iliyokuwa ushilika wa lumbila  jijini Mbeya swila amema kuwa dini ni nyingi sana hapa nchini  na duniani kwa ujumla lakini dini ni juhudi za wanadamu  kumtafuta mungu ila kufa kwa yesu ni juhudi za Mungu kuwatafuta   wanadamu.

Aidha Swila amewashauli wakristo kuanza kuchunguza dhambi zilizobakia na kumludia Mungu  na muumini kutafakali alipo na aendapo  na tumaini lake lipo wapi kwaajili ya Yesu  na kuongeza kuwa Yesu ndiye ushindi na uopionyaji kwa kila amwaminiye.