WANYAMA NA MBUGAZETU


Wakati akiwa anamaliza mizunguko ndani ya pori la akiba la Selous hivi karibuni, Mdau Tom alikutana na kundi hili la masikio likiwa linakatisha kwenye runway ya uwanja wa ndege wa Mtemere. walikuwa wametoka kunywa maji mto Rufiji na wakawa wanaelekea kwenye maeneo yao mengine ya kujidai. Barabara inayoonekana ktk taswira ndio njia inayotumia na ndege wakati wa kutua au kupaa ktk kiwanja kidogo cha Mtemere.

Ili kuhakikisha kuwa hali kama hii haihatarishi maisha ya wasafiri kunakuwa na wafanyakazi ambao kazi yao ni kuhakikisha kuwa wanyama kama hawa wanafukuzwa au kuwaarifu marubani kuhusu uwepo wao ktk uwanja. Siku moja nikiwa hapo nilishuhudia mmoja wa wafanyakazi akilazimika kuwatimua swala waliokuwa wanzunguka kwenye hiyo barabara muda ambo ndege ilikuwa imeshakaa tayari kwa kuruka.