Showing posts with label pole. Show all posts
Showing posts with label pole. Show all posts

SALAMU ZA RAMBIRAMBI ZA CCM KIFO CHA MPIGANIA UHURU BI HADIJA BINT KAMBA.


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Kanali mstaafu Abdulrahman Kinana amemtumia salamu za rambi rambi Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es salaam Ndg. Ramadhan Madabida kufuatia kifo cha Muasisi wa TANU Bibi Hadija Bint Kamba, kilichotokea jana tarehe 30 Novemba, 2016 jijini Dar es salaam.

Bibi Hadija Bint Kamba ni miongoni mwa wanaharakati waliopigania uhuru na ukombozi wa Taifa letu. Ameshiriki kuanzisha Baraza la Wanawake Tanganyika mwaka 1955 na baadae Umoja wa Wanawake wa Tanganyika (UWT) tarehe 02 Novemba 1962 akishirikiana na Bibi Titi Mohamed.

Bibi Hadija hakuwahi kushika nafasi za uongozi ndani ya Chama na Serikali baada ya uhuru mpaka mwaka 1985 ambapo Mwalimu Nyerere alimtangaza mbele ya Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM na Baraza la Wazee wa Dar es salaam Diamond Jubilee, kuwa ni mtu aliyetoa mchango mkubwa katika ujenzi wa Chama na Nchi, tangu wakati huo Bibi Hadija Bint Kamba alihudhuria Mikutano mikuu ya Chama kama mjumbe mwalikwa mpaka umri ulipomzuia kuweza kushiriki.
Bibi Hadija Binti Kamba, atakumbukwa na wanachama wa CCM kwa uadilifu, uvumilivu, ujasiri na mchango wake mkubwa katika ujenzi na uimarishaji wa Chama chetu, na kwamba mchango wake katika kupigania uhuru na kuleta ukombozi na maendeleo kwa Wanawake wa taifa hili utaendelea kuenziwa na kuthaminiwa na Watanzania.
Hakika sisi ni wa MwenyeziMungu na kwake yeye ndio marejeo yetu. 
Imetolewa na:- 
                   
Christopher Ole Sendeka (MNEC)
MSEMAJI WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
01.12.2016
Attachments area
Muigizaji Kinyambe Afariki dunia usiku wa leo Mbeya

Muigizaji Kinyambe Afariki dunia usiku wa leo Mbeya

image.jpegMchekeshaji aliyekuwa anakuja juu kwa kasi Mohammed Abdallah "KINYAMBE" amefariki dunia leo usiku huko nyumbani kwao Mbeya.

Mmoja wa wanandugu wa Kinyambe ameithibitisha kuwa, msanii huyo wa filamu ambaye pia alikuwa akijulikana kwa jina la James, amefariki baada ya kuugua kwa siku kadhaa.


Chanzo Jamii Forum 

Kumbukumbu ya Hayati Waziri mkuu Moringe Sokoine

 Rais Mstaafu Mzee Benjamin William Mkapa akimaliza kuweka saini katika kitabu cha Kumbukumbu ya miaka 32 ya kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania Hayati Edward Moringe Sokoine kabla ya Ibada maalumu ya Kumbukumbu ya kifo hicho katika kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam Jumanne April 12, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda alipowasili kuhudhuria Ibada maalumu ya Kumbukumbu ya kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu Hayati Edward Moringe Sokoine  katika kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam Jumanne April 12, 2016

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa na Katibu Mkuu wa TEC Fr. Raymond Saba  alipowasili kuhudhuria Ibada maalumu ya Kumbukumbu ya kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu Hayati Edward Moringe Sokoine  katika kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam Jumanne April 12, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa na mtoto Balozi Joseph Moringe Sokoine  alipowasili kuhudhuria Ibada maalumu ya Kumbukumbu ya kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu Hayati Edward Moringe Sokoine  katika kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam Jumanne April 12, 2016
 Wajane na binti wa   aliyekuwa Waziri Mkuu Hayati Edward Moringe Sokoine  wakiwa katika Ibada Maalumu ya Kumbukumbu ya miaka 32 ya kifo chake katika kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam Jumanne April 12, 2016
 Ibada Maalumu ya Kumbukumbu ya miaka 32 ya kifo chake katika kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam Jumanne April 12, 2016

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Rais Mstaafu Mzee Benjamin William Mkapa wakishiriki katika Ibada ya Kumbukumbu ya miaka 32 ya Kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu Hayati Edward Moringe Sokoine katika kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam Jumanne April 12, 2016
 Sehemu ya waliohudhuria katika Ibada ya Kumbukumbu ya miaka 32 ya Kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu Hayati Edward Moringe Sokoine katika kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam Jumanne April 12, 2016
  Sehemu ya waliohudhuria katika Ibada ya Kumbukumbu ya miaka 32 ya Kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu Hayati Edward Moringe Sokoine katika kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam Jumanne April 12, 2016
  Viongozoi wa taasisi mbalimbali waliohudhuria katika Ibada ya Kumbukumbu ya miaka 32 ya Kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu Hayati Edward Moringe Sokoine katika kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam Jumanne April 12, 2016
   Viongozoi wa taasisi mbalimbali waliohudhuria katika Ibada ya Kumbukumbu ya miaka 32 ya Kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu Hayati Edward Moringe Sokoine katika kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam Jumanne April 12, 2016
   Balozi Joseph Sokoine na viongozoi wa taasisi mbalimbali waliohudhuria katika Ibada ya Kumbukumbu ya miaka 32 ya Kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu Hayati Edward Moringe Sokoine katika kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam Jumanne April 12, 2016
   Sehemu ya watu waliohudhuria katika Ibada ya Kumbukumbu ya miaka 32 ya Kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu Hayati Edward Moringe Sokoine katika kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam Jumanne April 12, 2016
   Sehemu ya watu waliohudhuria katika Ibada ya Kumbukumbu ya miaka 32 ya Kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu Hayati Edward Moringe Sokoine katika kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam Jumanne April 12, 2016
   Sehemu ya kinamama na watoto wao waliohudhuria katika Ibada ya Kumbukumbu ya miaka 32 ya Kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu Hayati Edward Moringe Sokoine katika kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam Jumanne April 12, 2016
   Wanakwaya katika Ibada ya Kumbukumbu ya miaka 32 ya Kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu Hayati Edward Moringe Sokoine katika kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam Jumanne April 12, 2016
 Rais Mstaafu Mzee Benjamin William Mkapa akiongea  machache wakati wa Ibada ya Kumbukumbu ya miaka 32 ya Kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu Hayati Edward Moringe Sokoine katika kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam Jumanne April 12, 2016
  Msemaaji wa familia akiongea  wakati wa Ibada ya Kumbukumbu ya miaka 32 ya Kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu Hayati Edward Moringe Sokoine katika kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam Jumanne April 12, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiongea  machache wakati wa Ibada ya Kumbukumbu ya miaka 32 ya Kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu Hayati Edward Moringe Sokoine katika kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam Jumanne April 12, 2016
 Balozi Joseph Sokoine na wageni wengine wakisiliza hotuba  wakati wa Ibada ya Kumbukumbu ya miaka 32 ya Kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu Hayati Edward Moringe Sokoine katika kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam Jumanne April 12, 2016
 Wageni wakisikiliza hotuba mbalimbali  wakati wa Ibada ya Kumbukumbu ya miaka 32 ya Kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu Hayati Edward Moringe Sokoine katika kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam Jumanne April 12, 2016
 Wageni wakisikiliza hotuba mbalimbali  wakati wa Ibada ya Kumbukumbu ya miaka 32 ya Kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu Hayati Edward Moringe Sokoine katika kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam Jumanne April 12, 2016
 Wageni wakisikiliza hotuba mbalimbali  wakati wa Ibada ya Kumbukumbu ya miaka 32 ya Kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu Hayati Edward Moringe Sokoine katika kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam Jumanne April 12, 2016
 Mzee Kingunge Ngombale Mwiru na mkewe na wageni wengine wakifuatilia yaliyojiri 
Wageni wakisikilizawakati wa Ibada ya Kumbukumbu ya miaka 32 ya Kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu Hayati Edward Moringe Sokoine katika kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam Jumanne April 12, 2016

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam la kanisa Katoliki, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo wakati wa Ibada ya Kumbukumbu ya miaka 32 ya Kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu Hayati Edward Moringe Sokoine katika kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam Jumanne April 12, 2016
 Katibu Mkuu wa TEC Fr. Raymond Saba  akiongea wakati wa  Ibada maalumu ya Kumbukumbu ya kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu Hayati Edward Moringe Sokoine  katika kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam Jumanne April 12, 2016
 Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam la kanisa Katoliki, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo akiongea wakati wa Ibada ya Kumbukumbu ya miaka 32 ya Kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu Hayati Edward Moringe Sokoine katika kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam Jumanne April 12, 2016

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Rais Mstafu Mzee Benjamin William Mkapa wakifurahia jambo wakati wa hotuba ya Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam la kanisa Katoliki, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo wakati wa Ibada ya Kumbukumbu ya miaka 32 ya Kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu Hayati Edward Moringe Sokoine katika kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam Jumanne April 12, 2016
 Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam la kanisa Katoliki, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo na Katibu Mkuu wa TEC Fr. Raymond Saba wakiwapa mikono familia ya Marehemu wakati wa Ibada ya Kumbukumbu ya miaka 32 ya Kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu Hayati Edward Moringe Sokoine katika kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam Jumanne April 12, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwapa mikono familia ya Marehemu wakati wa Ibada ya Kumbukumbu ya miaka 32 ya Kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu Hayati Edward Moringe Sokoine katika kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam Jumanne April 12, 2016

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwapa mikono wajane wa  Marehemu wakati wa Ibada ya Kumbukumbu ya miaka 32 ya Kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu Hayati Edward Moringe Sokoine katika kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam Jumanne April 12, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Rais Mstafu Mzee Benjamin William Mkapa  wakiwapa mikono wajane wa  Marehemu wakati wa Ibada ya Kumbukumbu ya miaka 32 ya Kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu Hayati Edward Moringe Sokoine katika kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam Jumanne April 12, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisi dikizwa na Balozi Joseph Moringe Sokoine baada ya Ibada ya Kumbukumbu ya miaka 32 ya Kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu Hayati Edward Moringe Sokoine katika kanisa la Mtakatifu Joseph jijini Dar es salaam Jumanne April 12, 2016.
PICHA NA IKULU

Aliye oa wanaum wawili afariki dunia

MKAZI wa Kijiji cha Ikondamoyo, Wilaya ya Mlele mkoani Katavi, Veronica Salehe (54), aliyeoa wanaume wawili kwa kipindi cha miaka tisa amefariki dunia.

Akizungumza na waandishi wa habari juzi, Mwenyekiti wa Kitongoji cha Ikondamoyo, John Maganga, alisema Veronica alifariki dunia wiki iliyopita mkoani Tabora alikokuwa amekwenda  kupatiwa matibabu kwa kaka yake.

Maganga alisema kuwa ndoa hiyo iliwezeshwa na mume mkubwa ambaye alikubali kuishi na mume mdogo.

Alisema kuwa Veronica ndiye aliyewaoa wanaume wote wawili na kuishi nao kwa miaka tisa, na kwamba ndiye aliyekuwa na amri kuu katika nyumba yao.

Aliwataja wanaume hao kuwa ni Paulo Sabuni (62) ambaye ndiye mume mkubwa na Arcado Mlele (47).

Maganga alisema Veronica na mume wake mkubwa, walifika kijijini hapo miaka 24 iliyopita wakitokea Kijiji cha Usumbwa, mpakani mwa Chunya na Tabora.

“Baada ya kufika kijijini hapa, walianza kujishughulisha na shughuli za kilimo na biashara ya kuuza pombe za kienyeji aina ya komoni,” alisema Maganga.

Katika uhai wake, Veronica alibahatika kupata watoto wanne, kati yao wawili wa kike.

Maganga alisema mtoto mdogo wa kiume, ni wa mume mdogo ambaye ana miaka tisa, anayesoma darasa la nne katika Shule ya Msingi Ikondamoyo, na watoto wengine watatu ni wa mume mkubwa.

Kuhusu maisha ya Veronica ya kuishi na wanaume wawili, Maganga alisema haikuwa siri kijijini hapo kwa sababu walizoeleka kwa wanakijiji.

Alisema mume mdogo alikuwa anaishi kwenye nyumba aliyoachiwa na marehemu baba yake, lakini alikuwa akishinda kwa mume mkubwa ambako kulijulikana zaidi kwa jina la ‘nyumba kubwa’.

“Mambo ya kula, kunywa na mengine, mama   alikuwa akiwapangia zamu kama afanyavyo mume mwenye wake wengi,” alisema Maganga na kuongeza kuwa wanaume hao walikuwa wanaridhika na kufurahia maisha.

Alisema siku mama akichoka kupika, mume mdogo alikuwa akiingia jikoni na kuwaandalia chakula watoto na mume mkubwa maji ya kuoga.

Wakati wa mazishi, wanaume wote walishiriki shughuli zote, jambo ambalo limeacha maswali mengi kwa jamii.

Akizungumzia msiba huo, mume mkubwa alisema kuwa amepata pigo kubwa kwa sababu alikuwa anasaidiwa mno na marehemu Veronica kutokana na biashara zake za pombe za kienyeji ambazo zilisaidia kuendesha maisha ya kila siku.

“Veronica aliugua muda wa miezi miwili, nilikuwa namplekea Kituo cha Afya Urwila kupata matibabu, lakini Mungu kampenda zaidi,” alisema.
TAMKO LA SERIKALI YA TANZANIA KIFO CHA MWANAFUNZI HUKO INDIA HILI HAPA

TAMKO LA SERIKALI YA TANZANIA KIFO CHA MWANAFUNZI HUKO INDIA HILI HAPA



Waziri Mahiga ametoa ufafanuzi huo leo bungeni, na kuthibitisha ni kweli wanafunzi hao wamefanyiwa vitendo hivyo, ambavyo watanzania walikuwa wanavisikia bila kuwa na taarifa rasmi.
“Wananchi wa India walichoma gari lake, na punde kidogo gari lingine lilifuata likiwa na wanafunzi wanne watanzania, mmoja msichana na watatu wavulana, walilisimamisha lile gari na kuwavuta wale wanafunzi nje, na wakamchukua yule msichana na kumvua nguo na kuanza kumtembeza barabarani uchi, wale wavulana walipigwa na gari lao lilichomwa, katika gari lile kulikuwa na simu zao na documents mbali mbali nazo ziliteketea”, alisema waziri Mahiga.

Waziri Mahiga aliendelea kwa kusema kuwa baada ya hapo askari wa India walifika lakini hawakuonyesha ushirikiano wa kutosha, lakini wanafunzi hao walipelekwa hospitali na kupatiwa matibabu ya majeraha waliyokuwa nayo, lakini walilazimika kuondoka mapema kwa kuwa hawakuwa na pesa.

“Baada ya hapo ubalozi wetu wa India uliandika dokezo la kidiplomasia kwa serikali ya India, ikilaani kitendo hicho na kuitaka serikali ya india ichukue hatua za kisheria na haraka katika kupeleleza kufuatia matukio hayo, na waziri wa mambo ya nchi za nje wa India, alitoa taarifa rasmi kule New Delhi,kwanza kuomba radhi kwa Tanzania na watanzania walioko India kwa kitendo hicho kilichotokea, akaagiza serikali yake ichukue hatua za kisheria na kupeleleza na kukamata wale waliohusika, na wote sasa wamekamatwa na wamepelekwa mahakamani”, alisema Waziri Mahiga.

Pamoja na Hayo Waziri Mahiga alisema serikali India iliagiza kwamba wanafunzi wa Tanzania wapewe ulinzi maalum kule wanakoishi na kusindikizwa pale wanapokwenda masomoni au madarasani , na tatu serikali ya India ilimtaka balozi wetu afuatane na maafisa waandammizi wa wizara ya mambo ya nchi za nje ya India mjini Bangalow, ili kukutana na wanafunzi wa Tanzania na wengine wa Afrika, na kuweka mahusiano mazuri kati ya wananfunzi na wenyeji katika mji huo.

Pia Waziri Mahiga alitoa taarifa rasmi juu ya kifo cha mwanafunzi mwingine Mtanzania nchini humo, na kusema mwanafunzi huyo hakufariki kwenye tukio hilo la uvamizi, bali alipata ajali ya pikipiki iliyosababisha kifo chake.

“Nilielezwa kwamba kuna mwanafunzi mmoja ambaye amefariki karibu na maeneo hayo hayo , taarifa za awali zilikuwa zinatatanisha wakadhani kifo hicho kilitokana na tukio hilo la kuvamiwa wanafunzi wetu, lakini si kweli, mwanafunzi huyo mtanzania alikuwa anaendesha piki piki bila kofia, akaenda kugonga nguzo ya taa na kufariki pale pale, ubalozi wetu unashughulikia mazishi na mwili wake utarudishwa Tanzania mapema iwezekanavyo.

Tukio hilo limeingia siku ya tatu sasa tangu kutokea kwake nchini India, ambapo kumeibuka hisia tofauti tofauti miongoni mwa watanzania, na kuwatia hofu wanafunzi wanaosoma nchini humo.

MTANZANIA MWANAFUNZI MWINGINE AFARIKI INDIA LEO HII ..KIFO CHAKE CHAZUA UTATA BARABARANI








Taarifa kutoka TASABA, 
UONGOZI WA TASABA. Kupitia rais Prosper Mwakitwange.
Unatangaza ya kuwa kulingana, na taarifa za msiba,ni kwamba tupo katika legal process za kukabithiwa mwili wa ndugu yetu, ambapo tunataraji kufanikisha Leo. Na baadae tutatangaza process zinazofuatia nikifanikiwa, na balozi ambaye kwa sasa yupo Bangalore, nitawatangazia hatua tuliofikia na muwajulisha wapi na mahali tutakutana, naomba mjitaarishe tukiwajulisha mfike bila ya kukosa. 
Mungu ibariki TASABA,
MUNGU Ibariki Tanzania.


: TAARIFA ZA MSIBA, 
UONGOZI WA TASABA.
Unasikitika kutangaza MSIBA wa Mwanachama na Mwanafunzi mwezetu, CHRISTIAN BENJAMIN MUTANDIS, alikuwa anasoma Koshys College, second year, BCA course. Kilichotokea jioni ya Leo, kwa ajali ya pikipiki.
Taratibu za kuuwaga mwili,ibada na misa na sala fupi tutatangaza kesho Taratibu zote na mahali tutapokutana pamoja na kuuwaga mwili.
Tunawaomba tushirikiane kwenye kipindi hichi kigumu na familia yake. 
Bwana ametoa na Bwana ametwa, 
Jina lake lihimidiwe.

Kategori

Kategori