Showing posts with label WALEMAVU. Show all posts
Showing posts with label WALEMAVU. Show all posts

MAADHIMISHO YA SIKU YA ULEMAVU DUNIANI YALIKUWA HIVI KATIKA KITUO CHA CHILDREN SUPPORT TANZANIA CHA MBEYA


Mgeni rasmi toka benki ya NMB akikata utepe kuzindua uwanja wa michezo wa kituo hicho
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo hicho Noela Msuya amesema katika maadhimisho ya Ulemavu duniani watanzania wanapaswa kutowatenga watoto wenye ulemavu kwa kuwa hakuna eneo wala kijiji kilichotengwa kwa ajili ya watu wenye ulemavu bali tunatakiwa kuishi nao pamoja.
Mwalimu Mkuu wa Kituo hicho, Omoding James amesema kituo kilianza kupokea watoto tangu mwaka 2009 baada ya kusajiliwa kikiwa na watoto 13 lakini hadi sasa kuna watoto zaidi ya 200.
Mtoto Maxel mlemavu wa mikono na miguu nae akiwa katika vazi rasmi la mahafali ya kumaliza Darasa la awali kuingia darasa la kwanza

Kituo cha kulelea na kufundishia watoto cha Children Support Tanzania kilichopo Block T Jijini Mbeya kimeungana na Ulimwengu mzima katika kuadhimisha siku ya Ulemavu Duniani inayoadhimishwa kila tarehe 3 Disemba kwa kuzindua uwanja wa mazoezi na mahafali ya Chekechea.

Aidha kituo hicho kimetumia siku hiyo kwa kusheherekea mahafali ya watoto 15 ambao wanavuka hatua kutoka Chekechea tayari kwa kujiunga na Darasa la Kwanza mwakani baada ya kupata sifa za kujua kusoma na kuandika.

Katika Sherehe hizo zilizofanyika katika Viwanja vya kituo hicho zilizohudhuriwa na wazazi wa wanafunzi wanaosoma hapo pia umezinduliwa uwanja wa mazoezi unaofahamika kwa jina la CST Fun Village ambao utakuwa na michezo mbali mbali ya watoto.

Akizungumza katika Sherehe hizo Mwalimu Mkuu wa Kituo hicho, Omoding James amesema kituo kilianza kupikea watoto tangu mwaka 2009 baada ya kusajiliwa kikiwa na watoto 13 lakini hadi sasa kuna watoto zaidi ya 200.

Amesema kituo hicho kinapokea watoto wenye ulemavu wa akili, Viungo,viziwi, wanaoishi katika mazingira magumu na watoto wa kawaida ambapo wanafundishwa elimu maalumu ya darasani, ufundi, mziki na michezo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo hicho Noela Msuya amesema katika maadhimisho ya Ulemavu duniani watanzania wanapaswa kutowatenga watoto wenye ulemavu kwa kuwa hakuna eneo wala kijiji kilichotengwa kwa ajili ya watu wenye ulemavu bali tunatakiwa kuishi nao pamoja.

Amesema kauli mbiu ya Siku ya walemavu Duniani inasema, “Vunja vizuizi, fungua milango kwa jamii jumuishi kwa maendeleo kwa wote”ambayo inapaswa kuenziwa kwa kuwajengea mazingira ya kuwapenda walemavu na kuwashirikisha katika shughuli za kiuchumi.

Na Mbeya yetu

WALEMAVU WAJENGEWE UWEZO WA KUJITEGEMEA

JAMII imetakiwa kutowaficha watu wenye ulemavu bali iwajengee uwezo wa kufanya kazi kwa kuwatengea maeneo na siyo kuwaacha wakiwa omba omba mitaani na wengine kufungiwa majumbani.

 Mlemavu wa Viungo, Damas Sanga(48) mkazi wa Igurusi Wilayani Mbarali Mkoa wa Mbeya wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukutwa akiomba msaada katika baadhi ya Ofisi Mkoani Jijini hapa.



JAMII imetakiwa kutowaficha watu wenye ulemavu bali iwajengee uwezo wa kufanya kazi kwa kuwatengea maeneo na siyo kuwaacha wakiwa omba omba mitaani na wengine kufungiwa majumbani.
Rai hiyo imetolewa jana na Mlemavu wa Viungo, Damas Sanga(48) mkazi wa Igurusi Wilayani Mbarali Mkoa wa Mbeya wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukutwa akiomba msaada katika baadhi ya Ofisi Mkoani Jijini hapa.
Sanga alisema si kila mlemavu anastahili kubweteka na kusubiri kupewa misaada na kuomba omba mitaani bali wengine wanauwezo wa kufanya kazi za ujasiliamali kutokana na kuwa na uwezo mkubwa wa kiakili.
Alisema hivi sasa yeye binafsi anauwezo wa kufanya kazi ya ufundi vyuma hivyo ameamua kuomba msaada ili aweze kununua baadhi ya vifaa vitakavyomsaidia katika kazi yake hiyo ili aondokane na kuwa tegemezi kwa kujitafutia riziki yake yeye mwenyewe.
Alivitaja baadhi ya vifaa vinavyohitajika kuwa ni pamoja na Jenereta kubwa, Inveta na Kabwe kwa ajili ya shughuli ya kuchomelea vitu vinavyogharimu Shilingi 390,000 ambapo hadi sasa amefanikiwa kupata shilingi 290,000 alizochangiwa na wasamaria wema hivyo kubakiwa na Shilingi 100,000/= tu.
Mjasiliamali huyo mwenye ulemavu wa miguu alisema hivi sasa anafamilia ya mke mmoja na watoto wanne ambao hawezi kuwahudumia bila kuwa na kazi ya kumwingizia kipato na ndiyo maana anaomba msaada ili aweze kuendesha shughuli zake na kujipatia kipato kitakachoweza kuhudumia familia.
Alisema kwa mtu yeyote atakayeguswa na hali yake awasiliane naye kwa simu namba  0764 036150  au afike nyumbani kwake Shule ya Msingi Igurusi Wilayani Mbarali Mkoani hapa kwa msaada wa hali na mali.

Na Mbeya yetu

Kategori

Kategori