Showing posts with label Vodacom. Show all posts
Showing posts with label Vodacom. Show all posts

Mshindi wa Jaymillions na mafanikio yake: Ajenga nyumba ya kisasa na kuishi na familia yake goba, kufungua biashara


Mmoja ya washindi wa kitita cha shilingi Milioni 100 kupitia promosheni ya Jaymillions iliyokuwa inaendeshwa na Vodacom Tanzania iliyomalizika mwezi Aprili mwaka huu Irene Mrema, amesema tangu aibuke na ushindi amepata mafanikio makubwa mojawapo ikiwa ni kuweza kujenga nyumba ya kuishi na familia yake maeneo ya Goba nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam. 
“Nashukuru Mwenyezi Mungu kwa kunikwamua kimaisha kupitia Jaymillion ya Vodacom kwa kuwa imeleta mafanikio makubwa katika maisha yangu na familia yangu kwa kuwa imetuwezesha kujenga na kumiliki nyumba nzuri ya kisasa ambayo tayari tumehamia pamoja na familia yangu”alisema. 
Mbali na ujenzi wa nyumba hiyo Irene Mrema alieleza kuwa hivi anajipanga kufungua biashara ambayo bado anaifikiria kwa fedha alizosalia ili kuwezesha kukuza kipato cha familia 
“Natarajia kufungua biashara katika siku za hivi karibuni kwa ajili ya kuniwezesha kijitegemea na kuongeza kipato cha familia” 
Aliishukuru kampuni hiyo kwa kubuni promosheni zenye kuboresha maisha ya wateja wake na kuongeza kuwa fedha hizo alizoshinda zimeweza kusaidia katika mambo mbalimbali ya kijamii na akifungua biashara atatoa ajira kwa wafanyakazi ambao nao watanufaika na ushindi wake. 
”Mafanikio haya ambayo yanaonekana kwangu kama ndoto ukimwelezea mtu anaweza akashindwa kuamini hususani wale ambao wanakuwa na dhana kuwa promosheni za makampuni kwa wateja kama ilivyokuwa Jaymillion ni za uongo lakini napenda kuwahakikishia kwamba hakuna uongo,upendeleo wala kujuana bali ni bahati ya mtu na akishinda anapewa fedha zake kama ilivyotokea kwangu”,alisema Irene kwa furaha. 
 Naye Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu ambaye alifanya ziara ya kufuatilia maendeleo ya washindi wa promosheni hiyo alisema amefurahishwa na hatua aliyofikia mshindi huyo ya kupiga hatua ya kimaendeleo kimaisha. 
“Kwetu Vodacom mafanikio haya ya mteja ni faraja kubwa kwa kuwa mbali na kutoa huduma bora na kubuni huduma za kurahisisha maisha ya wateja pia ni kufanya maisha ya wateja wetu kuwa murua kupitia promosheni zetu”, alisema Nkurlu. 
 Alisema promosheni za kukwamua maisha ya wateja zikiwa na tija na kuleta mafanikio kwa wateja zinahamasisha kampuni kuendelea kubuni promosheni zingine ili ziweze kubadilisha maisha ya wateja wengi zaidi 
Alimalizia kwa kuwataka wateja wa mtandao huo kuchangamkia fursa mbalimbali zinazotolewa na kampuni hiyo na zitakazokuwepo katika siku za usoni.
 Irene Mrema aliyekuwa mmoja wa washindi wa kitita cha shilingi Milioni 100 kupitia promosheni ya Jaymillions iliyokuwa ikiendeshwa na Vodacom Tanzania(kushoto) akimwelezea Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo,Matina Nkurlu(kulia)alipomtembelea nyumbani kwake kujua maendeleo ya mafanikio aliyoyapata baada ya ushindi wake likiwemo la kumalizia nyumba ya kisasa anayoishi na familia yake maeneo ya Goba  jijini Dar es Salaam.
Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(kushoto)akisalimiana na Irene Mrema aliyekuwa mmoja wa washindi wa kitita cha shilingi Milioni 100 kupitia promosheni ya Jaymillions iliyokuwa ikiendeshwa na kampuni hiyo,Alipomtembelea nyumbani kwake kujua maendeleo ya mafanikio aliyoyapata baada ya ushindi wake likiwemo la kumalizia nyumba ya kisasa anayoishi na familia yake maeneo ya Goba  jijini Dar es Salaam.
Nyumba ya Irene Mrema anayoishi na familia yake Goba jijini Dar es Salaam aliyomalizia kuijenga baada ya kukabidhiwa kitita chake cha shilingi Milioni 100 alichojishindia mwezi wa Nne kupitia promosheni ya Jaymillions iliyokuwa ikiendeshwa na Vodacom Tanzania.

MAWAKALA WA VODACOM TANZANIA WAPIGWA MSASA KUTOA HUDUMA BORA KWA WATEJA


 Mkuu wa Kitengo cha M-Pesa wa Vodacom Tanzania, George Kagaruki akitoa mafunzo kwa Mawakala wa M-Pesa wa kanda ya Mbagala jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Wakati wa Semina iliyoandaliwa na Kampuni hiyo kwa ajili ya mawakala hao kujifunza jinsi ya kutoa na kuboresha huduma  za kifedha, kuepukana na  udanganyifu wa kifedha na jinsi ya  kupata faida zaidi kwa kuuza Vodafasta (muda wa hewani) na kuunganisha wateja wa kampuni hiyo kwa kutumia huduma ya M-Pawa.
 Wakufunzi wa Semina ya Mawakala wa Vodacom Tanzania, kanda ya Mbagala jijini Dar es Salaam wakiwa kwenye Semina iliyoandaliwa na Kampuni hiyo kwa ajili ya mawakala hao kujifunza jinsi ya kutoa na kuboresha huduma za kifedha, kuepukana na  udanganyifu wa kifedha na jinsi ya  kupata faida zaidi kwa kuuza Vodafasta (muda wa hewani) na kuunganisha wateja katika huduma ya M-Pawa.
 Mkufunzi wa Semina ya Mawakala wa Vodacom Tanzania, kanda ya Mbagala jijini Dar es Salaam, John Mahingwa akiuliza swali wakati wa Semina hiyo iliyoandaliwa na Kampuni hiyo kwa ajili ya mawakala hao kujifunza jinsi ya kutoa na kuboresha huduma za kifedha, kuepukana na  udanganyifu wa kifedha na jinsi ya  kupata faida zaidi kwa kuuza Vodafasta (muda wa hewani) na kuunganisha wateja katika huduma ya M-Pawa.
  Meneja Mauzo wa Vodacom Tanzania, Kanda ya Mbagala jijini Dar es Salaam, akifafanua jambo kwa Mawakala wa kampuni hiyo waliohudhuria katika Semina  iliyoandaliwa na Kampuni hiyo kwa ajili ya mawakala hao kujifunza jinsi ya kutoa na kuboresha huduma za kifedha, kuepukana na  udanganyifu wa kifedha na jinsi ya  kupata faida zaidi kwa kuuza Vodafasta (muda wa hewani) na kuunganisha wateja katika huduma ya M-Pawa.

Burudani za Vodacom zaleta furaha Pasaka Dar


Mshinda wa kitita cha shilingi milioni 10/- kupitia promosheni ya Jaymillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania Shamila Ramadhani(kushoto)akikabidhiwa hundi yake na Balozi wa promosheni hiyo Hillary Daud ‘JayMillions’ baada ya kuipuka mshindi wa kitita hicho kupitia promosheni hiyo katikati ni mume wa mshindi huyo Abdallah Mahoka.Makabidhiano hayo yalifanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Dar Live wakati wa Tamasha la Mwana Dar Live lililofanyika Mbagala jijini Dar es Salaam.Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno JAY au AUTO kwenda namba 15544.
Balozi wa promosheni ya Jaymillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania Hillary Daud ‘Jaymillions’akiwasomea tarakimu kwenye hundi iliyokuwa na thamani ya shilingi milioni 10/-wakazi wa mbagala waliofika katika tamasha la Mwana Dar live lililofanyaika katika ukumbi wa Dar live mbagala jijini Dar es Salaam katika kuadhimisha sikukuu ya pasaka,Hundi hiyo ilikabidhiwa kwa mshindi wa promosheni hiyo Shamila Ramadhani(kusho)akiambatana na mumewe Abdallah Mahoka(katikati) Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno JAY au AUTO kwenda namba 15544.
Mshinda wa kitita cha shilingi milioni 10/- kupitia promosheni ya Jaymillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania Shamila Ramadhani(kushoto)pamoja na mumewe Abdallah Mahoka wakiinua hundi yao juu ili wakazi wa mbagala waliohudhuria tamasha la Mwana Dar Live waione baada ya kukabidhiwa rasmi na Balozi wa promosheni hiyo Hillary Daud(hayupo pichani) baada ya kuipuka mshindi wa kitita hicho kupitia promosheni hiyo.Makabidhiano hayo yalifanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Dar Live wakati wa Tamasha hilo lililofanyika Mbagala jijini Dar es Salaam.Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno JAY au AUTO kwenda namba 15544.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Ali Kiba akiwapagawisha washabiki wa muziki wake waliofurika katika Tamasha la Mwana Dar Live lililodhamini na Vodacom Tanzania, Katika kuadhimisha sikukuu ya pasaka na kufanyika katika ukumbi wa Dar Live Mbagala jijini Dar es Salaam.
Mamaa Aisha Mashauzi akitumbuza muziki wa Taarabu katika Tamasha la Mwana Dar Live lililodhamini na Vodacom Tanzania, Katika kuadhimisha sikukuu ya pasaka na kufanyika katika ukumbi wa Dar Live Mbagala jijini Dar es Salaam.
Msanii wa nyimbo za mchiriku Sueleman Jabiri”Msaga Sumu”akisaga sumu ipasavyo kwa washabiki wa muziki wake wakati wa Tamasha la Mwana Dar Live lililodhamini na Vodacom Tanzania, Katika kuadhimisha sikukuu ya pasaka na kufanyika katika ukumbi wa Dar Live Mbagala jijini Dar es Salaam.

Wapenzi wa burudani  ya muziki wa kizazi kipya na muziki wa taarabu wamepata burudani ya kusherehekea sikukuu ya Pasaka  kutoka kwa magwiji wa muziki wa kizazi kipya  na taarabu katika matamasha ya burudani yaliyoandaliwa na kudhaminiwa na  Vodacom Tanzania yaliyofanyika Coco Beach na Dar Live ,Mbagala jijini Dar es Salaam.

Tamasha la wazi lililofanyika Coco beach liliwavutia wakazi wengi wa jiji hususani vijana pia kuhakikisha watoto hawaachwi nyuma nao waliandaliwa burudani zao ambapo waliweza kucheza na kufurahia sikukuu ya Pasaka.

Wasanii wa kizazi kipya Bob Junior na  Shilole waliacha historia ya aina yake kwa mamia ya washabiki wa muziki wa kizazi kipya waliofika katika fukwe ya Coco kwa jinsi walivyoweza kukonga nyoyo zao na kudhihirisha kuwa muziki wao ni wa kiwango cha juu pia walikuwepo wasanii mbalimbali chipukizi ambao pia walimwaga burudani kwa mashabiki.

Funga kazi ilikuwa Dar live Mbagala ambapo msanii mahiri wa Bongofleva Ali Kiba kwa kushirikiana na mwanamama anayetamba katika muziki wa taarabu nchini Aisha Mashauzi walimwaga burudani za aina yake na kupagawisha washabiki waliofika katika tamasha la Mwana Dar Live ukumbini hapo kusherehekea sikuu ya Pasaka.

Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu amesema kuwa  kampuni yao imeamua kuandaa na kudhamini matamasha haya  kwa ajili ya kuwapatia furaha na burudani wateja wake na  wananchi kwa ujumla katika msimu huu wa sikukuu ya Pasaka na  kuweza kuwakutanisha washabiki na wanamuziki wawapendao na itaendelea kufanya hivyo kupitia promosheni ya Ishi Kistaa na aliwakumbusha wateja kutuma neno STAR kwenda namba 15670 ili wapate fursa ya kuwakutanisha na wasanii wawapendao.

“Kama ilivyo kauli mbiu yetu kuwa “ukiwa na Vodacom maisha ni murua”tunahakikisha mbali na kutoa huduma bora kwa wateja wetu pia tunajua kuwa kuna muda wanahitaji kufurahi kwa burudani hivyo ndio maana tunaandaa na kudhamini matamasha ya  aina hii na tutaendelea kufanya hivyo siku zote ikiwa ni moja ya njia ya kusema ahsante kwa wateja wetu kwa kutuunga mkono”Alisema.

Vodacom yaja na huduma ya Vinjari na M-Pesa

 

Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia(katikati)akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani)wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Vinjari na M PESA itakayowawezesha wateja wa mtandao huo kufanya malipo ya huduma katika sekta ya usafiri wa anga,mahoteli na utalii kwa njia ya kieletroniki huduma hiyo inapatikana kupitia tovuti ya vinjari,Wengine katika picha maafisa waandamizi wa tovuti ya vinjari kushoto ni Manase Banduka Mkurugenzi wa Uendeshaji,kulia Mkurugenzi Mtendaji Andrew Mboma.
Mkurugenzi Mtendaji wa tovuti ya Vinjari Andrew Mboma(kulia)akifafanua jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani)wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Vinjari na M PESA itakayowawezesha wateja wa Vodacom Tanzania kufanya malipo ya huduma katika sekta ya usafiri wa anga,mahoteli na utalii kwa njia ya kieletroniki huduma hiyo inapatikana kupitia tovuti ya vinjari, Wengine katika picha Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Rosalynn Mworia(katikati) kushoto ni Manase Banduka Mkurugenzi wa Uendeshaji.
Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia(kushoto)akipongezana na maafisa waandamizi wa tovuti ya vinjari (katikati ) Manase Banduka Mkurugenzi wa Uendeshaji,(kulia )Mkurugenzi Mtendaji wa tovuti hiyo Andrew Mboma wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Vinjari na M PESA itakayowawezesha wateja wa Vodacom kufanya malipo ya huduma katika sekta ya usafiri wa anga,mahoteli na utalii kwa njia ya kieletroniki huduma hiyo inapatikana kupitia tovuti hiyo.

Katika kuzidi kurahisisha huduma za malipo  wakati tukielekea msimu wa sikukuu za Krismas na Mwaka Mpya,kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania leo imezindua huduma mpya ya kufanya malipo kwa njia ya kielektroniki.

Huduma hii mpya inayozinduliwa leo inajulikana kama Vinjari na M-Pesa ambayo itawawezesha wateja wa Vodacom kufanya malipo ya huduma katika sekta ya usafiri wa ndege na utalii kwa njia ya kieletroniki kama ambavyo yamekuwa yakifanyika kwa kutumia kadi mbalimbali za kufanyia malipo kimataifa.

Akiongea wakati wa uzinduzi wa huduma hii Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia amesema huduma hii kwa kuanzia itafanyika kwa kushirikiana na mtandao wa malipo ya kieletronikali nchini ujulikanao kama Vinjari.co.tz ambao unafanya kazi na zaidi ya taasisi 300 za kutoa huduma yakiwemo  mahoteli ya utalii na makampuni mbalimbali yanayotoa huduma hususani za  masuala ya utalii na sehemu za mapumziko na burudani.

“Kadri siku zinavyozidi kusonga mbele tunazidi kushuhudia mapinduzi makubwa ya kiteknolojia hususani katika masuala ya biashara, Vodacom tumeona umuhimu wa kuanzisha huduma hii ili kuwawezesha wateja wetu kufanya miamala yao kwa njia ya kieletroniki kupitia huduma ya M-Pesa ili kwenda na wakati zaidi. Kwa kuanzia tutatoa huduma hii kupitia mtandao  mpana  wa malipo ya kielektronoki wa vinjari.co.tz na kadri siku zitakavyosonga mbele tutazidi kuboresha huduma hii,” alisema.

Aliongeza kuwa Vodacom inaelewa kuwa idadi kubwa ya Watanzania hawana kadi za kimataifa za kufanya miamala ya malipo kwa njia ya kielekroniki ndio maana imekuja na huduma hii ikiwa inawalenga wateja wetu wanaotumia  huduma ya M-Pesa.

Naye Mkurugenzi wa Vinjari.com,Andrew Mboma amesema ili kupata huduma hii mteja anaingia katika sehemu ya kawaida ya kufanya miamala ya M-Pesa kwenye simu yake atakuta sehemu inayomuelekeza jinsi ya kupata huduma kupitia Vinjari na M-Pesa ambapo ataweza kufanya muamala kwa kadri  ya huduma atakayokuwa anahitaji na atakatwa fedha kutoka akaunti yake ya M-Pesa kulipia huduma hiyo na malipo kidogo ya kutumia huduma hiyo. Maelezo zaidi yanapatikana kwa kutembelea tovuti ya vinjari.co.tz

Katika miaka ya karibuni kumekuwepo na ongezeko kubwa la matumizi ya simu za mkononi nchini ambapo pia kumekuwemo na ongezeko la watumiaji wa mtandao wa internet.

Inakadiriwa kuwa zaidi ya watanzania milioni 28 wanatumia huduma za simu za mkononi ambapo zaidi ya watanzania milioni 6 wanatumia huduma za internet.

Kategori

Kategori