Showing posts with label Vituko Duniani. Show all posts
Showing posts with label Vituko Duniani. Show all posts

Video: Wema Sepetu, Jackline Wolper, Bosi wa GSM ndani ya China kunani?

Kwenye Instagram zao mastaa hao wamepost waki safiri toka dar siku moja na wote wamepost picha wakiwa dubai same day then wote wamepost wakiwa china same place Canton Kama Picha zinavyoonesha Location ila hawajapiga picha pamoja.. Ambapo mdogo wa GSM counselor Salaah amepost akiwa Canton fair na wema na wolper wakipost wakiwa canton railway station same area ila wamekuwa makini kutopiga picha pamoja au labda hawafahamiani. Au labda ma baby wao idriss na harmonize ndo wamegharamia safari yao ya china.. Au labda yule MCM aliyempost kawasponso

Tazana Video Hapa chini






Video: Mrembo Atinga Global Afichua Siri Za ‘Scorpion’


Mrembo aitwaye Talta Msofe (21) akiwa katika pozi baada ya kutinga katika ofisi za Global Publishers kufichua siri za mtuhumiwa huyo, Salum Njwete ‘Scorpion’, mkazi wa Yombo Machimbo jijini Dar es Salaam.

Tazama hapa video Akifunguka 





Nyoka 'watoroka' katika shamba China

Nyoka 'watoroka' katika shamba China



cobra

Maafisa mashariki mwa China wanawasaka zaidi ya nyoka 50 aina ya swila (cobra kwa Kiingereza) waliotoweka kutoka shamba la nyoka linaloendeshwa bila ya kibali .
Zaidi ya nyoka 200 walitoweka kutoka shamba hilo mnamo Agosti mwaka huu. Wafugaji nyoka katika shamba hilo wameambia polisi kwamba walikuwa wanajaribu kuwasaka nyoka hao waliotoroka pasi kuwaarifa maafisa wa eneo hilo.
Tatizo hilo lilidhirika kwa umma baada ya swila mmoja kuonekana na kuwashutusha wakaazi katika shamba jingine kwenye eneo la karibu.
Serikali ya eneo hilo inajaribu kuwahakikishia wakaazi kuwa wana dawa za kutosha za kukata sumu ya nyoka hao iwapo wakaazi wataumwa kabla ya nyoka wote kupatikana.

Nyoka atafuta 'joto' kwenye kiatu huko Australia

Image copyright

Nyoka mwenye sumu kali atafuta 'joto' kwenye kiastu Australia 
Mwanamke wa Australia amewaita maafisa wa wanyama pori kumtoa nyoka wa urefu wa mita 1 mwenye sumu kali kutoka kwenye kiatu chake.
Mnasa nyoka Rolly Burrell alimdhibiti nyoka huyo wa rangi ya chokoleti aliyekuwa anatafuta ''joto'' nyumbani mwa mwanamke huyo Adelaide, kusini mwa Australia.
Alikuwa ametoka nje ya nyumba yake iliopo mashambani kukusanya viatu vyake na hapo akaona mkia ukipotea ndani ya kiatu chake kimoja.
Nyoka huyo ni mmoja wa wanaoonekana kuwa wenye sumu kali duniani na hupatikana katika pwani na maeneo ya ndani ya ardhi kavu Australia.
"Alitoka nje kuchukua viatu vyake na akaona kitu kikitoweka kwa kasi," Burrell ameiambia BBC.
"Aligundua kuwa ni nyoka."
Nyoka huyo ambaye ni aina inayopenda kujificha, alichiliwa msituni kando na mbali na maenoe ya makaazi ya watu .
Bwana Burrell amesema kampuni yake iliitwa kwa mara nyengine kutoa nyoka kwenye kiatu takribana mwaka mmoja uliopita.
Viatu hivyo aina ya buti, vimetengenezwa kwa ngozi ya kondoo, na hutumika sana Australia, Huwana joto zuri wakati wa msimu wa baridi, pengine ndio sababu iliomvutia nyoka huyo.
"Ndio wanaanza kuamka kutoka usingizini," Bwana Burrell anasema.
"Msimu wao wa kujamiiana umeanza kwa hivyo wanatafuta joto na wana njaa."

Kategori

Kategori