Showing posts with label Rwanda. Show all posts
Showing posts with label Rwanda. Show all posts
Paul Kagame anarudi Madarakani mwaka 2017? Hii hapa kutoka Mahakamani Rwanda..

Paul Kagame anarudi Madarakani mwaka 2017? Hii hapa kutoka Mahakamani Rwanda..


Mahakama Kuu Rwanda imepokea Shauri kutoka Vyama vya Upinzani Rwanda ambavyo vinahitaji Rais Paul Kagame asigombee Urais kwa awamu nyingine tena baada ya kumaliza awamu mbili za kuiongoza Nchi hiyo.
Jopo la Majaji nane litajadili ishu hiyo, japo Serikali iliweka pingamizi Mahakamani kwamba kisijadiliwe chochote lakini jopo hilo linaloongozwa na Jaji Immaculee Nyirinkwaya lilitupilia mbali pingamizi hilo na Shauri litaendelea kusikilizwa Mahakamani September 23 2015.
Rwanda's President Paul Kagame attends the opening ceremony of the 24th Ordinary session of the Assembly of Heads of State and Government of the African Union (AU) at the African Union headquarters in Ethiopia's capital Addis Ababa, January 30, 2015. REUTERS/Tiksa Negeri
Rais wa Rwanda, Paul Kagame
Rais Kagame hakuwahi kutamka kama atagombea awamu ya tatu ya Urais au hapana, lakini kila alipoulizwa amekuwa akijibu kwamba hayo ni maamuzi ya Watu wa Rwanda wenyewe kumruhusu aendelee au hapana.
Kumekuwa na mvutano wa muda mrefu kuhusu ishu ya Katiba ya Rwanda kufanyiwa mabadiliko ili kumruhusu Kagame agombee tena Urais kwenye Uchaguzi Mkuu 2017 lakini upande wa Upinzani wameonekana kutokubaliana kabisa na mapendekezo hayo.
gty_obama_ethiopia_presser_02_mm_150727_4x3_992
Rais Barack Obama alipokuwa Ethiopia July 2015.
Rais wa Marekani Barack Obama ni mmoja ya Viongozi ambao hawakubaliani na kitendo cha  Kiongozi yoyote kubadili Katiba ili aendelee kubaki Madarakani >>> ‘Nadhani mimi ni Rais bora kabisa, hata nikisema nigombee Urais wa Marekani kwa mara nyingine ninashinda… Hakuna mtu anatakiwa kuwa Rais milele, ni vizuri mkapeana nafasi na mwingine aje aongoze akiwa na mawazo mapya‘- Hii ni nukuu ya alichokisema Rais Obama akiwa kwenye ziara Ethiopia July 2015.
Ni watu 10 pekee wanaopinga muhula wa 3 wa Kagame

Ni watu 10 pekee wanaopinga muhula wa 3 wa Kagame


Kagame
Maafisa nchini Rwanda wanasema kwamba baada ya mashauriano ya kitaifa ni watu kumi tu wanaompinga rais Kagame kuwania muhula wa tatu.
Gazeti la New Times lililo karibu na serikali linasema kati ya watu milioni mbili walioshauriwa kuhusu kufanyia katiba mageuzi ni watu kumi tu waliopinga fikra hiyo.
Katiba inasema rais anapaswa kuhudumu kwa mihula miwili pekee.
Wachambuzi wanasema raia wengi wa Rwanda huenda wameogopa kupinga pendekezo hilo.
Rais Kagame amehudumu madarakani tangu 1994.
(Taifa jirani la Burundi lilikumbwa na mgogoro mnamo mwezi Aprili baada ya rais Pierre Nkurunziza kuwania uhula wa tatu).
Tume ya Rwanda kuchunguza makala ya BBC

Tume ya Rwanda kuchunguza makala ya BBC

Rais wa Rwanda Paul Kagame
Serikali ya Rwanda imetangaza tume itakayotoa tathimini kuhusu shutuma na madai dhidi ya makala ya BBC iliyorushwa kwa njia ya Televisheni mwezi Oktoba, kuhusu mauaji ya Kimbari ya mwaka 1994.
Tume ya Watu watano akiwemo mwendesha mashtaka wa zamani wa Rwanda Martin Ngoga, pia wahadhiri wawili wa masomo ya uandishi wa habari .Serikali ya nchi hiyo imewapa kazi ya kuchunguza na kutathimini Makala ya BBC iliyoitwa 'untold Story'.
Katika Makala hayo, aliyekua mkuu wa majeshi alimshutumu Rais wa Rwanda Paul Kagame kutoa amri ya kuidungua ndege iliyokua imembeba Raisi wa nchi hiyo wakati huo Juvenal Habyarimana na mwenzake wa Burundi wakati huo,Cyprian Ntaryamira. Baadhi ya wadadisi wa mambo wanaona kuwa tukio hilo lilikua chanzo cha mauaji ya kimbari mwaka 1994.
Mamlaka nchini Rwanda iliamua kufungia matangazo ya BBC ya ukanda wa maziwa makuu kusikika nchini humo.
Tume hiyo imetoa kipindi cha miezi mitatu kutathimini makala hayo hata hivyo muda zaidi unaweza kuongezwa kabla ya Ripoti ya tume kufikia uma.
Halikadhalika vipindi vya BBC vimepigwa marufuku kurushwa kwenye Redio ya Rwanda FM na mtandao wa BBC pia umezuiliwa na Serikali.
BBC imekanusha vikali ikisema kuwa hakuna sehemu yoyote katika makala hayo inayoelezea kukataa mauaji ya kimbari dhidi ya watutsi.
Katika taarifa ya hivi karibuni BBC imesema inawajibu wa kuchunguza maswala magumu na yenye changamoto pia imesema inaamini makala hayo yametoa mchango mkubwa katika kuleta uelewa kuhusu historia ya Rwanda na ukanda mzima.pia shirika hilo limesema limekua likifanya jitihada mara kadhaa kuipata Serikali ya Rwanda lakini halikufanyikiwa.

Kategori

Kategori