Kupitia akauntI yake ya Twitter, amesema shirika hilo linamsikitisha kwa madai kwamba badala ya kuwa shirika lenye hadhi kuu zaidi, limekuwa kama baraza la watu kukusanyika na kupiga gumzo.
Hii ni baada ya jaribio lake la kutaka kupinga azimio lililokemea mpango wa Israel kuendelea kujenga makaazi yao katika ardhi ya Wapalestina kufeli.
Trump
Baraza la usalama la Umoja wa Matifa limesema kuwa Israel inakiuka sheria za kimataifa kwa kujenga katika ardhi ya Wapelestina.
Azimiio hilo lilipitishwa Ijumaa iliyopita huku Trump akitoa onyo kwamba mambo yatakuwa tofauti wakati atakaposhika rasmi hatamu za uongozi wa Marekani.
Wapiga kura watapiga kura Ntarehe 8 Novemba kumchagua rais atakayemrithi Barack Obama wa chama cha Democratic.
Hapa tutakupatia tathmini ya udadisi wa kura za maoni nchini humo, hasa kuhusu ushindani kati ya mgombea wa Democratic Hillary Clinton na mwenzake wa Republican Donald Trump.
Baada ya mdahalo, huchukua siku kadha kabla ya matokeo yake kudhihirika kwenye kura za maoni.
Image captionUtathmini wa kura za maoni kufikia 13 Oktoba
Kura za maoni zina umuhimu?
Ni vigumu kubaini maoni ya watu zaidi ya 300 milioni lakini watafiti wa maoni bado hujaribu. Watu wanaotumiwa huwa ni 1,000 hivi na kwa kuzingatia maadili ya utafiti na sayansi, huwezekana kubashiri matokeo.
Majimbo yanayoshindaniwa sana?
Kuna majimbo 13 ambayo yanatarajiwa kushindaniwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu. Hapa chini ni ramani ya majimbo hayo na uwezekano wa nani atashinda kwa kutumia matokeo ya kura ya maoni ya tovuti ya Real Clear Politics.
Ndipo Donald Trump aweze kupata nafasi nzuri, anahitaji kujishindia Florida na Ohio na majimbo mengine kadha. Kwa sasa hali ilivyo, Clinton yupo mbele kidogo Florida na Ohio.
Matokeo kamili ya kura za maoni za karibu majimbo hayo yanayoshindaniwa ni kama ilivyo hapa chini.
Trump na Clinton ndio wagombea pekee?
La hasha, kuna wagombea wengine wengi. Lakini wale wakuu ni Hillary Clinton na Donald Trump.
Mgombea wa Green Party Jill Stein, 66, ni daktari na mwanaharakati ambaye anatarajia kupata uungwaji mkono kutoka kwa wafuasi wa Democratic waliomuunga mkono Bernie Sanders ambao bado wanampinga Bi Clinton.
Gavana wa zamani wa New Mexico Gary Johnson, 63,anawania kupitia chama cha Libertarian Party na sana anaangazia kuwavutia wafuasi wa Republican wasiopendezwa na Bw Trump.
Kwa mujibu wa Real Clear Politics, Bi Stein ana karibu 2% ya kura naye Bw Johnson ana zaidi ya 7%.
Wawili hawa wanaweza kuchangia sana kuamua mshindi kwani watavutia wapiga kura kutoka kwa wagombea wakuu.
Clinton amefanya vyema?
Image copyrightAP
Bi Hillary Clinton amepigiwa upatu kushinda lakini kuna wakati mwingine ambapo uongozi wake hupunguzwa sana. Majuzi zaidi ilikuwa mapema Septemba. Mwanzo, alionekana kuwakosoa wafuasi wa Donald Trump na kusema ni "kapu la watu wa kusikitisha" na wasioweza kuokolewa.
Baadaye, alionekana kukaribia kuzirai wakati wa sherehe ya ukumbusho wa shambulio la 9/11.
Umaarufu wake ulishuka kidogo lakini baadaye akajikwamua.
Trump aliongoza lini mwisho?
Image copyrightAP
Wakati mmoja Trump aliachwa nyuma sana na Bi Clinton, akiwa nyuma kwa karibu 20% majira ya joto 2015 wagombea walipokuwa wengi. Hata hivyo, amefanikiwa kumpita Bi Clinton mara chache sana.
Mwisho ni alipopokea idhini ya kuwania urais mwisho wa Julai kwenye Kongamano la Taifa la Republican.
Hakuongoza kwa muda mrefu kwani mpinzani wake naye alijikwamua kongamano la Democratic lilipofanyika siku chache baadaye.
Wagombea wenza walisaidia?
Zamani wagombea wenza walisaidia sana, mfano Bill Clinton alipanda 12% baada ya kumteua Al Gore mgombea mwenza 1992.
Lakini karibuni mambo yamekuwa tofauti na mwaka 2016 hakujakuwa na mabadiliko makubwa.
Mgombea mwenza wa Trump, Gavana wa Indiana Mike Pence aliteuliwa Julai 15 naye wa Clinton, gavana wa zamani wa Virginia Tim Kaine akatangazwa Julai 22 July, lakini hakukutokea mabadiliko makubwa kwenye kura za maoni.
Image copyrightGETTY IMAGESImage captionJanet Jackson ana mumewe, Wissam al-Mana wanatarajia kujifungua mtoto wao wa kwanza
Muimbaji Janet Jackson amethibitisha rasmi kwamba anatarajia kujifungua mtoto wake wa kwanza akiwa na umri wa miaka 50.
Ameliambia jarida la People: "Tunashukuru Mungu kwa baraka tuliyonayo", na akapigwa picha na tumbo lake linalozidi kuwa kubwa kudhihirisha uja uzito.
Fununu kuhusu uja uzito wake zilizuka Aprili alipojitokeza kuahirisha shughuli zake na tamasha la kimataifa 'Unbreakable' akisema anataka kupanga uzazi na mumewe Wissam al-Mana.
Ameonekana hivi karibuni London akinunua vitu katika duka la watoto.
Jarida la The People limenukuu duru iliyo karibu na familia ya Jackson aliyesema: "Ana furaha sana kuhusu uja uzito wake na anedelea vizuri sana. Ana raha kuhusu kila kitu."
Katika video iliowekwa kwenye Twitter mwezi April, amewaambia mashabiki wake kuwa ana ahirisha shughuli zake, kwasababu "kumekuwa na mabadiliko ya ghafla".
Image copyrightJANET JACKSON/@TWITTERImage captionJanet Jackson alitangaza Aprili anaahirisha shughuli zake kupanga familia
"Nilidhani ni muhimu mujue kwanza. Mimi na mumewangu tunapanga familia yetu," alisema, na kuongeza: "Tafadhali iwapo munaweza, jaribu muelewa kuwa ni muhimu nifanye hivi kwa sasa."
Aliendelea kusema: "Ni lazima nipumzike, ni agizo la daktari."
Janet Damita Jo Jackson alizaliwa Mei 16 1966 Gary, Indiana Marekani
Ni mdogo katika ndugu tisa na ni dadake muimbaji nyota Michael Jackson
Alitoa albamu yake ya kwanza Janet Jackson mnamo 1982
Ana albamu 11 ya hivi karibuni ikiwa ni Unbreakable, iliotolewa 2015
Ni mshindi mara 7 wa tuzo ya Grammy
Alianza taaluma yake kwa kushiriki katika kipindi cha televisheni The Jacksons mnamo 1976 na ameshiriki katika filamu kadhaa ikiwemo ya Tyler Perry 'Why Did I Get Married'
Muimbaji huyu ameolewa na mumewe wa tatu, Bilionea raia wa Qatari Wissam al-Mana, 2012.
Janet Jackson sio mwanamke maarufu wa kipekee kuzaa katika umri mkubwa.
Mshindi wa tuzo ya Oscar Halle Berry amezaa mtoto wake wa pili akiwa na miaka 47, miaka mitatu iliyopita.
Mkewe John Travolta, Kelly Preston amezaa mtoto wake wa tatu akiwa na miaka 48.
Image copyrightAFPImage captionWasichana 250 walitekwa Aprili 2014
Afisa wa cheo cha juu serikalini ameiambia BBC kwamba wasichana 21 waliokuwa miongoni mwa wasichana wa shule waliotekwa na wapiganaji wa Boko Haram eneo la Chibok sasa wako huru.
Taarifa zinasema wasichana hao kwa sasa wamo mikononi mwa maafisa wa usalama katika mji wa Maiduguri, kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.
Msemaji wa Rais Muhammadu Buhari amethibitisha kuachiliwa huru kwa wasichana hao.
Bw Mallam Garba Shehu ameandika kwenye Twitter: "Imethibitishwa kwamba wasichana 21 wa Chibok wameachiliwa na kwa sasa wamo mikononi mwa Idara ya Masuala ya Serikali."
Haijabainika iwapo wasichana hao walikomombolewa na wanajeshi au waliachiliwa huru na wanamgambo hao.
Jeshi la Nigeria kwa muda limekuwa likiendesha operesheni kubwa ya kijeshi katika msitu wa Sambisa, ngome ya Boko Haram.
Tangu wakati huo, ni msichana mmoja pekee aliyekuwa ameokolewa.
Kundi la kujihami la wanakijiji lilimpata Amina Ali Nkeki mwezi Mei akiwa na mumewe, ambaye anatuhumiwa kuwa mwanachama wa Boko Haram, pamoja na mtoto wake.