Showing posts with label June 19. Show all posts
Showing posts with label June 19. Show all posts
MEYA WA UBUNGO AKAMATWA NA POLISI

MEYA WA UBUNGO AKAMATWA NA POLISI

Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob amekamatwa na polisi kwa ajili ya mahojiano hata hivyo sababu za kuchukuliwa kwake bado hazijawekwa wazi.
Tukio limetokea leo Jumatatu saa sita mchana katika makao makuu ya wilaya hiyo yaliyopo Kibamba.
Askari wapatao wanne wakiwa katika gari aina ya Land Cruise walifika katika eneo hilo kisha kuzuia msafara wa viongozi wa Chadema waliokuwa tayari kuanza ziara ya kutembelea manispaa hiyo.
Miongoni mwa viongozi hao wa Chadema ni waziri mkuu mstaafu, Frederick Sumaye na viongozi wengie wa Ubungo na Kanda ya Pwani.
Baada ya kuzuia msafara huo, mmoja wa askari alishuka na kumfuata Jacob na kumweleza anamuhitaji kuambatana naye hadi Kituo cha Polisi cha Mbezi.
“Tunakuomba uongozane na sisi hadi kituoni tuna maongezi na wewe yasiyozidi dakika 10 tukiridhika tunakuachia uendelee na shughuli zako,”
Baada ya kumweleza hayo, ofisa huyo alikwenda moja kwa moja katika gari la Sumaye na kumweleza kuwa wanamuhitaji meya kwa dakika 10 kisha watamuachia.

from Blogger http://ift.tt/2srrQsK
via IFTTT

from Blogger http://ift.tt/2tEIsg1
via IFTTT

FAHAMU : MADHARA YA KUNYWA VINYWAJI VYA KUONGEZA NGUVU

FAHAMU : MADHARA YA KUNYWA VINYWAJI VYA KUONGEZA NGUVU

April mwaka jana, Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TDFA) ilikamata makopo 1,526 ya vinywaji vya kuongeza nguvu katika soko la Tanzania ambavyo vilikuwa havikidhi viwango vya ubora na usalama kwa matumizi ya binadamu.
Vinywaji vya kuongeza nguvu, visivyo na kilevi, kisayansi vinaelezwa vina kiasi kikubwa cha kafeini, vitamini pamoja na kemikali za taurine, glucuronolactone.Wakati mwingine pia huongezewa dawa aina ya guarana pamoja na mitishamba aina ya ginseng kwa lengo la kusisimua akili na kuongeza nguvu za mwili.
Mtafiti wa madhara ya dawa za kulevya wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Dk Stephen Nsimba anasema kwamba vinywaji hivi vina kiasi kikubwa cha kafeini ambayo ni dawa inayosisimua ubongo na kwa kuvichanganya na pombe athari zake kwenye mfumo wa fahamu za mwili huongezeka.
“Baada ya kuchanganya vinywaji hivi, kafeini katika vinywaji vya kuongeza nguvu, hupunguza athari za kilevi na kumfanya mtumiaji asibaini haraka kuwa amekunywa kiasi kikubwa cha kilevi. Hili ni jambo la hatari” ameonya Dk Nsimba.
Matokeo ya utafiti mmoja yaliyowasilishwa katika mkutano wa mwaka 2013 wa Chama cha Afya ya Moyo cha Marekani (American Heart Association) uliofanyika katika mji wa New Orleans, ilibainika kuwa kunywa kopo moja hadi matatu ya vinywaji vya kuongeza nguvu, kunaweza kusababisha maoigo ya moyo kudunde bila mpangilio na kuongeza shinikizo la damu, na kusababisha kifo cha ghafla.
Hii ni kwa mujibu wa utafiti wa T. Van Batenburg-Eddes na wenzake uliochapishwa katika jarida la Front Psychology toleo la 5, mwaka 2014.

from Blogger http://ift.tt/2sOhlT2
via IFTTT

BREAKING: VIGOGO WA ESCROW WAFIKISHWA MAHAKAMANI LEO

BREAKING: VIGOGO WA ESCROW WAFIKISHWA MAHAKAMANI LEO

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) aimewafikisha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wafanyabiashara James Rugemarila na Harbinder Sethi kwa tuhuma za uhujumu uchumi na makosa mengine yanayofanana na hao.
Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Valentino Mlowola alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo alisema kuwa muda mrefu wamekuwa wakiulizwa kuhusu kesi ya Escrow hivyo sasa anaamini ni wakati muafaka wa kuwafikisha watuhumiwa hao wawili mahakamani.
Mlowola alisema kuwa taasisi hiyo imefanya uchunguzi wa kutosha kwa muda wote ambao ilikuwa kimya, na hivyo wamefikishwa mahakamani kisutu na baada ya hapo mahakama itafanya taratibu za kuhamishia kesi hiyo katika Mahakama ya Rushwa na Uhujumu Uchumi.
Kabla ya vigogo hawa wawili kufikishwa mahakamani leo, baadhi ya watumishi wa TANESCO tayari walishtakiwa kufuatia tuhuma za kupokea fedha kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya VIP Engeneering & Marketing ambaye pia alikuwa Mkurugenzi wa kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Ltd (IPTL), James Rugemalira.
 ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2rMX1gk
via IFTTT

KIJANA Ajinyonga Kwa Kamba Juu ya Mti Kisa Ugumu wa Maishaโ€ฆ.

KIJANA Ajinyonga Kwa Kamba Juu ya Mti Kisa Ugumu wa Maisha….

Kijana Paulo Ezekiel, amejinyonga kutokana na kile kinachodaiwa ugumu wa maisha.
Paulo (17) alikuwa anaishi na wazazi wake Mtaa wa Mazinge Kata ya Ndembezi mjini Shinyanga, alifariki dunia juzi usiku kutokana na kudaiwa kujinyonga kwa kamba juu ya mti jirani na nyumbani kwao.
Picha ya Tukio jingine
Tukio hilo lilitokea majira ya saa kumi alfajiri baada ya marehemu kutoka nje ya geti la nyumba yao na kuelekea kwenye mti huo kisha kijipiga kitanzi kunakodaiwa kusababisha kifo chake.
Akizungumza tukio hilo jana, baba mzazi wa marehemu, Ezekiel alisema awali kijana wake alikuwa na ugomvi na marafiki zake ambao ni madereva bodaboda, lakini huo ulisuluhishwa na akaendelea na majukumu yake.
Alisema chanzo cha kifo chake hakijafahamika vizuri, lakini mara kwa mara alikuwa akilalamika kuwa maisha ni magumu.

“Ilipofika majira ya saa 10 usiku nilisikia mlango wa chumba cha kijana wangu ukifunguliwa, nikajua ametoka kwenda kujisaidia lakini muda mrefu ulipopita bila kusikia amerudi, ndipo nikatoka nje na kukuta geti la uani likiwa wazi, nikaanza kumtafuta bila mafanikio”, alisema. 

Aliongeza:

“Niliporudi ndani nikamwamsha mama yake mzazi na wadogo zake wa kike, tukaanza kumsaka ndipo tukamuona akiwa juu ya mti jirani na nyumba yetu, akiwa ameshafariki kwa kujinyonga na kamba”. 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Jumanne Murilo, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa hakuna mtu yeyote anayeshikiliwa na jeshi la hilo kuhusiana na tukio hilo.
Alisema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha maiti katika Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga na unatarajiwa kuzikwa leo kwenye Makaburi ya Mtaa wa Dodoma mjini hapa.
Chanzo: Nipashe
 ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2srAbg5
via IFTTT

Wananchi Wavamia Tena leo Mgodi wa Acacia

Wananchi Wavamia Tena leo Mgodi wa Acacia

Kundi kubwa la wananchi kutoka vijiji vitano vinavyozunguka mgodi wa Acacia North Mara wamevamia mgodi huo.
Taarifa kutoka eneo la tukio hivi sasa zinaeleza kuwa wananchi hao wanaendelea kukusanyika katika lango kuu la mgodi huo maarufu Boom Gate huku jeshi la polisi likijaribu kuwatawanya.
Hilo ni jaribio la pili kwa wananchi hao kutaka kuingia mgodini humo baada ya lile ya jana ambapo polisi walifanikiwa kulizima.
Taarifa zaidi kukujia
 ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2srEwjp
via IFTTT

Kategori

Kategori