Showing posts with label June 15. Show all posts
Showing posts with label June 15. Show all posts
Picha hizi,Manchester United imekamilisha usajili wa beki Victor Lindelof kutoka Benfica…

Picha hizi,Manchester United imekamilisha usajili wa beki Victor Lindelof kutoka Benfica…

Klabu ya Manchester United imekamilisha usajili wa beki Victor Lindelof ,22 kutoka klabu ya Benfica kwa ada ya Pauni milioni 30.7.
Victor Lindelof ameshawasili Carrington leo kwa ajili ya vipimo vya afya na kukamilisha usajili wa kujiunga na Man United.
Victor amekuwa target ya meneja Jose Mourinho toka January mwaka huu.
 ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2s4WVUv
via IFTTT


Exclusivee…Alichokisema Irine Uwoya Baada ya Dogo Janja Kumtaka Awe Mpenzi Wake..!!!

Exclusivee…Alichokisema Irine Uwoya Baada ya Dogo Janja Kumtaka Awe Mpenzi Wake..!!!

Wiki kadhaa baada ya Dogo Janja aka Janjaro kuweka wazi kwenye vyombo vya habari kuwa muigizaji Irine Uwoya ndiye anayemkosesha usingizi na angependa siku moja awe barafu wa moyo wake, Uwoya amemfungukia.
Janjaro aliwahi kusema kuwa, “Irene Uwoya nampenda tangu nikiwa mtoto, nimeshabandika sana picha yake maghetoni. Nampendaga sana na ni mtu ambaye nammezeaga mate.”
Muigizaji huyo ambaye amekuwa akitajwa mara kwa mara kwenye nyimbo za wasanii wa Bongo Flava akihusishwa na mfano wa uzuri na mvuto, amekejeli ombi la Janjaro ambaye amedai ni mdogo wake mwenye matatizo yake binafsi.
“Yaani kale jamani… ni mdogo wangu, naongeaga naye tunapiga story. Kananifurahisha lakini, hivyo tu,” Uwoya alisema
Hata hivyo, Uwoya aliweka wazi kuwa katika kumchagua mwandani yake, umri sio kigezo cha kumpima mwanaume anayetaka kuwa naye.
 ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2seN5hh
via IFTTT


HII NDIYO SHULE YA MSINGI ANAYOFUNDISHA MSANII ROMA MKATOLIKI

HII NDIYO SHULE YA MSINGI ANAYOFUNDISHA MSANII ROMA MKATOLIKI

Msanii wa muziki wa Hip Hop nchini Tanzania, Ibrahim Mussa (Roma Mkatoliki) amegeukiwa kufundisha ambapo jana aliibukia katika Shule ya Msingi Mchikichini iliyopo Mbagala Rangi Tatu jijini Dar es Salaam na kufundisha wanafunzi wa darasa la saba somo la hisabati.
Msanii huyo akiongea na gazeti la MTANZANIA alisema kuwa anafundisha somo hilo kwa wanafunzi wa darasa la saba kwani wengi hufeli kutokana na kuwa na walimu.
  • “Mimi kitaaluma ni mwalimu wa hisabati, kutokana na kufeli mno somo hilo nimeanza kampeni ya kufundisha na kugawa vitabu kwa kuanza na shule hii kwa sababu pia nitakuja kufanya onyesho la muziki kwenye sikukuu ya Eid kwa mara ya kwanza,” alisema Roma.
Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Ramadhan Mashaka alisema kuwa msanii huyo amepata kibali cha kufundisha shuleni hapo.


“Nimekagua na kugundua kuwa Roma ni mwalimu mzuri wa hisabati hivyo tumemkaribisha afundishe wanafunzi bila hofu, tukiwa na imani kubwa kuwa wataelewa kwa sababu wanafundishwa na mtu wanayempenda na hii itaongeza morali ya wanafunzi shuleni hapa,” alisema Mwalimu Juma.

Licha ya kufundisha, atafuturisha watoto yatima wa Kituo cha Nira kilichopo Mbagala Chamazi na atatoa zawadi za sikukuu ya Eid.

from Blogger http://ift.tt/2t62JvI
via IFTTT


RASMI IBRAHIM AJIBU NI MALI YA YANGA

RASMI IBRAHIM AJIBU NI MALI YA YANGA

Mshambuliaji wa Simba, Ibrahim Ajibu imefahamika kuwa sasa ni rasmi anajiunga na Yanga baada ya klabu yake ya sasa kushindwa kufikia nae makubaliano ya kumbakiza kwenye kikosi.
Mabosi wa Simba na mchezaji huyo wameshindwa kuafikiana juu ya makubaliano ya mkataba wake mpya na hiyo imewapa nafasi Yanga waweze kumchukua.
Taarifa kutoka ndani ya Simba imeeleza kuwa wameamua kumruhusu aondoke baada ya mchezaji huyo kuonyesha kutokuwa na nia ya kuendelea kubaki klabuni hapo.
“Tumemwacha aende anakotaka kwenda kwa sababu hana ‘spirit’ tunayoihitaji sisi, acha aende tu sisi mbele kwa mbele,” amesema mtoa taarifa.
Ajib ambaye alianza kutamba Simba akitokea kikosi cha vijana, atatua Yanga aliwa mchezaji huyu kutokana na mkataba wake kuelekea mwishoni.
 ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2t5PLOp
via IFTTT


Kategori

Kategori