Showing posts with label JK NA GEITA. Show all posts
Showing posts with label JK NA GEITA. Show all posts

JK AMTAMBULISHA MAKAMU WA RAIS MHE. SULUHU KWA RAIS WA CHINA MHE. XI JINPING, JOHANNESBURG

RAIS MSTAAFU 

Rais Mstaafu wa awamu Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, kwa Mhe. Rais wa China Xi Jinping, wakati walipokutana kwenye Mkutano wa Tano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na China uliofanyika leo Jijini Johannesburg. Mhe Rais Mstaafu amehudhuria Mkutano huo kama Rais Mstaafu. Picha na OMR

Rais mstaafu Jk anedelea na shughuli zake Ofisi za CCM



Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Katibu wa Itikadi na Uenezi  Nape Nnauye mara baada ya kuwasili kwenye Makao Makuu ya Chama Ofisi Ndogo Lumumba.
 


Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa ofisini kwake Makao Makuu ya  CCM Ofisi Ndogo Lumumba .
Mpekuzi blog

CCM kujadili majina ya walioomba kugombea Uspika



 Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wana CCM alipowasili mjini Dodoma kwa ajili ya kikao cha siku moja cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu itakayojadili majina ya wana-CCM walioomba ridhaa ya kuteuliwa kugombea Uspika na Unaibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na makada wa CCM alipowasili mjini Dodoma kwa ajili ya kikao cha siku moja cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu itakayojadili majina ya wana-CCM walioomba ridhaa ya kuteuliwa kugombea Uspika na Unaibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

JK ATINGA OFISINI KWAKE LUMUMBA AANZA KUPIGA MZIGO FASTA


 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dk. Jakaya r Kikwete akisalimiana na Katibu wa NEC Oganaizesheni Ndugu Mohamed Seif Khatib mara baada ya kuwasili kwenye Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi,Ofisi Ndogo Lumumba.
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Katibu wa Sekretarieti Ndugu Anamringi Macha mara baada ya kuwasili kwenye ofisi za CCM Lumumba.
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wapenzi na wanachama wa CCM waliojitokeza kumpokea kwenye Makao Makuu ya Chama Ofisi Ndogo Lumumba.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akisani kitabu cha wageni mara baada ya kuingia kwenye ofisi yake,waliosimama ni Katibu wa NEC Oganaizesheni Ndugu Mohamed Seif Khatib (kulia) na Naibu Katibu Mkuu CCM (Bara) Ndugu Rajab Luhwavi.

JK AONDOKA RASMI IKULU LEO


 Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiagana na watumishi wa Ofisi ya Rais Ikulu wakati wakiondoka rasmi katika jumba hilo waliloishi akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miaka 10 iliyopita na kurudi kijijini Msoga. kushoto kwake ni Rais wa awamu ya tano Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
  Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete  akiagana na watumishi wa Ofisi ya Rais Ikulu wakati akiondoka rasmi katika jumba hilo waliloishi kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miaka 10 iliyopita. kushoto kwake ni Rais wa awamu ya tano Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
  Rais wa awamu ya tano Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimsindikiza Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete   wakati akiondoka rasmi Ikulu alimoishi kama Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miaka 10 iliyopita. 
  Rais wa awamu ya tano Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimsindikiza Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete   na mkewe mama Salma Kikwete wakati wakiondoka rasmi Ikulu alimoishi kama Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miaka 10 iliyopita. 
 Wakielekea kwenye helikopta itayowachukua hadi kijijini Msoga
 Picha ya pamoja kabla safari ya Msoga kuanza
  Rais wa awamu ya tano Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiagana na  Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete   na mkewe mama Salma Kikwete wakati wakiondoka rasmi Ikulu walimoishi kama Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miaka 10 iliyopita. 
 Rais wa awamu ya tano Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue na Katibu Mkuu Ikulu Mhe Peter Ilomo na watumishi wa Ofisi ya Rais wakiagana na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt Jakaya Mrisho kikwete

Kategori

Kategori