Showing posts with label China. Show all posts
Showing posts with label China. Show all posts

KATIBU MKUU WA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA AFUNGUA MAONYESHO YA BIASHARA YA BIDHAA ZA CHINA 2015, DAR ES SALAAM LEO


 Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Uledi Mussa (wa tano kulia), akifurahi baada ya kukata utepe kuashiria ufunguzi wa Maonyesho ya Biashara ya Bidhaa za China 2015, uliofanyika Ukumbi wa Karimjee Dar es Salaam leo asubuhi. Wengine na maofisa biashara wa China na wadau wa masuala ya biashara.
 Hapa Katibu Uledi Mussa akitia saini wakati wa ufunguzi wa maonyesha hayo.
 Hapa akioneshwa bidhaa mbalimbali.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Uledi Mussa, akizungumza na wanahabari.


Na Dotto Mwaibale


SHIRIKA la Viwango Tanzania(TBS) limesema  bidhaa zinazotoka china zina ubora huku likitoa mwito kwa wafanyabishara kutumia fursa ya kujifunza kupitia maonesho ya bidhaa za china.

Akizungumza Dar es Salaam leo asubuhi kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, Joseph Masikitiko,Mkurugenzi wa biashara Agnes Mneney alisema haiwekani kujua kma bidhaa zina ubora au la kwa kuangalia kwa macho.

Alisema TBS ndio waliopewa dhamana na Serikali ya kukangua ubora wa bidhaa zote za ndani na za nje kisha kubainisha kwa wananchi kama bidhaa zina ubora au ni hafifu kwa maslahi ya taifa.

''TBS ndio imepewa dhamana ya kudhibiti bidhaa zenye ubora kwa maslahi ya taifa kwahiyo watanzania wasipende kutoa hukumu kwa njia ya kukaangali kwa macho,''alisema.

Agnes alisema mtanzania anachotakiwa kufanya ni kuhahakikisha ananunua bidhaa ambazo zina nembo ya TBS kwasababu bidhaa zote sokoni zinatakiwa kuwa na viwango vya shirika hilo.

''Bidhaa za nchini China lazima ziwe na vuwango vya ubora vinavyotolewa TBS ili kuzingatia kiwango cha ubora katika soko la Tanzania,''alisema.

Kwa upande wake Mwakilishi wa masuala ya biashara na uchuminchini China,Lin Zhiyong alisema maoyesho ni ya siku tatu ambapo zaidi ya wafanyabishara kutoka nchina 230 wameshawasili nchini.     

Akizungumzia ubora wa bidha zao,Zhiyong alisema kupitia udhibiti waTBS wafanyabishara wa china wameanza kuondoa bidhaa ambazo ni hafifu sokoni.

''Bidhaa hafifu zimeanza kuondolewa sokoni kwa takribani miezi mitatu iliyopita ili kuimarisha ushirikiano wetu na TBS  na mkakati wa wafanyabishara wa China ni kuhakikisha tunaondoa bidhaa zote hahifu ili kulinda bora,''alisema.

Kwa upende wake Katibu Mkuu wa viwanda na bishara,Uledi Mussa alisema Tanzania imekuwa na urafiki mkubwa wa masuala ya kiuchumi na China.

Alisema kupitia urafiki huo ni imani yake China itaisaidia Tanzania kujenga viwanda na kuisaidia Tanzania kuzalisha vitu vyenye ubora na kuviuza.

Mussa alisema Tanzania inaanda mpango wa kuanzisha viwandana kwamba dhamira ya wizara husika ni kuwawesha wafanyabishara wazawa kumiliki viwanda kwa maaendeleo ya nchi.

''Tumekuwa na mambo mengi lakini dhamira ya Serikali kwa miaka mitano inayokuja ni kujenga viwanda na kuwezesha wafanyabishara wazawa kuvimiliki,''alisema. 


Maonesho hayo ni ya nne tangu kuanza kuonyeshwa nchini ambayo yanaendelea kwa siku tatu katika viwanja vya Daimond Jubilee jijini Dar es Salaam.
China yatakiwa kusitisha ujenzi baharini

China yatakiwa kusitisha ujenzi baharini

Uwanja wa ndege unaojengwa na China katika visiwa vya Spatry
Marekani imetaka kuwepo usitishwaji wa ujenzi wa miradi kwenye maeneo yanayozozaniwa katika bahari ya kusini mwa China.
Waziri wa ulinzi wa Marekani Ash Carter aliuambia mkutano mkuu wa ulinzi nchini Singapore kuwa tabia ya China eneo hilio imekiuka sheria za kimataifa
Carter amesema kuwa kuvihami kijeshi visiwa bandia ambavyo vinajengwa na China ni hatua inayoweza kusababisha mizozo ya kijeshi.
China yatakiwa kusitisha ujenzi baharini
Matamshi yake yanakuja siku moja baada ya makao makuu ya jeshi la marekani kusema kuwa china imeweka silaha katika moja ya visiwa hivyo.
Bwana Carter anasema kuwa hakutakuwa na suluhu la kijeshi . Hata hivyo amesema kuwa Marekani itaendelea kuwa na jeshi lake katika eneo hilo.

BALOZI WA CHINA NCHINI TANZANIA, LIU DONG AZINDUA TAMTHILIA YA TUOANE 'LETS GET MARRIED'


 Balozi wa China nchini Tanzania, Liu Dong akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa Tamthilia mpya ya Tuonae ,Lets Get Married iliyichezwa na wachina na kutafsiriwa kwa kiswahili. Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar e Salaam jana. Kulia ni Ofisa kutoka ubalozi wa China, ambaye alikuwa ni mkalimani wa balozi huyo, Yetianfa Attache.
  Balozi wa China nchini Tanzania, Liu Dong (kulia), akipeana mkono na Balozi wa StarTimes nchini, Msanii Nurdin Bilal 'Shetta' wakati wa uzinduzi wa Tamthilia hiyo.

Balozi wa China nchini Tanzania, Liu Dong (kulia), akipeana mkono na Balozi wa StarTimes nchini, Msanii Nurdin Bilal 'Shetta' wakati wa uzinduzi wa Tamthilia hiyo.

 Maofisa wa Kampuni ya StarTimes wakifurahia jambo kwenye uzinduzi huo.
 Wanahabari wakichukua tukio hilo.
 Warembo wa StarTimes wakiwa tayari kwa zoezi la kuzindua Tamthilia hiyo. Kutoka kulia ni Hadija Saidi, Nyachilo Bunini na Fausta Mushi.
 Balozi wa StarTimes nchini, Msanii Nurdin Bilal 'Shetta'  (katikati), akiwa na wadau wengine kwenye uzinduzi huo.
Wadau wakiwa kwenye uzinduzi huo.

Na Dotto Mwaibale


BALOZI wa China nchini Tanzania, Liu Dang amesema ushiriano wa kirafiki baina ya Tanzania na China ni muhimu sana katika ukuzaji wa sekta ya utamaduni.


Kauli hiyo aliitoa wakati akihutubia katika uzinduzi wa Tamthilia ya Tuonane 'Lets Get Married iliyochezwa na wachina baada ya kutafsiriwa kwa lugha ya kiswahili.


"China na Tanzania ndugu na ushirikiano na ubadishilianaji katika sekta mbalimbali hasa sekta  ya kiutamaduni zinahistoria ndefu hivyo zinapaswa kudumishwa" alisema Balozi Dong.


Alisema Rais wa China Xi Jingping alipotembelea Tanzania mwaka jana serikali za hizi nchi mbili zilipeana vizuri mawazo na kusaini mikataba mingi mbalimbali ya ushirikiano ambapo ziara hiyo iliziletea nchi hizi mbili mafanikio makubwa na kufungua ukurasa mpya wa maendeleo ya historia ya uhusiano baina yao.


Akizungumza katika uzinduzi huo Mchambuzi wa Vipindi wa Kampuni ya StarTimes Tanzania, Rehema Kisyombe alisema kutokana na ushiriano mzuri wa nchi hizo kwa upande wao StarTimes wameadhimia kuudumisha kwa njia ya burudani kwa kuleta vipindi mbalimbali kutoka china.


Alisema kwa kutambua hilo StarTimes imekuwa ikileta tamthilia mbalimbali za kichina zilizotafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili ambapo mpaka hizi sasa wamekwisha onesha nne kupitia chaneli ya Kiswahili ijulikanayo kwa jina la Star Swahili.


Kisyombe alizitaja tamthilia hizo kuwa ni Mapambano, Ujana wangu, Matumaini ya Baba na Hot Mom ambazo zilipokelewa vizuri na watamazaji wa chaneli hiyo na sasa wanawaletea tamthilia hiyo ya Tuoane. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)
Programu ya mashoga yafadhiliwa Uchina

Programu ya mashoga yafadhiliwa Uchina

Programy ya kuwaunganisha mashoga nchini Uchina yapata ufadhili.
Programu ya kuwaunganisha mashoga nchini Uchina imejipatia ufadhili wa dola millioni 30 kutoka kwa wawekezaji wa kampuni ya DCM.
Blued, iliobuniwa na mtandao wa jamii wa Danlan mwaka 2012 hutumiwa na takriban watu millioni 15.
Kulingana na mtandao wa habari wa Tech barani Asia,watumiaji hao wanaonekana kutoka katika miji mikuu mikubwa kama vile,Beijing,Shangai na Guangzou.
Ushoga nchini Uchina ulikuwa haramu hadi mwaka 1997 na ulionekana kama ugonjwa wa akili hadi mwaka 2001.
Mashoga
Xiaofeng Wang ,ambaye ni mchambuzi katika kampuni ya utafiti ya Forrester ,amesema katika ripoti ya kampuni hiyo ya huduma za data kwamba programu za mesenja zina umaarufu mkubwa nchini Uchina kwa kuwa kasi ya mtandao wa simu iko chini.
Lakini katika kuchumbiana, programu hiyo hutumika wazi na wapenzi wa jinsia tofauti,programu moja ya kuchumbiana kwa jina Momo ina takriban watumiaji millioni 52.
Lakini upande wa mashoga swala hilo hufanywa kwa siri kubwa sana.''Huwezi kuwaona mashoga walio na ari ya kutangaza jinsia zao''.alisema Forrester.
Nchini Uchina takwimu rasmi zinaripoti kwamba kuna wavulana 118 kwa kila wasichana 100 wanaozaliwa katika famila za wachina.
Tangazo la biashara lazua zogo China

Tangazo la biashara lazua zogo China

Polisi wanachunguza ikiwa kampuni hiyo ilivunja sheria ya matangazo ya biashara
Kampuni moja nchini China inakabiliwa na tisho la kutozwa kiwango kikubwa cha faini kwa kuwakodi wanawake kuvua nguo zao kwenye treni mjini Shanghai kwa lengo la kutangaza biashara ya kampuni hiyo kwa abiria.
Katika moja ya video iliyowekwa kwenye mtandao wiki jana, wasichana wawili ghafla walianza kuvua nguo zao na kusalia na nguo za ndani pekee katika treni hiyo iliyokuwa imejaa watu.
Abiria walionekana wakirekodi wasichana hao kwa simu zao za viganjani lakini mwanamke mmoja wa makamo aliwakaripia sana.
Mwanamume mmoja kutoka katika kampuni ya huduma za dobi ambayo wasiahana hao walikuwa wakiitangaza, naye alionekana akiokota nguo za wasichana hao walizokua wanavua.
Baada ya filamu ya wasichana hao wakivua nguo kuenea mitandaoni, polisi waliwasiliana na kampuni hiyo kujibu walichokuwa wanakifanya.
Kampuni hiyo inayotoa huduma za dobi ,kwa jina 'Tidy Laundry', ilipoona ikipata sifa mbaya, iliamua kuomba radhi kwa kosa hilo ikisema kuwa ilinuia tu kutangaza huduma zake kwa wabiria waliokuwa ndani ya treni hiyo.
Taarifa hii ni kwa mujibu wa jarida la Shanghai Daily.
Wamiliki wa kampuni hiyo, wanasema kila aliyehusika kwenye tukio hilo alikuwa muigizaji aliyekuwa amekodiwa.
Hata hivyo huu bila shaka sio mwisho wa masaibu ya kampuni hiyo-polisi wanasema wanachunguza ikiwa ilivunja sheria zinazopiga marufuku matangazo ya kibiasga ambayo yanakera jamii.

YAFUATAYO NI MASHARTI YA KUONA NCHINI CHINA ENDELEA HAPA

 
Ajali za barabarani duniani hutokea kila uchao, na wahitaji wa damu wanazidi kuongezeka huku idadi ya wachangia damu nayo ikizidi kushuka siku hadi siku na kuleta hatari kwa maisha ya wahitaji.Kutokana na hali hiyo mji wa Baoji nchini China uko kwenye harakati za uhamasishaji uchangiaji wa damu kwa mtindo wa kipekee , kampeni ambayo imewekwa ni kwamba kama unahitaji kujiunga na chuo,ukitaka kujifunza udereva na hata ukitaka kuoa ama kuolewa sharti uchangie damu, kampeni ambayo imezua mjadala mkubwa kwenye mitandao ya kijamii.

Sharia hiyo mpya iliyotambulishwa katika jimbo la Shaanxi 


mjini,itaanza kutumika rasmi wiki ijayo inawataka askari na wanachuo wa mwaka wa kwanza kuchangia damu walau mara moja kwa mwaka .Wananchi wa China wanaotaka kuomba leseni za udereva,wanaopokea vyeti vya uhitimu wa mafunzo, wanaoajiriwa kwa mara ya kwanza, na wale wanaofunga ndoa kwa msajili wa ofizi za mji wa Baoji wanapaswa kuchangia damu kwa lazima kama mchango wao kwa jamii.

Taarifa hii ilichapishwa katika mtandao na website ya mji huo wa Baoji, lakini kampeni hii imekumbwa na changamoto ikiwemo wakaazi wa mji huo kuhoji damu hiyo inayotakwa kwa mtindo huo wanahoji uchangiaji ukoje na damu hiyo itatumika wapi, badala ya kuifikiria Zaidi sharia hiyo mpya.

Katika jimbo la Pujiang lililoko Zheijang wao wameichukulia tofauti kampeni hiyo na hivyo wanaongeza alama za ziada kwa wanafunzi wa sekondari ambao wazazi na walezi wenye utamaduni wa kuchangia damu.

Kategori

Kategori