Showing posts with label 2017 at 12:24PM. Show all posts
Showing posts with label 2017 at 12:24PM. Show all posts
Sababu 5 zinazoweza Kuchangia Hedhi yako Kuchelewa Kuiona

Sababu 5 zinazoweza Kuchangia Hedhi yako Kuchelewa Kuiona


Wasichana wengi huanza kutawaliwa na hofu kila wanapoona wakati wa kuonda siku zao (hedhi) umefika halafu hawaoni hali ikijitokeza.

Wengi wanapoona hali hiyo mawazo yao yote hueleka kuwa wameshashika ujauzito, lakini kumbe hali hiyo huweza kutokea kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo hizi hapa 5 chini;-

1. Huweza kuwa ni mabadiliko ya homoni mwilini

2. Mabadiliko ya uzito wa mwili

3. Msongo wa mawazo

4. Mpangilio au mabadiliko ya mlo

5. Maambukizi kwenye via vya uzazi

from Blogger http://ift.tt/2oxU8Sw
via IFTTT


Staa wa SA aliyekuwa na tatizo na kukua haraka Ontlametse Phalatse afariki dunia

Staa wa SA aliyekuwa na tatizo na kukua haraka Ontlametse Phalatse afariki dunia

Staa wa nchini Afrika Kusini aliyekuwa akipendwa kutokana na kuwa mwenye furaha licha ya tatizo la kukua haraka alilokuwa nalo, Ontlametse Phalatse amefariki dunia.
Amefariki jana usiku kwenye hospitali ya Dr George Mukhari Academic huko Ga-Rankuwa, Pretoria. Phalatse aliyekuwa na miaka 18, alikuwa mmoja kati ya wasichana wawili tu nchini humo wenye tatizo hilo nadra liitwalo Progeria.
Awali madaktari wake walitabiri kuwa angekuwa hadi akifikisha miaka 14 tu. Mwezi uliopita Rais Jacob Zuma alitimiza ndoto ya msichana huyo kuonana naye.
Taarifa ya familia yake imesema: It is with great sadness to inform you of the passing of our first lady, Ontlametse Ntlami Phalatse. Our hearts are filled with pain and sadness but Ontlametse — as we know her — would want us to carry on with her courageous spirit.”
Alikuwa maarufu sana Instagram ambako alikuwa na followers 63.6k.

from Blogger http://ift.tt/2pswjJ2
via IFTTT


Kikongwe wa miaka 100 aliwa na fisi.

Kikongwe wa miaka 100 aliwa na fisi.

Kikongwe anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 100, Asyenepe Laia, amefariki dunia baada ya kushambuliwa na fisi.
Miaka 100 auawa na fisi
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, baada ya fisi hao kumuua, katika tukio lililotokea Alhamisi iliyopita, waliondoka na mwili wake kwenda katika msitu ulioko jirani na eneo analoishi na kula nyama yake.
Mashuhuda hao walisema katika tukio hilo, Asyenepe alikamatwa na fisi hao alipokuwa anaokota kuni ajili ya kuchochea katika moto alio kuwa ameuwasha ndani ya nyumba yake.
Walisema tukio hilo lilitokea katika Kijiji cha Kalulu Mashambani kandokando na Hifadhi ya Msitu Hifadhi ya Taifa ya Selous katika Tarafa ya Matemanga, Tunduru mkoani Ruvuma.
Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Tunduru, Dk. Gaufrid Mvile, alisema chanzo cha kifo hicho kilisababishwa na kitendo cha wanyama hao kumshambulia.
Alisema katika tukio hilo walikuta mabaki ya vipande viwili vya mifupa, michirizi ya damu na mabaki ya nguo, mambo yaliyoashiria kuwa kikongwe huyo aliuawa na fisi hao na kumla nyama yake yote.

from Blogger http://ift.tt/2nDkAee
via IFTTT


Fahamu Maajabu ya Nanasi Ambayo Yatakuacha Kinywa Wazi..!!!

BAADHI ya watu wamekuwa wakidai tunda la nanasi kuwa siyo salama kwa akina mama wajawazito, ingawa suala hili bado halijathibitishwa kitaalamu, kwani wapo wanaokula na haijawahi kuripotiwa madhara. Linatumika kama tunda ama juisi na lina faida mbalimbali kwa afya ya mwanadamu.
BAADHI YA FAIDA HIZO NI PAMOJA NA:
Lina vitamini A, B na C, madini ya chuma, calcium, copper na phosphorous ambayo yote ni muhimu sana katika afya ya mwanadamu.Tunda hili husaidia kutengeneza damu, kuimarisha mifupa , meno, neva na misuli (muscles).
Hutibu matatizo ya tumbo, bandama na ini, husaidia kusafisha utumbo mwembamba, hutibu homa, vidonda mdomoni, magonjwa ya koo, hutibu tatizo la kupoteza kumbukumbu, hutibu kikohozi, kutetemeka na uoga (Anxiety). Leo nimeandika tiba ya nanasi kwa sababu ni mjadala mkubwa ulioibuka kuwa tunda hili lina madhara, lakini nikuhakikishie msomaji hakuna madhara ya kukufanya

from Blogger http://ift.tt/2mTwYD7
via IFTTT


Kategori

Kategori