Showing posts with label 2017 at 12:19PM. Show all posts
Showing posts with label 2017 at 12:19PM. Show all posts
Serikali Yatoa Ajira Mpya 3,081 za Walimu

Serikali Yatoa Ajira Mpya 3,081 za Walimu

Serikali imeajiri walimu wapya 3,081 na watatakiwa kuripoti kuanzia Aprili 18, 2017. Bado kuna nafasi za walimu 1,048 zilizotolewa kibali cha ajira.

Waziri wa TAMISEMI, George Simbachawene amesema kuna upungufu wa walimu 26,026 wa masomo ya sayansi na hisabati na kuna ziada ya walimu 7,463 wa masomo ya sanaa.

from Blogger http://ift.tt/2pwuAlV
via IFTTT


Baraka The Prince Awaonya Mashabiki wa Kiba Wasimpangie cha Kufanya

Baraka The Prince Awaonya Mashabiki wa Kiba Wasimpangie cha Kufanya

Mwanamuziki wa RnB anayetamba na ngoma ya ‘Acha Niende’ Baraka The Prince amewaonya mashabiki wasimpangie maisha binafsi na kwamba wao kinachowahusu kutoka kwake ni muziki mzuri, video pamoja na kuwaandalia Show za kuwapa burudani. 
Akizungumza leo kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio Barakah ametoa kauli hiyo baada ya siku kadhaa kushambuliwa na baadhi ya mashabiki ambao walimuita msaliti kwa kuonekana amepiga picha na meneja wa msanii anayetafsiriwa kuwa ni hasimu wa msanii mwenzake kutoka katika lebo yao ya Rock Star 4000. “Wewe kama ni shabiki wangu wa muziki haimaanishi pia ni shabiki wa maisha yangu binafsi, maisha yangu binafsi mniachie. Shabiki wewe ni nani sasa mpaka unipangie maisha? kama mtu niliyepiga naye picha ni binadamu siyo shetani lakini cha ajabu mashabiki ndiyo wanaonitukana na kuongea hivi na vile wakati uongozi wangu haujasema kama nakosea”. Amesema Barakah The Prince. 
Katika hatua nyingine Baraka ameweka wazi kuwa tangu kusajiliwa katika lebo ya Rock Star chini ya Bi. Seven Mosha kumemuongezea nafasi na wigo mpana wa kujulikana ndani na nje ya Afrika Mashariki ikiwa ni pamoja na kuongeza thamani kubwa katika maisha yake. 
Kwa upande mwingine Barakah amekanusha tetesi za yeye kutengwa katika lebo hiyo. “Unajua kwenye kampuni kila mtu ana makubaliano yake na mikataba yake, Lady Jaydee ana mkataba tofauti na mimi na pia kazi zinaenda kwa muda. Huu ulikuwa muda wake wa kuachia albamu lakini mimi nilikuwa na ‘promote kazi yangu mpya hivyo watu wasiseme kama Rock Star inanitenga kwani hawajui mkataba wangu uko vipi. Wao wakae tuu na kusubiri kazi nyingi” Alisema Barakah The Prince.
.
TOA MAONI YAKO HAPA

from Blogger http://ift.tt/2oBYpEw
via IFTTT


Soma kwa Makini Hii Kitu Itakusaidia…!!!

HAKUNA anayebisha kwamba ndoa ni jambo la msingi sana katika maisha ya kila binadamu. Aidha, kuoa ama kuolewa ni heshima katika jamii na ndiyo maana leo hii wapo wanaofanya kadiri wawezavyo kuhakikisha wanapata watu wa kuwa nao kama mwili mmoja pale wanapofikia umri wa kufanya hivyo.
Kufunga ndoa kuna wakati wake, siyo kwamba pale unapojisikia kufanya hivyo basi ufanye hata kama mazingira, umri na hali yako kimaisha havikuruhusu. Lakini sasa, kibaya ambacho nimekuwa nikikishuhudia katika jamii yetu kila siku ni kwamba wapo ambao huchukulia kuoa ama kuolewa kama ‘fasheni’, hali ambayo huwasababishia kuingia katika matatizo ambayo hawakuyatarajia.
Ieleweke kwamba hadi kufikia hatua ya kutamka kwamba unataka kufunga ndoa ni lazima uwe umefanya uchunguzi wa hali ya juu na kuhakikisha kwamba unaingia katika maisha ambayo hutajutia. Suala la kuoana si la kukurupuka, ni lazima kwanza uangalie, je ni kweli unastahili kuoa ama kuolewa kwa wakati huo? Hili ni swali la msingi kujiuliza na kama jibu litakuja akilini mwako kwamba muda bado, basi unatakiwa kusubiri. Suala la kuoa ama kuolewa ni la heri na halitakiwi kuharakishwa eti kwa kufuata mkumbo. Kumbuka waswahili wanasema, mambo mazuri hayataki haraka.
Kwako wewe mwanamke, unapodhani umefikia umri wa kuolewa, kwanza unatakiwa kuangalia mwanaume sahihi, ambaye hata utakapoingia kwenye maisha hayo ya ndoa, utadumu na kufurahia. Epuka sana wanaume walaghai ambao mara nyingi hutumia gia za kuoa ili wakubaliwe kimapenzi.
Anapokutokea mwanaume na kukuambia anakupenda na angependa kuwa wako wa maisha, mchunguze kwa muda mrefu kabla hujafanya maamuzi sahihi. Usimkubalie haraka ili nawe uitwe mke wa mtu kama ilivyo kwa rafiki au ndugu yako aliyeolewa hivi karibuni. Kwa ujumla ni kwamba kabla ya kumtamkia yule ambaye ungependa umuite mke na yeye akuite mume ni lazima kwanza mtaanza kuwa wapenzi wa kawaida kisha baada ya kuona kwamba, mmependezana kitabia ndipo mtafikia hatua moja kati yenu kugusia suala la kuoana.
Kama mtaafikiana katika hilo, mnaweza kuingia katika hatua nyingine ambayo ni kwenda kutambulishana kwa wazazi wenu na baada ya hapo mtakuwa ni wachumba ambao mnatarajia kufunga pingu za maisha.
Jambo la msingi ni kuwa makini sana na nyendo za mpenzi wako katika maisha yenu ya kila siku. Mchunguze kwa undani, je anafaa kuwa mke ama mume wako? Anakufaa au umedondoka katika penzi ambalo siyo sahihi? Isije ikatokea eti kwa sababu mmekuwa wapenzi kwa muda mrefu basi atakapokutamkia kwamba anataka kukuoa, basi ukubali tu hata kama umeona kwamba maisha ya ndoa yenu yanaweza kutokuwa ya amani kutokana na kuwepo kwa migongano ya mara kwa mara pindi mlipokuwa wapenzi wa kawaida.
Wapo wapenzi ambao wanaonekana hata wakija kuoana watakuwa na maisha mazuri. Ni dhahiri kwamba wapenzi ambao wamekaa kwa muda wa zaidi ya mwaka mmoja na haijawahi kutokea wamegombana, kutukanana, kuvunjiana heshima kwa namna moja ama nyingine, hawa wanaweza kuoana na wakaishi maisha ya raha mustarehe.
Nimalizie kwa kusema waswahili wanasema nyota njema huonekana asubuhi na kikubwa zaidi unatakiwa kuwa na imani. Amini kwamba huyo uliyempata ambaye unataka awe mwandani wako ndivyo alivyo na ndivyo atakavyokuwa hata mtakapokuja kuoana. Usiwe na mawazo kwamba anaweza kuja kukugeuka ilimradi tu uwe umempenda na umethibitisha na yeye anakupenda.
Amini ni wako na mnastahili kuwa mke na mume na maisha ya furaha na amani yatakuwa upande wenu.
Tazama video Mtoto amvua kofia 
Papa Francis

from Blogger http://ift.tt/2nCFWFm
via IFTTT


JINSI YA KUJIUNGA NA SEEBAIT NA KUJIPATIA KIPATO KUPITIA BLOG/WEBSITE

Habari ndugu zangu katika tech leo tutazungumzia kuhusu kujiinua kiuchumi sisi kama blogger’s, nalizungumzia hili baada ya kupata maswali na maoni kuhusu seebait kutoka kwa blogger’s wenzangu hivyo tunatimiza Ahadi kama kawaida yetu, naam nisikupotezee wakati twende kwenye mada moja kwa moja.
Jinsi ya kujiunga na seebait hatua kwa hatua hatua ya kwanza ingia kwenye site ya Seebait.com kisha bonyeza sehemu iliyoandikwa Login/SignUp 
Itaonekana muonekano kama huu pichani
Itakuletea muonekano huo pichani , kwasababu sisi ndio tunahitaji kujipatia pesa kupitia Seebait.com basi tutaenda sehemu iliyoandikwa Select option you want to use kisha chagua mtandao unaohitaji kujisajili seebait kupitia mtandao ulioidhinishwa na seebai ambao ni Facebook, twitter na google+ hivyo nitakuonyesha kupitia google+ kwasababu bloggers wengi tunatumia google+
ukibonyeza google+ itakuomba idhini hivyo bonyeza Allow, 
Itakuwezesha kuingia katika dashibodi ya seebait kama inavyoonekana pichani kisha utucopy hizo code na kwenda kuzipaste kwenye blog yako
Katika dashidadi ya seebait walishakuelekeza sehemu ya kuweka , hivyo ingia kwenye blog yako bonyeza theme kisha edit Html, kisha search maneno haya <head> [ jinsi ya kutafuta code kwenye HTML bonyeza mouse yako mara moja kwenye code za templete yako kisha bonyeza Ctrl+F utaona sehemu ya kusearch] kisha paste code za seebait chini ya code hii <head>. save tempalte yako.
kisha rudi kwenye website ya seebait.com bonyeza sehemu inayosomeka Properties , kisha bonyeza Add Property 
Utaona fomu kama hiyo hapo juu pichani jaza fomu hiyo kama hapa chini pichani
Hiyo picha hapo juu ni mfano hivyo jaza kutokana na mahitaji ya blog yako hakikisha hauvunji sheria zaseebait.com, kisha ukimaliza bonyeza Submit
Ukisha submit itakuletea muonekano huo hapo juu kama umekidhi mahitaji ya seebait , lakini kuna vitu vitapungua kutokana na picha yangu ipo aproved lakini yako haitakuwa aproved kwasababu bado hajakubaliwa na kwenye status itakuonyesha not verify hivyo tumalizie hivi bonyeza sehemu yenye alama ya mshale ulioelekea chini unapatinaka upande wa kulia wa properties yako , utaidownload properties yako kupitia mshale huo, kisha ifungue kwa ku doble-click , itafunguka kupitia browser yako mimi nimetumia Chrome pichani hapa chini
Utaona code mfano wa hizo hapo juu sasa andaa code zako kwaajili ya ku verify akaunti yako ya seebait , pia seebait wameelekeza kuhusu kukamilisha hilo nenda juu kabisa kulia kwenye dashibodi ya seebait utaona alama ya magazine bonyeza hapo kisha tafuta Property Activation 
Utaona makala hiyo ya msaada wako imekuwa nambari moja bonyeza neno Read itafunguka makala kisha copy code hii <meta name=”seebait” content=”ACTIVATION CODE HERE” /> Kisha paste sehemu unayodhani utaweza kuiedit mimi huwa natumia notepad kisha irekebishe hapo kwenye neno ACTIVATION CODE HERE paste zile code za kwenye file ulilodownload kwenye properties hivyo code zako zitakuwa hivi <meta name=”seebait” content=”ryyady-bhay49d26e96ac7ebfc7c9t.html” /> Chukua code zako hizo ulizozitengeneza vema kisha nenda kapaste chini ya kwenye code hii <head> hii tulishazungumzia sehemu ya kuipata kwenye maelezo yetu hapo juu.
kisha rudi tena kwenye dashibodi ya seebait.com nenda kwenye properties kulia bonyeza alama ya TIKI au Nike utaona mabadiliko sehemu ya status itaandika Active. 
kufikia hapo umefanikiwa kuwa na akaunti ya seebait malizia kuweka matangazo kisha subiri seebait.comwaipitie fomu yako ya maombi kama umekamilisha utakuta notification kwenye dashibodi yako yaseebait.com
Mpaka hapo utakuwa umefanikiwa sasa jitahidi kutafuta Traffic kwa nguvu ili upate pesa zaidi
Kidokezo
Jinsi ya kuweka tangazo ingia kwenye dashbbodi ya seebait kisha bonyeza Ad Spaces kisha bonyeza Add Ad Space 
Andika jina la tangazo, kwenye category chagua ukubwa unao uhitaji kisha bonyeza submit
kisha copy code sehemu iliyoandikwa space code kisha ka paste sehemu unayotaka tangazo lako lionekane kwenye blog yako. HONGERA UMEFANIKIWA
Bila shaka umefanikiwa kama umezingatia vema maelezo hayo, lakini kama hujaelewa usisite kuniachia maoni yako hapo chini wapi hujaelewa nami nitakusaidia haraka iwezekanavyo, maoni yako sio lazima yawe kuhusu swali kama umeelewa unaweza kuacha mtazamo wako hapo chini maoni yote ninayapenda muhimu usitumie lugha chafu. sambaza makala hii kwa marafiki ili tupate mwangaza wa mafanikio pamoja karibu sana

from Blogger http://ift.tt/2mPCgyS
via IFTTT


Rais WB Kuweka Jiwe la Msingi ‘Flyover’ Ubungo…!!!

RAIS wa Benki ya Dunia (WB), Dk Jim Yong Kim anatarajiwa kuwasili nchini keshokutwa na Jumatatu ijayo akiwa na Rais John Magufuli, wataweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya juu (mzunguko) eneo la Ubungo, Dar es Salaam ambayo itasaidia kupunguza msongamano wa magari jijini humo.
Kwa mujibu wa taarifa ya Benki ya Dunia, atafanya ziara ya siku tatu nchini kuanzia keshokutwa na Dk Kim atakutana na Rais Magufuli na kufanya naye mazungumzo muhimu ya kuimarisha ushirikiano wa kimkakati baina ya Tanzania na benki hiyo na pia kutembelea miradi ya uwekezaji inayofadhiliwa na benki yake katika miundombinu na kusisitizia haja ya kuendelea kuunga mkono uwekezaji katika maendeleo ya jamii hususani ubora wa elimu na kuwekeza katika elimu ya awali.
Dk Jim akiwa na mwenyeji wake Rais Magufuli ataweka jiwe la msingi la ujenzi wa njia ya makutano eneo la Ubungo na pia atatembelea Shule ya Msingi Zanaki iliyopo Upanga.
Hii ni mara ya kwanza kwa Rais huyo wa Benki ya Dunia kutembelea Tanzania.
Benki ya Dunia hivi sasa inafadhili jumla ya miradi 23 ya kitaifa nchini yenye thamani ya dola za Marekani bilioni 3.6, na sehemu kubwa ya miradi hiyo inahusika na ujenzi wa miundombinu ya usafiri na miradi ya maendeleo vijijini.

from Blogger http://ift.tt/2mdQOMC
via IFTTT


Kategori

Kategori