Msanii wa muziki Diamond Platnumz amekanusha taarifa ambazo zimekuwa zikizagaa katika mitandao ya kijamii kuwa Hamisa Mobeto ana mimba yake.
Aidha muimbaji huyo amekanusha pia kuwahi kutoka kimapenzi na video queen huyo ambaye anatikisa katika tasnia ya urembo.
Akiongea katika kipindi cha XXL cha Clouds Fm Jumatano hii wakati akiutambulisha wimbo wake mpya ‘I Miss You’, Diamond amedai tetesi za yeye kutoka kimapenzi na Hamisa zilianza baada ya kufanya naye kazi katika project ya wimbo, Salome.
“Toka nimeshoot na Hamisa Mobeto wimbo wa Salome, watu wamekua wakituhusisha pamoja, ujauzito wa Hamisa sio wangu,” alisema Diamond. “Jamani mwenye mimba si ajitokeze, si unajua hata mtu wake atakuwa anajisikia vibaya,”
Pia muimbaji huyo amedai wasichana wengi ambao anafanya nao kazi upakaziwa kuwa anatoka nao kimapenzi.
Kylian Mbappe anatajwa kuwa na thamani ya zaidi ya euro 100m kiasi ambacho kinaweza kuweka rekodi mpya ya usajili, Mbape ana miaka 19 tu lakini kuna hawa wachezaji watano ambao nao ni hatari hadi sasa na walinunuliwa kwa pesa ndefu wakiwa hawajafikisha miaka 20.
5.Sergio Aguero. Mwaka 2006 alikuwa na umri mdogo tu wa miaka 17 ambapo klabu ya Atletico Madrid walimuona akiichezea klabu ya Independiente na kutokana na uwezo wake mkubwa waliona kiasi cha euro 15m kinatosha kumchukua mshambuliaji huyo.
4.Sergio Ramos. Beki wa kutumainiwa wa klabu ya Real Madrid lakini mwanzo alikuwa akikipiga Sevilla na ilipofika mwaka 2005 Real Madrid walimnunua Ramos kutoka Sevilla kwa dau la euro 18.5m akiwa na umri wa miaka 19 tu na sasa amekuwa mlinzi bora haswa.
3.Wayne Rooney. Mshambuliaji wa klabu ya Manchester United alinunuliwa akiwa na miaka 18 kutoka katika klabu ya Everton mwaka 2004 na katika michezo 460 ambayo ameichezea klabu ya Manchester United mshambuliaji huyo amefunga jumla ya mabao 198.
4.Gabriel Jesus(19). Ukiongelea kinda ambaye amefanya makubwa ndani ya muda mfupi ni Jesus, huwezi amini kwamba huyu Jesus ndio ambaye mwaka 2014 alikuwa akipaka rangi mitaani nchini Brazil, alinunuliwa kwa euro 27m kutoka Palmeiras na hadi sasa anaonekana bora sana kuendana na thamani yake.
5.Lucas Moura. Kama ilivyo kwa Jesus huyu naye ni Mbrazil ambaye alikuwa akikipiga katika klabu ya Sao Paulo na tangu akiwa hajafikisha miaka 15 vilabu vikubwa duniani vilishaanza kumgombani lakini PSG walifanikiwa kumsaini kwa euro 28m, alikuwa na miaka 19 tu wakati akisajiliwa.
Leo April 12 Rais Dkt John Pombe Magufuli amezindua awamu ya kwanza ya ujenzi wa reli ambayo itakayorahisisha usafiri wa Dar es Salaam hadi Morogoro kwa njia ya treni.
Inawezekana mtu akawa anaishi Morogoro na kufanya kazi zake Da es Salaam kwani usafiri utakuwa wa uhakika na haraka zaidi. Rapper Stamina ambaye ni mzaliwa na Morogoro anayefanya mishe zake Dar, amehaidi kurudi kuishi Moro na wakati huo huo akiendelea kufanya mishe zake Dar endapo njia hiyo ya usafiri itaanza kufanya kazi.
“Ikikamilika hiyo Rais, naenda kuishi zangu Morogoro tu,” ameahidi Stamina wakati akipiga story na Prince Ramalove kupitia Kings Fm Leo.
Aliyekuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Suleiman Kova amesema marafiki wengi wa viongozi si marafiki wa kweli bali ni marafiki wa zile nafasi walizonazo.
Kamanda Kova alisema hayo katika uzinduzi wa Chuo Cha Fursa (APEC) kilichopo maeneo ya Ukonga, mwishoni mwa wiki ambapo mkurugenzi wa chuo hicho alimualika kuhudhuria hafla hiyo.
“Mkurugenzi wa APEC, Respicius Timanywa, alikuja ofisini kwangu mwaka 2010 akitaka ushauri na kupata maelekezo kuhusu mtaala wa kufundishia bodaboda, tuliandaa pamoja naye, leo amenikumbuka kanialika katika uzinduzi wa chuo,” alisema Kamanda Kova.
Aliongeza “Ni watu wachache sana wanaoweza kukumbuka, wengi ni marafiki wa kiti chako sio wewe, ukitoka katika kiti ukimpigia simu hapokei na mwingine anaitika kisha anazima kabisa.”
Aidha Kamanda huyo alisema kwa sasa anajishughulisha na kutoa ushauri wa masuala ya maafa, majanga na uokoaji.
Mjini Johannesburg, mvulana wa miaka 10 alilazimishwa kulala kifudifudi wakati mama yake akibakwa kwa muda wa saa nne katika teksi, hii ni kwa mujibu wa ripoti kutoka Afrika kusini.
Mvulana huyo na mama yake wanadaiwa kulaghaiwa kuingia ndani ya gari dogo la abiria (teksi). Baada ya mama na mwanae kuingia ndani ya teksi, mvulana alilazimishwa kulala kifudifudi chini kwenye sakafu ya gari hilo, huku wanaume watatu wakimbaka mama yake. Kabla ya kufanyiwa vitendo hivyo mama aliamrishwa kukabidhi kadi yake ya benki pamoja na namba za siri (PIN) za kadi hiyo, na wanaume hao waliokuwa na bunduki.
Inadhaniwa kuwa kuwa hili lilikuwa ni shambulio la hivi karibuni la genge la majambazi.
Taarifa za kwanza za watu wanaotumia magari kufanya matukio ya ubakaji ziliripotiwa mwaka mmoja uliopita. Kwa mujibu wa rekodi za Roodeport, matukio ya awali ya ubakaji yaliripotiwa mwezi Machi 2016, huku matukio mengine matatu yakifanyika katika kipindi cha wiki ya mwisho ya mwezi Juni. Matukio yote yalifanyika katika eneo la Soweto mjini Johannesburg.
Hata hivyo haijabainika wazi kuwa ni mashambulio mangapi yaliyokwisha kutokea huko katika kipindi cha miezi 12 bila kuripotiwa, na kama yote yalitekelezwa na kundi hilo hilo.
Luteni Kanali Lungelo Dlamini amesema “Kikundi cha wanaume watatu ama wawili waliokuwa wakiendesha magari mawili tofauti ya [Toyota] Quantums, moja la rangi ya kijivu na jingine la rangi nyeupe, yaliwachukua wanawake wawili yakijifanya ni magari ya teksi, wakawapora kwa silaha na baadae kuwabaka.”
Bwana Dlamini amesema kuwa haijabainika wazi kuwa magari hayo ya Quantum yalikuwa yana njama moja ama kila moja lilikuwa linatekeleza uhalifu huo kivyake.
Hadi sasa, wanawake wawili , akiwemo mama wa mvulana huyo , wamekwisha zungumza na vyombo vya habari vya Afrika Kusini, kuelezea kilicho wasibu.
Muathiriwa huyo aliliambia shirika la habari la EyeWitness News kwamba alikuwa anaomba wakati wa tukio hilo wabakaji hao wasimuumize mwanae.
Afrika Kusini ni nchi iliyoripotiwa kuwa na matukio mengi zaidi ya ubakaji duniani.
TAZAMA HARMORAPA ALIVYO TIMUA MBIO BAADA YA KUIONA BASTOLA
Toka sakata la Makonda kuvamia,nimejipa muda kuangalia hii Tv,vipindi na nyimbo wanazopiga ni kama wanafikisha ujumbe kwa mkulu na RC wa Dsm.Wanapiga nyimbo za “vijembe” na leo wameimba wimbo wa “Solidality Forever” huku wameshikana mikono studio.
Leo asubuhi nimeangalia kipindi cha “Clouds 360”,nimesikiliza nukuu zilizotolewa na watangaji wote watatu, lakini nimefurahia zaidi nukuu ya pili ya mtangazaji Sam Sasali
“Kuanzia sasa nitasoma kila kitu, nitasoma kila gazeti liwe la michezo siasa na kila kitu sitaki kupangiwa, sitaki kupigiwa simu za maelekezo kwamba hiyo story soma au hiyo usisome”
Hii imetoa picha kuwa kumbe hawa jamaa huko nyuma walikuwa “wanatumika”,walikuwa wanapangiwa nini cha kusoma na kujadili kwa maslahi ya watu fulani.
Ndio maana katika siku zote za sakata la “Bashite na vyeti feki”,hawa Clouds inasemekana hawakulizungumzia sana wala kulijadili kwa mapana ktk vipindi vyao.Lakini toka jana na leo,kuanzia kipindi cha muziki cha XXL mpaka Alasiri ya Clouds Tv,mjadala wa vyeti ulianza kushika hatamu.
Huu ni ujumbe kwa hawa wamiliki wa vyombo vya habari,zama za unafiki zimekwisha,wasimamie ukweli,maana wengine wanashindwa kusimama na Clouds Media Group sbb kwa muda mrefu walikuwa kama tawi la chama na kitengo cha propaganda mpaka wengine “tukazila” kuwafuatilia.Hili ni fundisho kwao.