Showing posts with label 2017 at 11:44AM. Show all posts
Showing posts with label 2017 at 11:44AM. Show all posts
SERIKALI YAWAKANYA MAAFISA ARDHI NA MAAFISA MIPANGO MIJI

SERIKALI YAWAKANYA MAAFISA ARDHI NA MAAFISA MIPANGO MIJI

Na Hassan Mabuye Kitengo cha Mawasiliano, Wizara ya Ardhi
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi amewaonya maafisa ardhi na maafisa mipango miji wasio waadilifu na kusababisha kero za migogoro ya ardhi nchini.
Waziri Lukuvi aliyasema hayo leo katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Lugalo mjini Iringa wakati wa Uzinduzi wa Master Plan ya Halmashauri ya Manispaa ya Iringa.
Amesema mchezo huo wa ufisadi ambao umekuwa ukitumiwa miaka yote na maofisa ardhi nchini ameubaini na kuwataka wakurugenzi wa Halmashauri nchini kutokubaliana na ramani za maeneo mapya zinazoletwa na wataalam hao bila ya wao kufika maeneo husika na kuoneshwa maeneo hayo ili kujiridhisha.
Waziri Lukuvi amefichua kuwa ufisadi unaofanywa na maafisa ardhi nchini kwa kupima viwanja hewa kwa ajili ya maslahi yao na kusema kuwa mbinu ambayo wamekuwa wakiitumia kuiibia serikali amekwisha ibaini na hata kubali kuona mbinu hiyo inapewa nafasi katika serikali hii ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Pombe Magufuli .
Maafisa ardhi wakishirikiana na maafisa mipango miji pamoja na wapima wamekuwa wakitajirika sana kwenye idara zao na wanatakata kwa ujanjaujanja na ufisadi wanaoufanya kwa kutengeneza ramani zinazoonesha maeneo mazuri na muhimu katika miji kwamba hayafai kutumika, kumbe wameyauza maeneo hayo kwa mlango wa nyuma na kwa bei za juu.
Unakuta kwenye ramani inayonyesha kuna bonde kubwa lisilofaa kujengwa kumbe ukifuatilia eneo hilo ni zuri kuliko yote na hapo wametenga viwanja vya kuuza. Unakuta ukipima kuna viwanja vingi na vizuri ambavyo ni vyao wao wanachofanya baada ya kuuza viwanja halali za Halmashauri hurudi kupima maeneo hayo walioonyesha ni mabonde na kugawana wao kwa ajili ya kuuza kwa faida yao.
Lukuvi amesema kuwa wathamini nao pi wamekuwa wakiwapunja wananchi wasio elewa kwa kuwafanyia tathimini kubwa zaidi ya uhalisia wake na pindi pesa inapotoka utakuta nyumba inathamani ya milioni 7 wakati wao wanasema inathamani ya milioni 20 ili cha juu wapate wao.
“Wakati nilipokuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam niliweza kubaini ujanja wa wathamini baada ya eneo ambalo nyumba zake zina thamani kati ya milioni 20 hadi 50 kwa maana nyumba hizo ni za udongo ila maofisa hao walimtafuta mtu na kutafuta nyumba nzuri zaidi na kumshikisha kibao kisha kumpiga picha na kuandika kuwa nyumba hiyo inathamani ya zaidi ya milioni 200.”
Niliamua kufanya uchunguzi wangu na kumtafuta mtu aliyekwenye picha na kumbana ndipo aliniambia ukweli kuwa mthamini huyo ni ndugu yake hivyo walikubaliana pesa ikitoka atalipwa milioni 70 na milioni 130 ni za afisa huyo”
Hata hivyo alisema kuwa ujenzi holela katika miji na halmashauri imesababishwa na ukilitimba wa utoaji wa vibali kwa wakati na ndio sababu ya wananchi kuvamia maeneo yasiyo pimwa japo kuanzia sasa wote waliopo katika maeneo yasiyo pimwa watapewa leseni ya makazi ya miaka mitano na watalipa kodi ya ardhi na baada ya miaka mitano wahakikishe wamepimiwa ili kupewa hati.
Hivyo Lukuvi aliwataka maafisa ardhi na wathamini wa ardhi manispaa ya Iringa kutofanya kama maeneo mengine kwa kufuata mpango maeneo yote ambayo yameelekezwa kwenye Masta Plan hiyo na kwenda kutenda haki.
Katika hatua nyingine waziri Lukuvi alitoa agizo kwa wale wote waliopewa ardhi kwa ajili ya ujenzi wa hoteli na viwanda na wale waliouziwa viwanda vya serikali, hotel na mashamba ya serikali kuviendeleza haraka kabla ya ardhi hiyo haijapokonywa .
Nae Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bibi Amina Masenza akimkaribisha waziri Lukuvi amesema kuwa mkoa wa Iringa umeendelea kuhamasisha wananchi kuzingatia sheria na taratibu za ujenzi na kuachana na ujenzi holela na ndio sababu ya kuja na Masta Plan hiyo ambayo imeanzishwa na aliyekuwa mstahiki meya wa halmashauri hiyo Amani Mwamwindi.
Akitoa taarifa ya uandaaji wa Masta Plan hiyo kwa ajili ya mwaka 2015-2035 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Dkt William Mafwere, alisema kuwa dhumuni la mpango huo ni kutatua changamoto zilizokuwa zinaikabili Manispaa na kuwa dhana kuu ya mpango huo ni dhana unganishi ikijumuisha dhana nyingine.
Alisema jumla ya miradi 31 itatekelezwa katika awamu ya kwanza 2015-2020 kuwa baadhi ya miradi hiyo ni kituo cha mabasi Igumbilo, kituo hicho kimeanza ujenzi na hatua ya utekelezaji imefikia asilimia 30.
Nae Mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa alisema kuwa kazi inayofanywa na Waziri Lukuvi ni tofauti na mawaziri wengine kwani amekuwa ni waziri wa mfano katika kuchapa kazi.
“Kwa mnaonifahamu vizuri mimi sio mbunge wa kusifia sifia ni mbunge mwenye msimamo ila nampongeza sana Waziri Lukuvi ni waziri mchapakazi na kazi zake zinaonekana na ndio maana hata bungeni ni waziri pekee ambaye bajeti yake ilipitishwa kwa kishindo hata na sisi wabunge wa kambi ya upinzani.”
Mpango Kabambe ni chombo cha kuchochea utumiaji wa fursa zilizopo katika mji, kuongeza kasi ya upangaji, upimaji na umilikishaji wa ardhi kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii na kupunguza na kumaliza migogoro ya ardhi. kudhibiti ujenzi holela mijini na hutumika pia kuongoza, kusimamia na kudhibiti ukuaji na uendelezaji wa mji na kutoa uhakika kwa wawekezaji katika Halmashauri za Manispaa ya husika.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akiwaonya maafisa ardhi na maafisa mipango miji wasio waadilifu na kusababisha kero za migogoro ya ardhi nchini wakati wa uzinduzi Master Plan ya mji wa Iringa.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akimkabidhi kitabu cha Master Plan ya mji wa Iringa Meya wa Halmashauri ya Iringa Alex Kimbe.


Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akiteta jambo na Meya wa Halmashauri ya Iringa Alex Kimbe na Mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akipongezwa na Mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa mara baada ya Uzinduzi wa Master Plan ya mji wa Iringa.

Baadhi ya wakazi wa mji wa Iringa waliofika kushuhudia Uzinduzi huo.

from Blogger http://ift.tt/2tytLPX
via IFTTT


UAMUZI WA MWISHO WA ZITTO KABWE KUGOMBEA URAIS TFF

UAMUZI WA MWISHO WA ZITTO KABWE KUGOMBEA URAIS TFF

Mwanasiasa machachari na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe amesema kuwa hawezi kugombea Urais wa TFF kutokana na kuwa na majukumu mengi katika ngazi ya chama na jimboni.
Zitto ambaye pia ni Kiongozi wa ACT Wazalendo kupitia taarifa aliyoweka katika ukurasa wake wa Facebook amesema kuwa licha ya kuombwa na kushawishiwa na wengi kugombea, lakini yeye mwenyewe ameona kuwa hatokuwa na muda wa kutosha kutumikia kofia zote tatu atakazokuwa nazo.
Hapa chini ni ujumbe wa Zitto alioandika leo asubuhi.
Ijumaa ya Aprili 21, mwaka huu, gazeti la michezo na burudani nchini, Mwanaspoti, liliandika habari kwenye ukurasa wake wa kwanza yenye kichwa: “Zitto ajitosa Urais TFF, Rage amkubali.”
Upande wangu, licha ya kwamba habari hiyo ilichapishwa bila kupata maoni yangu, lakini haikuwa ngeni. Hii ni kwa sababu kabla ya habari hiyo nilikuwa nimeshapokea maombi kutoka kwa watu mbalimbali, wakiwemo viongozi wakubwa wakinitaka nigombee Urais TFF.
Baada ya habari hiyo kuchapishwa na kupata umaarufu mkubwa, nilipokea maombi mengi zaidi pamoja na shinikizo lenye kunitaka muda ukifika wa uchukuaji fomu, nijitokeze nichukue fomu ya kuwania Urais TFF.
Msukumo ni mkubwa na maswali ni mengi kipindi hiki ambacho dirisha la uchukuaji fomu za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi TFF limefunguliwa.
Kila ombi na shinikizo ambalo nimepokea, nimelibeba kwa unyenyekevu mkubwa. Bila shaka wanaoniomba na kunishinikiza wanavutwa na mambo mawili; mosi, soka letu kutoleta nuru kwa Watanzania. Pili, imani kubwa kwamba kupitia uongozi wangu nuru ya soka letu itadhihirika.
Hata hivyo, yapo mambo mawili nimeyatafakari; Mosi, mahitaji ya soka letu na nguvu ya maarifa inayohitajika kulikwamua. Pili, nafasi yangu kama mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini na Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo.
Kuhakikisha kazi ya kulikwamua soka letu inafanikiwa na nuru inadhihirika kwa wapenda soka wote nchini, inahitaji uwekezaji mkubwa wa muda, vilevile uwekezaji mkubwa wa maarifa ya kiuongozi.
Soka la Tanzania lipo hapa kwa sababu ya uwekezaji usioridhisha wa maarifa ya uongozi, hiyo inatokana pia na viongozi wanaopata nafasi ya kulitumikia shirikisho letu la mpira wa miguu nchini, kutowekeza muda wao barabara kwenye soka.
Nikiwa Kiongozi wa ACT-Wazalendo, ninadaiwa mambo mawili, uwekezaji wa muda na uwekezaji wa maarifa ya kiuongozi ili kukiandaa vema chama chetu kushiriki uchaguzi kati ya miezi 28 mpaka 40 inayokuja.
Mwaka 2019, Chama kitashiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa, mwaka 2020, Chama chetu kitashiriki Uchaguzi Mkuu.
Hivyo basi, kwa kuongezea na uwakilishi wangu wa Jimbo la Kigoma Mjini ambako Chama chetu kinaongoza Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji, naona kuwa lipo eneo ambalo nitashindwa kulitimizia wajibu wake nikivaa kofia ya tatu ya Urais wa TFF.
Nimetafakari na kuchukua uamuzi kwamba Uongozi wa ACT-Wazalendo na Ubunge ni nafasi ambazo ninazo tayari, wakati Urais TFF ni nafasi mpya.
Kwa hali hiyo na kwa mapenzi makubwa ya soka la Tanzania, nimeamua nisichukue fomu ya kugombea Urais wa TFF, kwani naweza kuomba kazi ambayo nitashindwa kuitumikia kwa muda wa kutosha kutokana na majukumu yangu kwenye Chama na ubunge.
Uamuzi huu umezingatia mapenzi makubwa kwa soka letu. Nikijitokeza kuwania Urais wa TFF leo halafu nikakosa muda mzuri wa kutimiza matarajio ya wapenda soka nchini, utakuwa usaliti mkubwa kwa maendeleo ya soka la Tanzania.
Nawashukuru wote walioniomba na kunishinikiza nichukue fomu. Nawaambia kuwa kwa sasa tujielekeze kupata viongozi bora miongoni mwa watakaojitokeza. Wakati mwingine mazingira yakiruhusu, nitaweza kutii maombi hayo.
Asante sana.
Zitto Zuberi Kabwe Ruyagwa
 ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2rHbHT1
via IFTTT


Nay wa Mitego Adai Anatafutwa Kuuawa

Nay wa Mitego Adai Anatafutwa Kuuawa

“Usalama wa Maisha yangu umekua Mdogo kwasasa, Wana panga kunipoteza ikibidi nisiwepo kabisa kwenye hii Dunia. Nipo tayari kwa chochote wanacho panga kufanya Coz sijajipanga kupambana nao, Mimi ni Mwana Muziki si vingine. Kwa chochote kitachotokea Familia yangu itakua na chakuongea. Siwezi kuhama Nchi wala kukimbia nitafia hapa hapa. Na siko tayari kupindisha Chochote.! Nyie Ndo mtanilinda. Sina Mlinzi na sitarajii kua na mlinzi. OnlyGod
#Wapo
#Truth”
Ameandika Hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram

from Blogger http://ift.tt/2nSorRz
via IFTTT


Elibariki Kingu: Kwa Hili la Makonda, Naomba Niwe wa Kwanza kufukuzwa CCM..!!!

Nilisema Nitanyamaza lakini Nimeshindwa. Nimethibitisha bila mashaka Clouds kuvamiwa na Rc akiwa na ulinzi na askari wenye silaha mpaka kwenye matangazo.
Najua hofu mliyonayo watanzania juu ya huyu Rc.
Ikiwa mamlaka zitaendelea kufumbia macho.Mimi Elibariki Immanuel Kingu mbunge wa CCM nitakuwa wa kwanza kufukuzwa CCM kama kupinga matendo maovu ya Rc huyu itaonekana ni usaliti kwa nchi.
Haiwezekani Rais wetu atukanwe kila kona kwa matendo ya mtu huyu.
Wana CCM ukimya wetu kwenye hili halikubaliki.
Magufuli juzi ametuliza Dodoma kwa kuongea kwa hisia.Idara za usalama kweli mmeamua kuacha tutukanwe?
Naomba sasa niweke kumbukumbu sawa najua mnamchafua kila anayempinga RC huyu kwa matendo yake ambayo yanakiuka utawala bora.
Naomba niwe wa kwanza kufukuzwa CCM kwa kumpinga Rc Makonda
Elibariki Immanuel Kingu

from Blogger http://ift.tt/2ncZu4Z
via IFTTT


Kategori

Kategori