Showing posts with label 2017 at 11:22AM. Show all posts
Showing posts with label 2017 at 11:22AM. Show all posts
Ajib Ataka Milioni 60 Asaini Singida United..!!! ajib, Simba KIUNGO Mshambuliaji wa Simba, Ibrahim Ajib, amewataka Singida United kumpa Sh milioni 60 ili wapate saini yake kwa ajili ya kuwatumikia msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara. Ajib ambaye kaonyesha nia ya kuondoka Simba baada ya mkataba wake kuisha na kwenda kutafuta changamoto nyingine ya soka, jina lake limetajwa na kocha Hans Pluijm kwenye kikosi chake. Tayari mchezaji huyo amekwishaweka bayana kuwa anahitaji fedha hizo na endapo itashindikana, hawezi kujiunga na timu hiyo mpya kwenye Ligi Kuu msimu ujao. Mbali na Ajib pia timu hiyo imeonyesha nia ya kumtaka mchezaji wa Yanga, Deus Kaseke ambaye naye anahitaji Sh milioni 40. Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Singida United, Festo Sanga, alithibitisha kufanya mazungumzo na wachezaji hao, lakini bado hawajafikia hatua ya kuwafanya wasaini katika klabu hiyo. “Ni kweli tunawahitaji na tumefanya nao mazungumzo na tumeweka wazi kiasi ambacho tunacho mkononi, ila inaonekana wao bado hawapo tayari, hivyo tunawasubiri wao wakiwa tayari sisi hatuna shida muda wowote wakitufuata tutasaini,” alisema Sanga. Alisema kuwa malengo yao msimu huu ni kusajili wachezaji 25, wapya wakiwa 14, saba kutoka nje na saba wengine kutoka ndani, huku mpaka sasa wachezaji wa ndani bado watatu kwa kuwa wamesajili wawili tu.

Ajib Ataka Milioni 60 Asaini Singida United..!!! ajib, Simba KIUNGO Mshambuliaji wa Simba, Ibrahim Ajib, amewataka Singida United kumpa Sh milioni 60 ili wapate saini yake kwa ajili ya kuwatumikia msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara. Ajib ambaye kaonyesha nia ya kuondoka Simba baada ya mkataba wake kuisha na kwenda kutafuta changamoto nyingine ya soka, jina lake limetajwa na kocha Hans Pluijm kwenye kikosi chake. Tayari mchezaji huyo amekwishaweka bayana kuwa anahitaji fedha hizo na endapo itashindikana, hawezi kujiunga na timu hiyo mpya kwenye Ligi Kuu msimu ujao. Mbali na Ajib pia timu hiyo imeonyesha nia ya kumtaka mchezaji wa Yanga, Deus Kaseke ambaye naye anahitaji Sh milioni 40. Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Singida United, Festo Sanga, alithibitisha kufanya mazungumzo na wachezaji hao, lakini bado hawajafikia hatua ya kuwafanya wasaini katika klabu hiyo. “Ni kweli tunawahitaji na tumefanya nao mazungumzo na tumeweka wazi kiasi ambacho tunacho mkononi, ila inaonekana wao bado hawapo tayari, hivyo tunawasubiri wao wakiwa tayari sisi hatuna shida muda wowote wakitufuata tutasaini,” alisema Sanga. Alisema kuwa malengo yao msimu huu ni kusajili wachezaji 25, wapya wakiwa 14, saba kutoka nje na saba wengine kutoka ndani, huku mpaka sasa wachezaji wa ndani bado watatu kwa kuwa wamesajili wawili tu.

KIUNGO Mshambuliaji wa Simba, Ibrahim Ajib, amewataka Singida United kumpa Sh milioni 60 ili wapate saini yake kwa ajili ya kuwatumikia msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Ajib ambaye kaonyesha nia ya kuondoka Simba baada ya mkataba wake kuisha na kwenda kutafuta changamoto nyingine ya soka, jina lake limetajwa na kocha Hans Pluijm kwenye kikosi chake.
Tayari mchezaji huyo amekwishaweka bayana kuwa anahitaji fedha hizo na endapo itashindikana, hawezi kujiunga na timu hiyo mpya kwenye Ligi Kuu msimu ujao.
Mbali na Ajib pia timu hiyo imeonyesha nia ya kumtaka mchezaji wa Yanga, Deus Kaseke ambaye naye anahitaji Sh milioni 40.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Singida United, Festo Sanga, alithibitisha kufanya mazungumzo na wachezaji hao, lakini bado hawajafikia hatua ya kuwafanya wasaini katika klabu hiyo.
“Ni kweli tunawahitaji na tumefanya nao mazungumzo na tumeweka wazi kiasi ambacho tunacho mkononi, ila inaonekana wao bado hawapo tayari, hivyo tunawasubiri wao wakiwa tayari sisi hatuna shida muda wowote wakitufuata tutasaini,” alisema Sanga.
Alisema kuwa malengo yao msimu huu ni kusajili wachezaji 25, wapya wakiwa 14, saba kutoka nje na saba wengine kutoka ndani, huku mpaka sasa wachezaji wa ndani bado watatu kwa kuwa wamesajili wawili tu.

from Blogger http://ift.tt/2sHatTX
via IFTTT


IMEFICHUKA..Amri Hii ya Kikwete Iliitia Nchi Hasara ya Mabilioni ya Pesa..Mbunge Afichua A – Z Jinsi Ilivyokuwa..!!!

IMEFICHUKA..Amri Hii ya Kikwete Iliitia Nchi Hasara ya Mabilioni ya Pesa..Mbunge Afichua A – Z Jinsi Ilivyokuwa..!!!

AGIZO la Rais wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete kujengwa maabara kwa kila shule ya sekondari nchini limebainika kutumika kama mwanya wa watendaji wa serikali kufuja fedha za umma.
Aidha, agizo hilo limebainika kukamilisha miradi mingi ya maendeleo iliyokuwa imepangwa kutekelezwa katika bajeti kwa miaka ya fedha 2013/14 na 2014/15.
Novemba 4, 2012, Kikwete, maarufu JK, aliwaagiza wakuu wa mikoa na wilaya nchini, kujenga maabara kwa kila shule ya sekondari katika kipindi cha miaka miwili kuanzia siku hiyo.
JK alitoa agizo hilo alipohutubia wananchi wa Jimbo la Manyoni Magharibi mkoani Singida, waliohudhuria mkutano wa hadhara uliofanyika katika mji mdogo wa Itigi.
Alisema maabara za sayansi ni muhimu katika maendeleo ya wanafunzi kujifunza kwa nadharia na vitendo. JK alisema kutokana na umuhimu huo, kulikuwa kunahitajika ushirikiano kama ule ulioonyeshwa wakati wa ujenzi wa shule za sekondari za kata ulioanza mwaka 2006.
Hata hivyo, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) imekosoa utaratibu huo na kufichua ufujaji wa mabilioni ya shilingi uliofanywa na watendaji wa halmashauri na kukwamisha utekelezaji wa miradi mingi ya maendeleo, wakidai pesa zimeelelekezwa kwenye ujenzi wa maabara.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Vedasto Ngombale, ndiye aliyefichua kadhia hiyo katika mahojiano na Nipashe kwenye viwanja vya Bunge mjini hapa.
Alisema kuwa kutokana na tamko hilo la JK, watendaji wa halmashauri walilazimika kuelekeza kwenye ujenzi wa maabara fedha zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya miradi mingine ya maendeleo, huku baadhi yao wakipata mwanya wa kufuja fedha za umma kwa kisingizio kwamba wamezielekeza kwenye utekelezaji wa agizo la Rais.
“Kilichotokea lile lilikuwa tamko, lakini katika maeneo mengi hapakuwa na bajeti kwa ajili ya utekelezaji wa jambo hilo,” Ngombale alisema.
“Kama unavyofahamu, ili kutekeleza mradi wowote katika serikali, sharti kwamba mradi huo utajwe kwenye bajeti, lakini Mheshimiwa Kikwete, kwa mamlaka aliyokuwa nayo, akatoa tamko la utekelezaji wa jambo hilo.
“Sasa kilichotokea ni kwamba baada ya tamko lile, watendaji wa halmashauri kwa maana ya wakurugenzi watendaji, walichokifanya ni kuchukua pesa kutoka katika kasma mbalimbali kuhakikisha kwamba wanatengeneza maabara.
“Na matokeo yake, tulipokuja kupitia yale mahesabu baada ya utekelezaji, kukawa kumebainika kuna ufujaji mkubwa wa pesa katika halmashauri nyingi.”
Ngombale ambaye pia ni Mbunge wa Kilwa Kaskazini (CUF), alisema licha ya tamko hilo kusababisha kutumika kwa mabilioni ya shilingi yaliyokuwa yametengwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo ikiwamo ya maji, mpaka sasa bado kuna halmashauri nyingi hazijakamilisha ujenzi wa maabara, akiitolea mfano halmashauri ya Kilwa anayotoka.
Zipo halmashauri nyingi ambazo bado hazijakamilisha ujenzi wa maabara hali ya kwamba tamko hilo lilitolewa na utekelezaji ulifanyika kwa kuchukua pesa kutoka katika mafungu tofauti tofauti,” alisema Ngombale.
Mtoto huyo wa kaka mdogo wa mwanasiasa mkongwe, Kigunge Ngombale Mwiru, alisema agizo hilo la JK lilitolewa bila kuwa na bajeti, hivyo fedha za miradi mingine zilikuwa zinachukuliwa na kuingizwa kwenye ujenzi wa maabara, kinyume cha sheria ya bajeti ya mwaka husika.
“Lakini, katika utekelezaji huo, ndiyo mwanya wa matumizi mabaya ya pesa ulipatikana na sisi tulivyokagua, tumeona ni kiasi gani. Kuna ufisadi mkubwa,” alisema.

from Blogger http://ift.tt/2pVm7dd
via IFTTT


Huyu Ndiye Mwakyembe Bwana..Soma Hapa Maneno Aliyompokea Nayo Nay a Mitego Baada ya Kufika Dodoma…Lazima Ucheke Aisee..!!!

Rapper Nay wa Mitego, Alhamis hii aliitikia wito wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt Harrison Mwakyembe kukutana naye mjini Dodoma kwaajili ya kuzungumza namna ya kuuboresha wimbo wake Wapo ambao licha ya kuikosoa vikali serikali pamoja na Rais Dkt John Magufuli umepokelewa kwa mikono miwili.
Hatua hiyo ilikuja baada ya Rais Magufuli kuamuru kuachiwa huru kwa Nay ambaye alikuwa amekamatwa na polisi na wimbo wake kufungiwa na BASATA. Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma, Dkt Mwakyembe alisema wasanii wana nafasi kubwa katika kuisaidia serikali kukemea mambo maovu.
Amewataka vijana kutambua kuwa Tanzania ni nchi inayozingatia utawala wa sheria na kwamba wana uhuru wa kukosoa bila kutukana au kwenda nje ya maadili. “Na ndio maana tukasema kwa wimbo wa Nay hapana, hebu ngoja tuusikie, mbona ni wimbo mzuri tu,” alisema Mwakyembe.
Tazama video Mtoto amvua kofia
 Papa Francis

from Blogger http://ift.tt/2ofWYvJ
via IFTTT


Mwakyembe: Huwezi Kuwa Hakimu wa Kesi Yako Mwenyewe…..Ripoti ya Uvamizi Clouds Media Inamapungufu, Sitaipeleka Ngazi za Juu

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe leo amezungumza na waandishi wa habari Mjini Dodoma mara baada ya kukaribishwa rasmi Wizarani hapo..
Baada ya maongezi aliruhusu mwaswali ambapo moja ya swali aliloulizwa na wanahabari ni kuhusu ripoti iliyoachwa na Waziri wa zamani Nape Nnauye kuhusu uchunguzi wa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kudaiwa kuvamia ofisi za Clouds Media huku akiwa na Askari wenye silaha.
==>Haya ni majibu aliyoyatoa
“Wengi mnauliza nimeifanyia kazi gani ripoti ya Nape, mimi hiyo ripoti sijaiona na kama mwanasheria kwangu ni mwiko na sitapeleka taarifa ambayo haijakamilika.
“Kupitia vyombo vya habari taarifa imeeleza kuwa ushahidi ulitolewa na upande wa Clouds Media na mkakiri kuwa upande wa pili haukupatikana.
“Huwezi kuwa Hakimu kwenye suala lako wewe mwenyewe, kufanya hivyo ni ubatili kwahiyo hata mimi ningekuwa ni mwandishi wa habari ningesema hili jambo siliwezi kwakuwa linanihusu na mimi.
“Kanuni zinataka kusikiliza upande wa pili, sasa mmeshasema kitu kina upande mmoja alafu nimpelekee kiongozi wangu..NO, mimi kazi yangu ni kupata maelezo ya upande wa pili na nitapata.
“Hili jambo ni lakufa na kupona, yani niache kukutana na wakuu wa idara mbalimbali hapa kuhakikisha nakuza suala la sanaa na kuhakikisha vijana wetu hawaendelei kuibiwa nibaki kuhangaikia suala la ripoti.
“Mimi sikuapa kwa jambo hilo moja pekee lakini mimi ni mwanasheria mkongwe na nitahakikisha nalifuatilia lakini mimi sitaunda kamati katika jambo hilo.
“Lengo letu ni kuhakikisha hatutakuwa na matukio ya namna hiyo katika safari lakini tukitoka na kauli za papara tutakuwa tunajitafutia matatizo hapo mbeleni”
Tazama video Mtoto amvua kofia Papa Francis

from Blogger http://ift.tt/2odNGAD
via IFTTT


Noma Sana..Dude Atoa Yake ya Moyoni Kuhusu Aliyoyafanya Rais Magufuli Kwenye Mkutano wa CCM,Adai Alishangazwa na …!!!!

BAADA ya baadhi ya mastaa wa filamu kuungana na wanachama wa CCM kwenye Mkutano Mkuu uliofanyika mkoani Dodoma hivi karibuni, msanii Kulwa Kikumba ‘Dude’ alijikuta akipagawa baada ya Rais Dk. John Magufuli kuwapongeza wasanii.
Akizungumza na Risasi Mchanganyiko, Dude alisema Rais Magufuli alimfurahisha kwani ni kwa mara ya kwanza wasanii waliofika kwenye mkutano huo kila mmoja alitambulishwa kwa majina yake tofauti na miaka mingine huku akiwapongeza kwa kuungana nao katika mkutano huo.
“Nilifurahi sana kwa kweli maana kule kwenye mkutano Rais Magufuli alitupa kipaumbele na kutupongeza kwamba siyo kama wale wengine waliopata matatizo kidogo na kukimbia kwenye chama huku tukiahidiwa kuwa serikali itatuandalia sera nzuri ya filamu ili kuvuta wawekezaji,” alisema Dud

from Blogger http://ift.tt/2mjVcJY
via IFTTT


Marufuku Kufunga Ndoa Bila Cheti cha Kuzaliwa..!!!

Marufuku Kufunga Ndoa Bila Cheti cha Kuzaliwa..!!!

Serikali imepiga marufuku watu kufunga ndoa bila kuwa na cheti cha kuzaliwa kuanzia Mei Mosi, mwaka huu.
Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe ametangaza utaratibu huo mpya hii leo, akiwa ziarani Mkoani Morogoro na kuongeza kwamba, serikali imeamua kufanya hivyo ili kupata takwimu sahihi za wananchi wake zitakazosaidia kupanga mipango ya kimaendeleo sawia na kuzuia wageni kuingia kinyemela nchini.
Pamoja na mambo mengine, Dkt. Mwakyembe ameitaka Wakala wa Usajili wa Vizazi na Vifo, (RITA), kuhakikisha inasimamia Sheria ya Usajili ambapo amesema, bila kuwa na takwimu sahihi za vizazi na vifo ama ndoa inasababisha nchi kushindwa kusonga mbele kimaendeleo.
Amesema, kwa mfano Mkoa wa Morogoro kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012, inaonesha kuna jumla ya wakazi milioni 2.2, lakini waliosajiliwa na kuwa na vyeti vya kuzaliwa ni asilimia 11 pekee huku wengine wakiwa bado hawasajiliwa,

from Blogger http://ift.tt/2mW1pKO
via IFTTT


Kategori

Kategori