Showing posts with label 2017 at 11:17AM. Show all posts
Showing posts with label 2017 at 11:17AM. Show all posts
Kukamatwa Kwa Viongozi wa TFF na Takururu..Haji Manara Awatumia Pole ikiwa na Dongo Ndani yake

Kukamatwa Kwa Viongozi wa TFF na Takururu..Haji Manara Awatumia Pole ikiwa na Dongo Ndani yake

Baada ya taarifa za kukamatwa kwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF, Jamal Malinzi na Katibu Mkuu wake Mwesigwa Celestine leo mapema msemaji mkuu wa klabu ya Simba (aliyesimamishwa), Haji Manara ametoa pole kwa viongozi hao.
Haji Manara amesema sisi kama wanadamu tunapitia changamoto nyingi sana hivyo ni bora tukafarajiana japo hata kwa kupeana pole pale mwenzio anavyopatwa na matatizo.
“Poleni Viongozi wangu wa TFF,no matter wat!!ni challenges tu ktk life, bnadaam hatufai kuombeana mabaya,hata kama huwakukutendea haki, Mungu awasimamie kutendewa HAKI,“ameandika Haji Manara kwenye ukurasa wake wa Instagram.
Haji Manara ambaye alipigwa ‘STOP’ na TFF ya kutokujihusisha na masuala ya soka kwa mwaka mmoja kwa makosa ya kinidhamu bado anaendelea na msimamo wake wa kuitumikia klabu yake ya Simba kama kawaida kwani alilitaka Shirikisho hilo limpe barua ya kumsimamisha.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2ske5iH
via IFTTT


Mwanafunzi Azidiwa na Kukimbizwa Hospitali Baada ya Mwalimu Kumchapa Viboko 10..!!!

Mwanafunzi wa darasa la tatu katika shule ya msingi madeke halmashauri ya wilaya ya njombe mwenye umri wa miaka 10 inadaiwa kuwa anaendelea kuugulia maumivu ya adhabu ya kuchapwa viboko visivyopungua 10 na mwalimu wake wa hesabu baada ya kufeli somo hilo hapo machi 21 mwaka huu
Kwa mujibu wa baba mzazi wa mtoto huyo Bonface Manga Kwa masharti ya kutorekodiwa na waandishi mwanae Hosea Manga alichapwa viboko kumi na mwalimu wake na kisha akazidiwa na kukimbizwa hospitali.
Kutoka hospitali ya teule ya Mkoa wa Njombe Kibena ambako mtoto huyo amelazwa hali yake bado ingali si nzuri kwa kuwa hawezi kusimama wala kutembea licha ya kaimu mganga mfawidhi Wa hospitali hiyo Isaya mvinge kueleza kuwa uchunguzi wa kitabibu bado unaendelea
Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Njombe Kupitia Mkurugenzi Mtendaji monica kwiluvya anakiri kupokea taarifa kwa njia ya simu kutoka kwa afisa elimu kata kuwa mwalimu aliyehusika anashikiliwa na polisi
Jitihada za kupata taarifa ya jeshi la polisi zimegonga mwamba baada a kamanda wa jeshi la polisi kueleza kuwa yuko nje ya mkoa kikazi.
TAZAMA HARMORAPA ALIVYO TIMUA MBIO BAADA YA KUIONA BASTOLA

from Blogger http://ift.tt/2o2ilh7
via IFTTT


ZITTO Kabwe Ampongeza Kamanda Tundu Lissu

CHAMA cha ACT-Wazalendo kinachoongozwa na Zitto Kabwe, kimempongeza Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, kwa kushinda kiti cha urais wa Chama cha Wanasheria (TLS) katika uchaguzi uliofanyika juzi jijini Arusha.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Naibu Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo, Msafiri Mtemelwa, alisema Lissu anastahili pongezi kwa kufanikiwa kushinda nafasi hiyo kutokana na changamoto zilizomkumba katika kuisaka.
Alisema kuwa licha ya kupitia misukosuko mingi iliyokuwa inaonyesha njia ya kumkwamisha kufikia malengo yake, Lissu hakukata tamaa na alionyesha ujasiri.
Mtemelwa alisema kupata nafasi hiyo kwa kiongozi kutoka upinzani ni dalili njema na kipimo kwa wapinzani na kwamba anapaswa kuitendea haki nafasi hiyo kwa ustawi wa vyama hivyo vya upinzani.
“Mimi niseme tu kwamba, Lissu anastahili pongezi,” Mtemelwa alisema. “Tunahitaji watu kama hawa, watu majasiri. Pamoja na kwamba alipata misukosuko mingi, alipambana na akapenya.
“Sisi tuliopo upinzani, tunajua palivyopagumu, tunapambana sana na kukamatwa kamatwa. Pasipo kupambana, huwezi kupenya.
Kwa hiyo, (Lissu) anastahili pongezi, amepambana na hii ni ishara na kipimo kizuri kwa wapinzani, anatakiwa kufanya mazuri ili awaonyeshe kwamba wapinzani wanaweza, italeta sifa nzuri kwa wapinzani, vivyo hivyo akifanya vibaya italeta sifa mbaya.”
Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), aliibuka kidedea katika uchaguzi huo akipata kura 1,411 kati ya 1,682 zilizopigwa.
Kabla ya uchaguzi huo, Lissu alikumbana na changamoto kadhaa ikiwa ni kufunguliwa kwa kesi Dar es Salaam na Dodoma na mawakili wawili wakitaka usimamishwe kwa madai ya kuwapo kwa kasoro katika kanuni za uchaguzi huo.
Aidha, Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe, pia alikaririwa akitishia kukifuta chama hicho iwapo kitakuwa na mwelekeo wa kisiasa kauli ambayo ilionekana kumlenga Lissu.

from Blogger http://ift.tt/2n5z9p3
via IFTTT


Kategori

Kategori