Showing posts with label 2017 at 11:13AM. Show all posts
Showing posts with label 2017 at 11:13AM. Show all posts
Mbunge Mwingine CHADEMA Asimamishwa Kuhudhuria Vikao vya Bunge

Mbunge Mwingine CHADEMA Asimamishwa Kuhudhuria Vikao vya Bunge

Kamati ya Haki Kinga na Madaraka ya Bunge imependekeza Mbunge wa Viti Maalum (Chadema) Conchesta Rwamlaza asimamishwe kuhudhuria vikao vitatu vya mkutano wa saba unaoendelea wa Bunge la bajeti baada ya kumtia hatiani kwa kusema uongo.


Julai 11 mwaka jana akichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Rwamlaza alimtuhumu Mbunge wa Muleba Kusini (CCM) Profesa Anne Tibaijuka kuwa wakati akiwa Waziri wa wizara hiyo alitumia vibaya madaraka yake.
Rwamlaza alimtuhumu Tibaijuka kwa kujimilikisha zaidi ya ekari 4000 katika Kijiji cha Kyamnyorwa na kwamba kiasi hicho cha ardhi ni zaidi ya kiasi alichoomba kihalali ambacho ni ekari 1098.
Akisoma mapendekezo ya kamati hiyo leo (Jumatano) mwenyekiti wa kamati hiyo, George Mkuchika amesema kauli hizo zilimshushia heshima Profesa Tibaijuka mbele ya Bunge na jamii anayoiongoza.
Pia amesema kauli hiyo zilikuwa zikimgombanisha Profesa Tibaijuka na wananchi wa eneo hilo ambalo lipo ndani ya jimbo lake.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2s4cnOl
via IFTTT


Je Wajua ..Simba Hujitibu Maradhi Mbalimbali Yanayomsumbua kwa Kula Majani…!!!!?

Je Wajua ..Simba Hujitibu Maradhi Mbalimbali Yanayomsumbua kwa Kula Majani…!!!!?

SIMBA ni miongoni mwa wanyama ambao ni jamii ya paka, ukiondolea mbali kwamba ndiye mnyama mkubwa anayewinda katika jamii yao hiyo, lakini pia ni wanyama ambao hupenda kuishi kwa makundi makundi. Kwa lugha nyingine naweza kusema wanaishi kifamilia kama ilivyo kwa binadamu na familia zao huweza kuwa na simba takribani kumi na watano.
Njia rahisi ya kuwatambua kwa jinsia zao ni muonekano pamoja na majukumu, wakati simba dume shingoni likiwa limejaa manyoya mengi, simba jike huwa na manyoya sawa mwili mzima, hapo ni kwa mtazamo wa namna wanavyoonekana.
Katika majukumu, simba hugawana kazi ya kuhakikisha chakula cha kutosha kinapatikana katika familia, hilo ni jukumu la simba jike na simba jike aendapo mawindoni jukumu la simba dume ni kulinda mipaka tu. Uzito wa mnyama huyu huwa kati ya kilo 120 mpaka 240 inategemea na umri pamoja na afya.
Uhai wa simba kuishi ni kati ya miaka 10 mpaka 14 lakini kwa simba wa Afrika hufika hadi miaka 17 na zaidi. Simba huanza kufundisha mbinu za uwindaji watoto wake tangu wakiwa wadogo kabisa, ambapo huwatanguliza mbele na kuanza kuwabughuzi kwa kuwapiga piga ngwala, jambo ambalo hufanya watoto wake kuwa wenye hasira na wakali sana na mbinu hizo ndio hutumia akiwa anawinda ukubwani.
Simba mara zote hupendelea kukaa sehemu ambazo kuna miamba mizuri, pamoja na nyasi kavu kavu ambazo hufanana kwa mbali na rangi yake, kwakuwa huishi kifamilia dume ndio huanzisha makazi mapya, ambapo likiunguruma kwa sauti yake, sauti hiyo husafiri umbali mrefu na sehemu inayoishia ndio huwa mpaka wa makazi yao na kama katikati ya sauti hiyo itakumbana na makazi ya simba wengine, basi dume jingine litaitikia, hapo kinachofuata ni simba hao kuhama lakini kama hawatakubaliana kutoka basi madume ya pande hizo mbili yatakutana kuoneshana ubabe na litakalokubali kushindwa litaondoka na familia yake.
Simba dume huchukia sana jike akizaa dume, hasira yake huja pindi anapoyafikiria madaraka, kwani hutambua jamaa hao ndio watakao kuja kumpindua ili wao ndio wawe watawala, hivyo chuki yake hukuwa kila watoto hao wanapozidi kuongezeka kimo. Jukumu kubwa la kuyalinda madume hayo huwa chini ya mama yao, siku akizembea tu simba dume huvinyonga kikatili, mtifuano huo huwa hauishii kwa watoto tu. Hata simba dume linapozeeka na kushindwa kutimiza majukumu yake kwa ustadi hufukuzwa kabisa na wanafamilia wenza na nafasi yake itachukuliwa na simba dume ambaye anachipukia kwa wakati huo.
Kwa jina la kisayansi simba huitwa Pantela Leo, kuna msemo usemao akikosa nyama basi hula majani, msemo huu si sahihi inapotokea simba anakula majani si sababu ya njaa, bali hutumia baadhi ya mimea hasa majani, kama tiba pindi anaposumbuliwa na ugonjwa hususani tumbo.
Pamoja na kutumia tiba hiyo, lakini pia wana tabia ya kunyanyapaa simba mwenzao hasa anapopata ugonjwa ambao huonekana ni hatarishi katika jamii yao, badala ya msaada wenzie huamua kumtenga na kumfukuza ili kuepuka ugonjwa huo kusambaa zaidi.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2sPKSsD
via IFTTT


Gwajima Ajipanga Kununua Treni ya umeme

Gwajima Ajipanga Kununua Treni ya umeme

Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amesema amedhamiria kununu treni ya umeme baada ya Rais John Magufuli kuonyesha dhamira ya kujenga reli ya kisasa(standard gauge).
Gwajima ameyasema hayo leo katika ibada ya Jumapili huku akimsifu Rais Magufuli kwa kuchukua hatua hiyo.
Alisema licha yeye ni mchungaji wa Taifa na anaamini ipo siku Dar es Salaam yote itakwenda kanisani kwake kusali.

from Blogger http://ift.tt/2q5WmWQ
via IFTTT


WANANCHO WAOMBA KITUO CHA MABASI KUKARABATIWA

WANANCHI mjini Njombe wameiomba serikali kuboresha kituo cha mabasi cha Njombe Mjini wakati ikiendelea na ujenzi wa Kituo kipya cha mabasi ambacho Ujenzi wake bado unaendelea mkoani humo.
Kituo kinacho tumika kwa sasa kinajaa tope pindi mvua inaponyesha katika maeneo hayo na kusababisha kelo kwa wasafiri na wahudumu wa mabasi yanayoingia na kutoka katika mji wa Njombe kutoka maeneo mbalimbali ndani na nje ya mkoa huo.
Wananchi hawa wanazungumza na starTv Mjini Njombe ambapo wanaomba halmshauri ya mji wa Njombe kuikarabati Stendi hii ya Mji wa Njombe ili kuwasaidia wanapo safiri wakikumbwe na kero ya Tope.
Hata hivyo baadhi ya madereva wanasema kuwa nauli zinaweza kupanda kutokana na ubovu huo kwa kuwa uharaibifu wa vyombo unakuwa mkubwa.
Kuhusu kukarabati stendi ya Njombe mjini ya sasa Mwenyekiti anasema kuwa haita karabatiwa kwa sababu kuna stendi mpya inajengwa huku zile barabara za vijijini kuwa imara.
Amesema kuwa stendi hiyo inapitia katika hatua mbalimbali na kuwa sasa inaingia katika hatua ya kujenga sakafu na wamechukua ushauri wa waziri mkuu walio washauri alipokuwa mkoani humo miezi kadhaa iliyo pita.
Waziri mkuu akiwa mkoani Njombe alimtaka mkandarasi huyo kujenga stendi hiyo katika eneo la Sakafu kwa kiwango imara.
TAZAMA VIDEO HAPA CHINI STENDI YA NJOMBE ILIVYO CHAFUKA KUKINYESHA………………

from Blogger http://ift.tt/2p95rl1
via IFTTT


Afande Sele Amfananisha Bashite na Tumbili Aliyemaliza Kurukia Miti yote na Sasa Ameamua Kumrikia Anayemfuga…

Msanii mkongwe wa Muziki wa Bongo fleva Mwana Hip Hop Afande Sele TheKing ametoa ya moyoni baada ya Kuibuka Tetesi za Uvamizi wa Clouds Media.Kupitia Ukurasa wake wa Facebook Msanii huyo ambaye ndie mfalme wa kwanza wa Miondoko ya Kufokafoka nchini ameandika ya fuatayo:-
“Kama ni kweli Bashite ameongoza watu kufanya uvamizi kwenye kituo cha clouds media kwa jinsi inavyojieleza…Basi atakua mfano wa tumbili aliyemaliza kurukia miti yote sasa ameamua kurukia mwili wa anaemfuga…Na’Anko’akiendelea kushupaza shingo ktk hili huenda yale maandiko yakatimia kabla ya muda tarajiwa…muwe na Jpili Kareem akina ndugu…..” – Afande sele aliandika kupitia akaunti yake ya Facebook

from Blogger http://ift.tt/2nJ5Zui
via IFTTT


Magufuli Aukacha Mkutano wa SADC,Amtuma Samia Suluhu Kumuwakilisha…!!!

Magufuli Aukacha Mkutano wa SADC,Amtuma Samia Suluhu Kumuwakilisha…!!!

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewasili mjini Mbabane – Swaziland jana16-Mar-2017 kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC). 
Mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Kimataifa wa Mfalme Mswati III mjini Mbabane – Swaziland, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amepokelewa na Viongozi mbalimbali ambao wameongozwa na Waziri wa Utumishi wa Umma wa Serikali ya Swaziland Owen Nxumalo.
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan baada ya kuwasili uwanjani hapo amekagua gwaride la heshima lililoandaliwa kwa ajili yake na kushuhudia vikundi mbalimbali vya burudani uwanjani hapo.
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan atamuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Dakta JOHN POMBE MAGUFULI ambaye pia ni Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama inayojulikana kama SADC DOUBLE TROIKA kwenye mkutano huo.
Leo tarehe 17-Marchi-2017,Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan atahudhuria mkutano wa Wakuu na Serikali wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama unaojulikana kama SADC Double Troika ambao utajadili kwa kina hali ya ulinzi na usalama katika nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC)na Falme ya Lesotho.
Mkutano huo wa SADC Double Troika utafanyika kwa kuzingatia mapendekezo ya mkutano wa Mawaziri wa Kamati Ndogo ya Siasa na Diplomasia uliofanyika Dar es Salaam tarehe 24 februari 2017 ambapo mawaziri hao walionyesha ipo haja ya kuitisha mkutano huo ili kujadili kwa kina hali ya ulinzi na usalama kwenye hizo.
Mkutano wa SADC Double Troika utahusisha nchi Sita wanachama wa asasi hiyo ambazo ni Tanzania,Swaziland,Afrika Kusini,Angola,Botswana na Msumbiji.
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan katika msafara wake amefuatana na Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Kikanda na Kimataifa Dakta Augustine Mahiga,Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage na Waziri wa Biashara,Viwanda na Masoko wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Balozi Amina Salum Ali.

from Blogger http://ift.tt/2mBlTpp
via IFTTT


Kategori

Kategori