Showing posts with label 2017 at 10:50AM. Show all posts
Showing posts with label 2017 at 10:50AM. Show all posts
Gazeti la Mawio Waijibu Serikali Baada ya Kutangaza Kulifungia Kwa Miezi 24

Gazeti la Mawio Waijibu Serikali Baada ya Kutangaza Kulifungia Kwa Miezi 24

Uongozi wa gazeti la MAWIO umeapa kwenda mahakamani kupinga uamuzi wa serikali kulifungia gazeti hilo kutochapishwa kwa kipindi cha miezi 24.
Uamuzi wa kulifungia gazeti hilo ulitangazwa na serikali kupiti Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambapo sababu iliyotajwa ni gazeti hilo kukiuka maagizo ya serikali ya kutowahusisha marais wastaafu Mzee Mkapa na Dkt Kikwete katika ripoti za uchunguzi wa mchanga wa madini.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Victoria Media Services Ltd ambaye pia ni Mhariri Mtendaji wa gazeti la MAWIO, Simon Martha Mkina, aliliambia The Citizen kuwa, amuzi huo si wa haki na utapingwa mahakamani.
“Bodi itakutakana kujadili uamuzi huo kama jambo la dharura, lakini tunachoweza kukwambia kwa sasa, tutakwenda mahakamani,” alisema Mkina.
Kwa mujibu wa taarifa ya Waziri Dkt Mwakyembe iliyotolewa na Idara ya Habari (MAELEZO), Waziri alinukuliwa akisema, “Sina budi kulifungia gazeti lako, na kukutaka usitishe kuchapisha nakala ngumu au ya mtandaoni katika kipindi cha muda wa miezi ishirini na nne (24) tangu tarehe ya barua hii, kwa mamlaka niliyopewa chini ya Sheria ya Huduma za Habari Na. 12 ya mwaka 2016 kifungu cha 59.”
Gazeti hilo liliandika habari iliyokuwa na ujumbe wa jumla kuwa, marais hao wamelisababishia taifa hasara kubwa sana kutokana na usafirishaji wa mchanga nje ya nchi kwa kipindi cha miaka 19.
Kwa mujibu wa mamlaka iliyonayo kupitia Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976 sura ya 229 kifungu cha 25(1), Januari 15, 2016 Serikali ilitangaza kulifungia kwa muda wote gazeti la MAWIO lakini baada ya mwaka mmoja wa kukaa kifungoni lilirejea mtaani baada ya kushinda rufaa mahakamani.
 ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2swe4r5
via IFTTT


MEYA wa Rusha Calist na Mkuu wa Mkoa Gambo Mtafutano Waendelea

MEYA wa Rusha Calist na Mkuu wa Mkoa Gambo Mtafutano Waendelea

Meya wa Jiji la Arusha, Calist Lazaro, amempa siku saba Mkuu wa Mkoa Arusha, Mrisho Gambo kumwomba radhi yeye na viongozi wa dini aliowaweka ndani wakati wakijiandaa kupokea rambirambi ya wafiwa wa wanafunzi wa shule ya Lucky Vincent.
Akizungumza leo na waandishi wa habari Arusha, Meya Calist amesema kitendo cha kuwakamata wakiwa wamekusanyika shuleni hapo Mei 18, mwaka huu, kilikuwa ni ukiukwaji wa sheria na kwamba kabla ya kuwakamata alitakiwa awe na amri ya mahakama inayofafanua ukamataji wao, lakini haikuwa hivyo jambo ambalo anadai kuwa ni matumizi mabaya ya madaraka
Hata hivyo Mh. Calist amesema kuwa Mh. Gambo asipofanya hivyo baada ya siku hizo atampeleka mahakamani kwa kuwadhalilisha na kuwaweka ndani bila kosa lolote kwa kuwa hadi sasa hawajaambiwa kosa lao lilikuwa lipi.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2rWjSHW
via IFTTT


Zitto: Nitaungana na Vyama vya Upinzani Kumsimamisha Mgombea Mmoja wa Urais 2020

Kiongozi mkuu wa chama cha ACT wazalendokatika mahojiano maalum amesema mwaka 2020 kuwa hajapiga hesabu zakugombea urais amesema atakaa na vyama vya upinzani na kumsimamisha mgombea mmoja, mgombea huyo anaweza akatoka chama chochote kati ya Chadema, CUF,NCCR Mageuzi au ACT.
Alipoulizwa kama anaukubali UKAWA kama muungano thabiti amesema wataunda umoja mwingine kwa sababu ule ulikuwa ni kwa ajili ya mambo ya katiba.
My Take: Zitto naona amefanya busara, upinzani inabidi wafikirie namna yakuungana upya, maana kumekuwa na vijana wake wa ACT wazalendo wanapiga siasa za maji taka kwa upinzani wenzao hadi unashangaa kama lengolao ni nini
Video:

from Blogger http://ift.tt/2oQ39Eg
via IFTTT


Magufuli Nomaaa..Awakilishwa Kwenye Kikao Kingine cha Kimataifa Nnje ya Nchi….!!!

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amekutana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wakati akiwa uwanja wa ndege wa Julius Nyerere akielekea Port Louis, Mauritius.
Waziri Mkuu, anakwenda Mauritius kumwakilisha Rais John Magufuli, katika uzinduzi wa Jukwaa la Uchumi la Afrika(The inaugural session of The African Economic Platform).
Mauritius inakuwa mwenyeji wa mkutano huo utakaofanyika kuanzia Machi 20 hadi 22 katika hoteli ya Turtle Bay, jijini Balaclava.
Waziri Mkuu wa Mauritius, Pravid Jugnauth atafungua mkutano huo ambao pia utahudhuriwa na viongozi wakuu wa kisiasa wa Afrika, wafanyabiashara, vyuo vikuu, sekta binafsi na wasomi.

from Blogger http://ift.tt/2nRpS1g
via IFTTT


Kategori

Kategori