Showing posts with label 2017 at 10:08AM. Show all posts
Showing posts with label 2017 at 10:08AM. Show all posts
AUDIO: GIGY MONEY AWEKA WAZI SIRI YA KUCHEPUKA NA DIAMOND PLATNUMZ

AUDIO: GIGY MONEY AWEKA WAZI SIRI YA KUCHEPUKA NA DIAMOND PLATNUMZ

Muuza sura kwenye video za wasanii mbalimbali hapa nchini, Gigy Money ametoboa siri kwamba anamtamani mwanamuziki Diamond Platnumz nz kwamba kama yupo tayari atamchukua mateka.
Gigy Money alifunguka hayo alipokuwa akihojiwa na Soud Brown wa Clouds Fm kupitia kipindi cha XXL ambapo alisema haijalishi kama Diamond yupo kwenye uhusiano, ila akimkubali atamuweka mateka.
Zaidi alisema kuwa ana siri kubwa kuhusu yeye na Diamond na kwamba hawezi kuisema kwa sasa kwa sababu akishaisema haitakuwa siri tena. Msikilize hapa chini;
http://ift.tt/2vHH3Gy

from Blogger http://ift.tt/2gP7RSS
via IFTTT


Zitto Kabwe Amlilia Kiongozi wa Freemason..Afichua Siri Nzito Kati ya Kiongozi Huyo na Mwal Nyerere…!!!!

Zitto Kabwe Amlilia Kiongozi wa Freemason..Afichua Siri Nzito Kati ya Kiongozi Huyo na Mwal Nyerere…!!!!

MBUNGE wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT), ameeleza namna Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, alivyokosolewa na Sir Andy Chande baada ya kumnyang’anya kiwanda.
Zitto ambaye pia ni Kiongozi Mkuu wa ACT Wazalendo, alikumbusha hayo jana katika salamu zake za rambirambi kwa Sir Chande aliyefariki dunia juzi jijini Nairobi Kenya, alikokuwa akitibiwa.
Kwa mujibu wa taarifa yake aliyotoa jana, Zitto alisema Chande ambaye amekuwa Kiongozi mwanachama wa Freemason tangu 1954, alikuwa muathirika wa utaifishaji.
Alisema na Chande alikuwa mmiliki wa viwanda vya kusaga unga ambavyo Nyerere alivitaifisha mwaka 1967 na kuunda Shirika la Usagishaji la Taifa (NMC).
“Mzee Chande ni muathirika wa utaifishaji. Yeye alikuwa akimiliki viwanda vya kusaga unga ambavyo Mwalimu Nyerere alivitaifisha na kuunda NMC.
“Siku ya pili baada ya kuitwa na Waziri wa Biashara Prof. Abdurahman Babu na kuambiwa kuwa Dola imechukua kiwanda chake, aliitwa Ikulu na kufanya mazungumzo na Mwalimu,” alifafanua Zitto.
Alisema Nyerere aliomba radhi kwa uamuzi waliochukua na kueleza kuwa ni muhimu kwa nchi kwakuwa biashara hiyo ya kununua mazao ya kusaga unga, ilikuwa na uhitaji kwa wananchi na kwa mujibu wa Azimio la Arusha ilikuwa lazima kitaifishwe.
Zitto alieleza kuwa baada ya Mwalimu Nyerere kutamka maneno hayo, Chande alimjibu kuwa amefanya makosa makubwa kwa kuwa utaifishaji haukuwa jibu sahihi la matatizo ya kiuchumi ya Tanzania na kwamba historia itawahukumu kwakuwa haikujulikana nani alikuwa sahihi.
Baada ya hapo kwa mujibu wa Zitto, Rais Nyerere alimjibu kuwa asijali kuhusu historia na kumhoji kama anataka kazi serikalini au ubalozini atampa.
Zitto aliendelea kueleza kuwa Chande alimjibu kuwa hataki kazi, bali anataka kuendelea kuendesha kampuni hiyo kwa muda wote atakaoruhusiwa na Nyerere, jambo lililomfanya amjibu kuwa aendelee.
Alifafanua kuwa Mzee Chande aliendelea kuwa Mtendaji Mkuu wa NMC iliyotaifishwa na kuendelea kufanya kazi nyingi nyengine za mashirika ya umma.
Mashirika mengine aliyofanya kazi ni pamoja na kuwa Mwenyekiti wa Bodi wa Shirika la Ndege, Shirika la Reli, Shirika la Magazeti ya Serikali, Bodi ya Utalii na mengine kadha wa kadha. 
Zitto aliongeza kuwa hadithi hiyo na nyingine nyingi, Chande ameziweka katika kitabu chake ‘Journey from Bukene ‘.
“Mzee Chande ametangulia mbele ya haki, lakini Mzee Chande amebaki nasi kwani ameandika. Ametuachia historia yake na historia yake ni historia ya nchi yetu pia,” alisema Zitto.

from Blogger http://ift.tt/2oVKGsO
via IFTTT


Kategori

Kategori