Showing posts with label 2017 at 05:48PM. Show all posts
Showing posts with label 2017 at 05:48PM. Show all posts
WANAOENDESHA MAUAJI KIBITI WAUAWA NA POLISI
Jeshi la Polisi nchini limefanikiwa kuwaua watu wawili wanaosadikiwa kuwa ni miongoni mwa wahalifu wanaoendesha mauaji katika Kanda maalumu ya kipolisi Rufiji ambapo mmoja kati ya watu hao ametambulika kwa jina la Abdallah Ally Ngande Makeo ambaye alikuwa anatafutwa na Jeshi la Polisi kwa muda mrefu kutokana na kushiriki kwake katika matukio ya mauaji maeneo ya Ikwiriri, Kibiti pamoja na uvamizi wa kituo cha Polisi Ikwiriri.
Akielezea tukio hilo, Mkuu wa Operesheni Maalum za Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi, Liberatus Sabas alisema kuwa tukio hilo lilitokea mnamo tarehe 19, julai, 2017 saa mbili usiku katika eneo la Utende kata ya Ikwiriri, wilaya Rufiji Kanda Maalum ya Polisi Rufiji.
“Askari Polisi wa doria waliwatilia mashaka watu wanaokadiliwa kuwa watano ambapo walianza kuwafutilia ndipo walianza kukimbia huku wakiwashambulia askari kwa risasi, askari nao kwa ujasiri walijibu mashambulizi na kufanikiwa kuwajeruhi wahalifu wawili miongonio mwao ambao baadaye walifariki wakipelekwa Hospitali ya Taifa ya muhimbili kutokana na kuvuja damu iliyosababisishwa na majeraha ya risasi waliyoyapata” alisema Sabas.
Aliongeza kuwa katika eneo hilo la tukio ilipatikana silaha moja aina ya rifle 375 ambayo ilikutwa imekatwa kitako na mtutu ikiwa na risasi mbili (2). Aidha, Miili ya marehemu wote wamehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Kamanda sabas ameendelea kutoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kutoa taarifa zitakazosaidia kukamatwa wahalifu wengine waliosalia na kwamba opereheni hiyo ya kuwasaka wahalifu katika Kanda hiyo ya kipolisi Rufiji ni endelevu na hakuna atakaye baki.
Mkuu wa Operesheni Maalun za Jeshi la Polisi, Naibu kamishina wa Polisi (DCP) Liberatus Sabas akiwa katika eneo la tukio akizungumzia namna Jeshi la Polisi lilivyofanikiwa kuuawa watu wawili awanaosadikiwa kuwa ni miongoni mwa wahalifu wanaojihusisha na mauaji watu katika Ikwiriri na kibiti. (Kushoto kwake ) ni Kamanda wa Kanda maalum ya Kipolisi Rufiji, Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Onesmo Lyanga akiwa ameshika silaha aina ya Rifle 375 iliyokutwa katika eneo la tukio. Picha na Tamimu Adam.
from Blogger http://ift.tt/2vrJ3mU
via IFTTT
Mtuhumiwa Malkia wa Tembo ahoji juu ya Hapa Kazi Tu Mahakamani
Anayedaiwa kuwa Malkia wa Meno ya Tembo Yang Feng Clan (66), amesema kauli mbiu ya Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania ni hapa kazi tu lakini mbona Mahakamani hamna hiyo kazi tu.
Mshtakiwa wa kwanza katika kesi ya uhujumu uchumi, Clan ameuliza hayo mahakamani Leo wakati kesi yake ilipokuja kwa ajili ya kusikilizwa.
Kabla Clan hajasema kitu, Wakili wa Serikali Nassoro Katuga ameileza mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa kesi hiyo Leo imekuja kwa ajili ya kusikilizwa lakini wakili anayeendesha anamajukumu mengine kikazi.
Baada ya kusikia hayo, mshtakiwa Clan alinyoosha mkono ndipo Hakimu Huruma Shahidi anayesikiliza kesi hiyo akamruhusu kusema naye akalamika, ” tumekuja mร hakamani mara nyingi, leo mara ya nne hamna kitu, Rais Magufuli alisema hapa kazi tu, hapa court iko wapi hiyo kazi tu” amesema Mshtakiwa Clan kwa kutumia kiswahili chake chenye lafudhi ya kichina.
Hakimu Shahidi amewataka mawakili wa Serikali kuleta mashahidi na kuwaambia kuwa wanataka kesi zote ziishe kwa wakayi.Katika kesi hiyo Clan anashtakiwa pamoja na mfanyabiashara Salvius Matembo (39) na Manase Philemon (39).
Wanadaiwa kujihisisha na biashara ya meno ya tembo yenye thamani ya bilioni 5.4.
Wanadaiwa kati ya Januari Mosi 2000 na Mei 22, 2014 walijihusisha na biashara ya nyara za Serikali bila kibali.Katika kipindi hicho wanadaiwa kufanya biashara ya vipande 706 vya meno ya tembo vyenye uzito wa kilo 1,889 zenye thamani ya Sh5.4 bilioni bila leseni iliyotolewa na Mkurugenzi wa Wanyamapori.
Kesi hiyo itaendelea kusikilizwa Machine 20 na 30, mwaka huu.
TAZAMA JAMAA HUYU ALIVYOKOSWA KOSWA NA KIFO KWA AJARI MTONI
from Blogger http://ift.tt/2n1Bor3
via IFTTT
Subscribe to:
Posts (Atom)
