Showing posts with label 2017 at 05:47PM. Show all posts
Showing posts with label 2017 at 05:47PM. Show all posts
Mavugo Amsainisha Ndikumana Simba Sc,,Hivi Ndivyo Mchezo Ulivyokuwa..!!

Mavugo Amsainisha Ndikumana Simba Sc,,Hivi Ndivyo Mchezo Ulivyokuwa..!!

SIMBA inahitaji huduma ya beki Mrundi wa Mbao FC, Yusuf Ndikumana, katika msimu ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na sasa imeamua kumpa dili hilo Mrundi mwenzake, Laudit Mavugo ili alikamilishe.
Ndikumana ameonyesha kiwango kizuri akiwa katika kikosi cha Mbao FC ambayo ilipandishwa daraja kucheza msimu huu Ligi Kuu Tanzania Bara, baada ya kutokea upangaji wa matokeo kwa timu za Geita Gold na Polisi ya Tabora.
Beki huyo ambaye yuko katika rada za timu tatu hapa nchini Simba, Yanga na Kagera Sugar ambapo nao wanahitaji huduma ya mchezaji huyo, amedaiwa kuwa ameamua kuzipiga chini timu mbili na kukubali kutua Msimbazi.
Uongozi wa Simba umemtumia straika wao, Mavugo baada ya kubaini ukaribu uliopo kati yake na Mrundi huyo mwenzake na mambo yanaenda vizuri.
Ndikumana kwa sasa ni mchezaji huru mara baada ya kumaliza mkataba wake wa kukitumikia kikosi cha Wauza Mbao mkoani Mwanza.
Taarifa za uhakika kutoka ndani ya klabu ya Simba, zinaeleza kwamba mchakato wa kumpata beki huyo mwenye uwezo wa kucheza kama kiungo ulianzia baada ya kumalizika kwa fainali ya michuano ya Kombe la FA, mjini Dodoma.
Alisema Simba wameridhika na kiwango kilichoonyeshwa na mchezaji huyo, hali iliyopelekea kupendekeza jina lake katika usajili.
“Mchakato unaendelea vizuri, kwa upande wa mchezaji huyo haina shida kwani tayari maelekezo amepewa Mavugo ili msimu ujao awepo katika kikosi cha timu yetu,” alisema.
Alisema mara baada ya jina hilo kufika mezani, viongozi walifuatilia rekodi za mchezaji huyo kwa kujiridhisha ambapo mchakato wake sasa umefika katika hatua nzuri ya makubaliano ya kusaini miaka miwili.
DIMBA lilikuwa shuhuda wakati Ndikumana na Mavugo walipokaa pembeni na kuzungumza mara baada ya kumalizika kwa fainali, lakini pia mmoja wa wachezaji hao aliomba mawasiliano ya simu.
Ndikumana alipoulizwa juu ya hilo, hakutaka kuweka wazi na kusisitiza kwamba kwa sasa hajafanya mazungumzo na timu yoyote na kuhusu Mavugo alidai ni mtu wanayefahamiana kwa muda mrefu.
“Mavugo ni rafiki yangu tulikuwa wote timu ya Taifa ya Burundi, suala la Simba kama wapo tayari kutoa kiwango cha fedha anachotaka, nitajiunga nao,” alisema.

from Blogger http://ift.tt/2rLmnP6
via IFTTT


PICHA:RAIS MAGUFULI AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA BANDARI YA DAR

PICHA:RAIS MAGUFULI AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA BANDARI YA DAR

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 23 Machi, 2017 amefanya ziara ya kushtukiza katika bandari ya Dar es Salaam kwa lengo la kufuatilia utekelezaji wa maelekezo aliyoyatoa kwa nyakati tofauti juu ya kudhibiti udanganyifu wa mizigo inayoingia na kutoka nchini kupitia bandari hiyo ikiwemo usafirishaji wa mchanga wa madini kwenda nje ya nchi.
maguu
Katika ziara hiyo Mhe. Rais Magufuli ameshuhudia makontena 20 ya mchanga wenye madini kutoka kwenye migodi iliyopo kanda ya ziwa ambayo yamezuiliwa kusafirishwa nje ya nchi tangu alipotoa agizo la kupiga marufuku usafirishaji wa mchanga nje ya nchi tarehe 02 Machi, 2017.
Pamoja na kushuhudia makontena hayo, Mhe. Rais Magufuli amemuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP – Ernest Mangu na vyombo vingine vya dola kuhakikisha mchanga wa madini unashikiliwa popote ulipo, mpaka hapo uchunguzi wa kina utakapofanyika kubaini ukweli.
“Nataka niwaambie nchi yetu inachezewa mno, nimekuja kuyaona haya makontena kama yapo, na kweli nimeyaona, sasa utaratibu utakapokamilika nataka Watanzania na dunia nzima ione kilichomo humu ndani kama ni mchanga kweli ama dhahabu” amesema Mhe. Rais Magufuli.
Akiwa bandarini hapo Mhe. Dkt. Magufuli pia ameshuhudia udanganyifu mwingine unaofanywa na wafanyabiashara wanaoagiza mizigo kutoka nje ya nchi baada ya kuoneshwa makontena ambayo nyaraka zinaonesha yamebeba mitumba ya nguo na viatu wakati ndani yake kila kontena moja limebeba magari matatu ya kifahari.
Maafisa wa bandari ya Dar es Salaam na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wamemueleza Mhe. Rais Magufuli kuwa kufuatia maelekezo aliyoyatoa ya kuhakikisha mizigo yote inakaguliwa kwa mitambo ya mionzi (Scanning Machines) wamefanikiwa kubaini udanganyifu mwingi unaofanywa na wafanyabiashara wanaoingiza nchini na kusafirisha nje ya nchi mizigo mbalimbali yakiwemo makontena 10 ambayo yamepatikana yakiwa na magari ya kifahari ilihali nyaraka zake zikionesha yana mitumba ya nguo na viatu.
Mhe. Rais Magufuli amewapongeza maafisa na wafanyakazi wa bandari ya Dar es Salaam na TRA kwa kazi nzuri wanayofanya kudhibiti upotevu wa fedha za umma bandarini hapo na amewataka kuendelea kutekeleza wajibu wao kwa uzalendo na kujiepusha na rushwa.
“Leo mmenifurahisha sana, ninawatia moyo endeleeni kuwakamata wote wanaofanya udanganyifu huu na muwachukulie hatua kali za kisheria, lakini msimuonee mtu na msipokee rushwa, tunataka watu wajifunze kuwa hapa sio shamba la bibi” amesisitiza Rais Magufuli.
Aidha, ametoa wito kwa vyombo vyote vinavyoshughulikia udhibiti wa mizigo inayoingia na kutoka kupitia bandari ya Dar es Salaam na bandari nyingine hapa nchini, kuendelea kushirikiana ili kukomesha vitendo vyote vya udanganyifu ambavyo vinasababisha nchi kupoteza mapato mengi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika ziara ya kushtukiza katika Bandari ya Dar es Salaam kufatilia maagizo yake ya kudhibiti vitendo vya udanganyifu vinavyofanywa na wafanyabiashara wanaogiza na kusafirisha vitu mbalimbali nje ya nchi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akihesabu makontena 20 yenye mchanga wa madini ambapo ameamuru kontena hizo zisisafirishwe mahali popote
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza kuhusu makontena 20 yenye mchanga wa madini uliokuwa usafirishwe kwenda nje ya nchi ambapo ameagiza Kontena hizo zisisafirishwe mahali popote.
Makontena 20 yenye mchanga wa madini yakiwa yamezuiwa kusafirishwa nje ya nchi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli mara alipofanya ziara ya kushtukiza katika bandari ya Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akikagua nyaraka mbalimbali zenye kuhusu makontena ambayo husafirishwa nje ya nchi katika Bandari ya Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia baadhi ya magari yalivyoingizwa nchini kwa njia isiyo halali ya kudai kuwa ni makontena ya mitumba wakati ndani yake wanaficha magari yakifahari pamoja na vitu vilivyochakaa March 23,2017
Moja ya kontena likiwa lina magari matatu ndani yake aina ya Range Rover ambapo muagizaji alidai kuwa anaagiza mitumba lakini kumbe ndani yake wanakuwa wameficha magari ya kifahari.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na IGP Ernest Mangu mara baada ya kufanya ukaguzi Bandarini hapo.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
23 Machi, 2017

from Blogger http://ift.tt/2nb9CJm
via IFTTT


Ufafanuzi kuhusu tetesi za Simba kutaka kumsajili ‘rasta’ wa Madini FC

Kocha mkuu wa Madini FC Abdallah Juma ametoa ufafanuzi wa kina kuhusu tetesi za usajili zilizoibuka kuhusu mchezaji wake Awesu Awesu kuhusishwa na mpango wa kusajiliwa na klabu ya Simba baada ya kuonekana akizungumza na mwenyekiti wa kamati ya Usajili Zacharia Hans Poppe mara baada ya mchezo wa hatua ya robo fainali ya kombe la shirikisho hapo jijini Arusha.
Abdallah Juma amesema kiongozi huyo wa kamati ya usajili ya klabu ya Simba ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya utendaji ya klabu hiyo, ni kweli alifanya mazungumzo na mchezaji wake na wamempa nafasi ya kuwasilisha ofa mezani endapo ana nia ya dhati ya kumsajili.
Hata hivyo kocha huyo amesema mipango mingine ya usajili wa mchezaji huyo kama itatokea ipo katika mamlaka za uongozi wa juu wa klabu ya Madini FC japo anatambua Awesu ana uwezo wa kucheza katika klabu yoyote hapa nchini.
“Najua suala hilo lipo lakini mimi siwezi kulizungumzia rasmi, wamesema wanataka kukutana na mchezaji pamoja na viongozi kwa hiyo hilo suala litakuwa na utawala lakini hata mimi najua.”
“Kupitia radioni wamesema walifanya mazungumzo na mchezaji na kikubwa alikuwa anataka mawasiliano, atazungumza nae na atazungumza na uongozi wakikubaliana basi atakwenda kufanya kazi huko.”
Awesu Awesu alishawahi kuwa Azam FC kipindi cha nyuma akicheza kwenye kikosi cha U20 lakini baadae akajiunga na Madini FC ambako yupo hadi sasa.
KAMA ULIMIS VIDEO YA MCHEZAJI WA Ghana  ALIE JIKANYAGA KWA KUWASHUKURU MUKE NA MCHEPUKO WAKE TAZAMA HAPA

from Blogger http://ift.tt/2n9NEbv
via IFTTT


Kategori

Kategori