Showing posts with label 2017 at 03:16PM. Show all posts
Showing posts with label 2017 at 03:16PM. Show all posts
SERIKALI YATOA SABABU YA KUWAKAMATA WAFANYAKAZI WA ACACIA

SERIKALI YATOA SABABU YA KUWAKAMATA WAFANYAKAZI WA ACACIA

Idara ya Uhamiaji imesema jukumu la Udhibiti wa Uingiaji na Utokaji wa raia wa kigeni nchini, linatekelezwa kwa mujibu wa Sheria ya Uhamiaji Sura ya 54 (Rejeo la 2016) na wala haiwalengi wafanyakazi wa Kampuni ya Madini ya Acacia peke yake.
Ni hitajio la kisheria kwa kila raia wa kigeni anayeingia na kutoka nchini kukaguliwa ili kujiridhisha iwapo hakuna dosari zozote za Uhamiaji, Ulinzi na Usalama.
Sheria ya Uhamiaji inaitaka Idara ya Uhamiaji kumhoji mtu yeyote awe raia wa Tanzania au kigeni bila kujali anafanya kazi kwenye Kampuni au Shirika gani, pale inapotaka kujiridhisha juu ya uhalali wa ukaazi wake hapa nchini na ikijiridhisha kuwa mtu huyu hana dosari zozote inamwachia huru kama ilivyofanyika kwa wafanyakazi wa Kampuni ya Madini ya Acacia waliohojiwa na kuruhusiwa kuendelea na safari yao hivi karibuni.
Idara ya Uhamiaji inapenda kuuarifu Umma kuwa hakuna sababu zozote nje ya matakwa ya Sheria ya Uhamiaji zinazopelekea Idara ya Uhamiaji kuweka kizuizi cha kuja au kutoka kwa wafanyakazi wa kigeni wa Acacia.
Tunapenda kuujulisha Umma kuwa ni muhimu kwa watanzania na raia wa kigeni wanaokusudia kuingia na kutoka nchini kuhakikisha wanafuata Sheria za Uhamiaji ili kutimiza hitajio la kisheria.
Imetolewa na
Ally M. Mtanda
Msemaji wa Idara ya Uhamiaji
29 Julai 2017

from Blogger http://ift.tt/2uK0nVV
via IFTTT


Korea Kaskazini Wazidi Kuwa Kichwa Ngumu….Warusha Makombora Yakutungua Meli za Kivita

Korea Kaskazini Wazidi Kuwa Kichwa Ngumu….Warusha Makombora Yakutungua Meli za Kivita

Pyongyang, Korea Kaskazini. Korea Kaskazini imesema makombora iliyoyafanyia majaribio jana Alhamisi ni mahsusi kwa ajili ya kushambulia ‘kundi la meli za kivita’ ambazo zimekuwa zikiitishia nchi hiyo.
Shirika la Habari la Serikali la KCNA limesema majaribio hayo ya jana ya makombora ya ardhini kwenda baharini ni ya hivi karibuni katika msururu wa vitendo vya ukiukaji wa vikwazo vya Umoja wa Mataifa na yalishuhudiwa na kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong-Un.
Majaribio hayo yamefanyika siku moja baada ya Umoja wa Mataifa kuongeza makali ya vikwazo dhidi ya taifa hilo.
“Makombora hayo yaliyorushwa yaliweza kutambua kwa ufasaha vifaa vilivyolengwa vilivyokuwa vinaelea kwenye bahari ya mashariki mwa Korea,” KCNA wamesema, wakizungumzia Bahari ya Japan, ambako kuna meli mbili kubwa za Marekani za kubeba ndege za kivita.
Korea Kaskazini inawezekana inazilenga meli za USS Carl Vinson na USS Ronald Reagan zilizoongoza mazoezi ya siku tatu ambayo yalimalizika Juni 3 yakihusisha meli zaidi ya 10 za kivita za Marekani pamoja na mbili za Japan. Mazoezi hayo yalionekana kulenga kuitisha Korea Kaskazini.
Marekani imezidisha shughuli zake za kuonyesha ubabe wa kijeshi eneo hilo, ambapo ina nyambizi inayotumia nguvu za nyuklia, USS Cheyenne yenye uzani wa tani 6,900.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2sm03fX
via IFTTT


Kategori

Kategori