Showing posts with label 2017 at 02:24PM. Show all posts
Showing posts with label 2017 at 02:24PM. Show all posts
HAJI MANARA NA WENZAKE WASAMEHEWA ADHABU NA TFF

HAJI MANARA NA WENZAKE WASAMEHEWA ADHABU NA TFF

Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imefuta adhabu dhidi ya wanafamilia wanne waliofungiwa kushiriki masuala la soka kwa mwaka mmoja.
Wanafamilia hao ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Rukwa, James Mwakwinya; Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Rukwa (RUREFA), Blassy Kiondo; Kaimu Katibu wake, Ayoub Nyaulingo pamoja na Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara.
Haji Manara alitiwa hatiani Aprili 23, mwaka huu kwa makosa ya lugha chafu na za chuki kwa viongozi wa TFF na kupotosha umma dhidi ya kadi njano ya mchezaji Mohammed Fakhi wa Kagera Sugar ambako alifungiwa kushiriki masuala ya mpira kwa mwaka mmoja na faini ya Sh milioni tisa.
Viongozi wa RUREFA walifungiwa kwa mwaka mmoja na faini ya Sh. milioni mbili kwa kila mmoja kwa makosa ya kukiuka maagizo ya viongozi wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF iliyotaka wasitishe mchakato wa uchaguzi mkoa kwa kuwa kulikuwa na rufaa iliyokatwa TFF.
Akizungumza na Wanahabari leo Julai 17, 2017 Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu ya TFF, Tarimba Abbas, alisema viongozi hao wamesamehewa adhabu zao kwa kuwa waliomba kupitiwa upya kwa mashauri yao na kamati imeona ni bora kuwaachia huru ili kuendeleza masuala ya soka.
“Wapo wengi waliofungiwa wengine maisha na wengine adhabu fupi, msamaha huu ni kwa wale ambao wameomba tu kupitiwa upya kwa adhabu zao, pia milango ipo wazi kwa wengine ambao wanataka kupitiwa kwa mashauri yao, lakini si kwa wale waliopanga matokeo uwanjani,” alisema Tarimba.
Kadhalika, Tarimba aliwaomba viongozi wa TFF kuandaa semina ya Maofisa Habari na Viongozi wa Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza (FDL) ili kuepuka maneno machafu ambayo yanasababisha wao kufungiwa.
“Inaonekana viongozi na Maofisa Habari hawana maneno mazuri ya kuongea na wadau wa soka na ndio maana matatizo ya kufungiwa yanajitokeza mara kwa mara, naamini wakipata semina hiyo itawasaidia kujirekebisha na kupunguza kesi kama hizo,” alisema Tarimba.
Kwa niaba ya TFF, Ofisa Habari wa Shirikisho, Alfred Lucas, wameyapokea mapendekezo hayo kutoka kwa Tarimba na kwamba tutafanyia kazi ili kurekebisha makosa hayo kwa manufaa ya soka la Tanzania.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA

from Blogger http://ift.tt/2vBuXyB
via IFTTT


Wolper Akana Kuwahi Kubadili Dini na Kuwa Muislamu..Adai Ile Ilikuwa ni Maigizo Tu..!!!

Wolper Akana Kuwahi Kubadili Dini na Kuwa Muislamu..Adai Ile Ilikuwa ni Maigizo Tu..!!!

Muigizaji Jacquline Wolper amekanusha vikali kuhusu suala la kuwahi kubadilisha dini kwa shinikizo la mapenzi na kwamba yote yaliyowahi kuonekana au kusikika huko nyuma ni mambo ya sanaa.
Wolper amefunguka hayo na kudai kwamba yeye kama msanii kuna mambo anaweza kufanya ya kisanii lakini watazamaji wasijue kama ni sanaa lakini ukweli ni kwamba hajawahi kuhama ukristo na kwenda kwenye dini ya kiislamu.
“Sijawahi kubadilisha dini mimi, Sisi wasanii ndiyo tunajua tunafanyaga mimi mpaka watu wanaamini vitu kama kubadilisha dini. Ukweli wa dini yangu naujua mimi peke yangu lakini mengine yanayoonekana ni kazi ya sanaa” -Wolper alifunguka.
Akizungumzia suala la mapenzi Wolper amesema kwamba amekuwa na changamoto mbalimbali sana za kushindwa kudumu kwenye mahusiano kwa kuwa wanawake wenzake hupenda kumuingilia kwenye mahusiano yake kitu ambacho amekiita kipaji cha kukomeshwa.
“Mimi ni kama nina kipaji cha kukomeshwa kwenye mapenzi kwa sababu kipaji ninachokivumbua mimi wenzangu wanataka wapite hapo hapo ili kunikomoa. Ni kwamba nina kipaji cha kukomeshwa lakini huyo anayenikoa unakuta hajui mimi nimepambana vipi kumtengeneza mtu anipende” aliongeza Wolper.

from Blogger http://ift.tt/2qtClJz
via IFTTT


Giggs amtaja mchezaji bora kuwahi kucheza naye

Giggs amtaja mchezaji bora kuwahi kucheza naye

Ryan Giggs pengine ni kati ya wachezaji ambao wamecheza dhidi ya wachezaji wengi sana ulimwenguni, michezo zaidi ya 960 ndani ya misimu 24 inaonesha dhahiri jinsi Giggs alivyo nguli.
Amewahi kucheza na wachezaji wanaotajwa kuwa ni kati ya wachezaji bora sana kuwahi kutokea ulimwenguni, akiwemo Wayne Rooney, Ruud Van Niestroy, Roy Keane na hata Andy Cole.
Lakini kati ya hao wote Giggs ana mchezaji mmoja tu ambaye kwake anamuona kama alikuwa bora zaidi, Giggs anaona wote aliocheza nao ni bora na ndio maana walumsaidia kushinda vikombe vingi lakini yupo aliyewazidi wote.
“Mchezaji bora niliyecheza naye ni ngumu kumtaja kwakweli, lakini nadhani Cristiano Ronaldo ni bora sana” alisema Giggs wakati akihojiwa.
Cristiano ambaye kwa sasa ndio mchezaji mwenye tuzo ya mchezaji bora wa dunia kwa miaka 6 aliyoiyumikia Manchester United aliweza kubeba kombe la FA, kombe la Champions League, kombe la EPL na alifanikiwa kuchukua tuzo karibia zote ikiwemo Ballon d’or akiwa Uingereza.
Baada ya kuhamia Real Madrid kwa uhamisho uliovunja rekodi ya usajili kwa wakati huo wa £80m Ronaldo bado ameendelea kuweka rekodi na kuzidi kubeba makombe na hii inawafanya watu wengi duniani akiwemo Giggs kuamini Ronaldo ni bora.

from Blogger http://ift.tt/2npPC9x
via IFTTT


Kategori

Kategori