Showing posts with label 2017 at 02:13PM. Show all posts
Showing posts with label 2017 at 02:13PM. Show all posts
Hatareee..Korea Kaskazini Waonyesha Makombora Watakayoyatumia Kuipiga Marekani..Wamwambia Trump Alianzishe Wamwonyeshe Jinsi Vita Vinavyopigana..!!!

Hatareee..Korea Kaskazini Waonyesha Makombora Watakayoyatumia Kuipiga Marekani..Wamwambia Trump Alianzishe Wamwonyeshe Jinsi Vita Vinavyopigana..!!!

Katika kile kinachoonekana kuwa Kiongozi wa Korea Kaskazini, KIM JONG UN, haogopi chochote na yuko tayari kukabiliana na uvamizi wa Marekani, kiongozi huyo leo tarehe 15.04.2017 ameonesha makombora mapya katika Gwaride Maalum la Kumbukumbu ya 105 ya kuzaliwa kwa mwasisi wa taifa hilo la kikomunisti, KIM IL SUNG, ambaye pia ni babu yake.
Makombora yaliyooneshwa kwa mara ya kwanza leo ni yale ya kurushwa kutoka kwenye nyambizi, yaani submarine-launched ballistic missiles, na makombora ya masafa marefu (ICBM).
Makombora ya kurushwa kutoka kwenye nyambizi, aina ya Pukkuksong-2 submarine-launched ballistic missiles (SLBMs), yalipitishwa mbele ya Kim Jong Un katika malori maalum kwa mara ya kwanza huku kiongozi huyo, akiwa amevalia suti nyeusi, shati jeupe na tai, akiyapungia. 
Afisa mmoja wa ngazi za juu wa serikali ya Kim Jong Un anayeitwa CHOE RYONG HAE, akiwahutubia askari katika gwaride hilo, amemlaumu Rais DONALD TRUMP wa Marekani kwa kuanzisha hali ya vita katika rasi ya Korea na kuahidi kuwa watajibu ubabe wa Marekani kwa vita kamili. Afisa huyo alisema: “Tutajibu vita kamili kwa vita kamili na vita vya nyuklia kwa shambulizi la nyuklia kwa mtindo wetu”, amenukuliwa na shirika la habari la AP

from Blogger http://ift.tt/2pilM6J
via IFTTT


Jux Apata Kigugumizi Kuzungumzia Kinachoendelea Kati Yake na Vanessa..!!!

Jux Apata Kigugumizi Kuzungumzia Kinachoendelea Kati Yake na Vanessa..!!!

Baada ya tetesi kuzagaa katika mitandao ya kijamii kuwa Jux ameachana na mpenzi wake Vanessa 
Mdee, Jux ameshindwa kufunguka hukusu sakata hilo.
Muimbaji huyo amedai yupo kwenye mahusiano huku akishindwa kueleza anaendelea kutoka na Vanessa au amepata mrembo mwingine.
Akiongea katika kipindi cha FNL cha EATV, Jux amedai yeye naendelea na shughuli zake za muziki na Vanessa yupo nje ya nchi kwaajili ya shughuli zake za muziki.
“Kwanza nataka kukusahihisha kuwa mimi sio single boy, niko na mtu,” alisema JUX. “kuhusu Vanessa kama nipo naye that my business,
Katika hatua nyingine muimbaji huyo amewataka mashabiki wa muziki wake kukaa mkao wa kula kwaajili ya wimbo wake mpya.

from Blogger http://ift.tt/2pm7uPF
via IFTTT


Prezzo Amnyoosha Shabiki Aliyemdhihaki Kuwa Anaringishia Gari la Mama yake

Prezzo Amnyoosha Shabiki Aliyemdhihaki Kuwa Anaringishia Gari la Mama yake

Rapper controversial wa hapa nchini Kenya, amezua msisimuko wa hisia kwa wapenzi wa mtandao wa Instagram baada ya kumjibu vibaya shabiki aliyeandika jibu la kumkejeli kwenye post yake ya Instagram.
Prezzo ni rapper ambaye wengi wanamuogopa kwa vituko vyake ambavyo haviishi, si nyuma ya pazia la camera bali hadi akiwa live on air kwenye runinga inayotazamwa na mamilioni ya mashabiki.
Katika muktadha huu, rapper huyo na staa wa reality TV show ya Nairobi Diaries alionekana kukerwa na jibu la Kelvin Masakhwi ambaye alimchana Prezzo kwa kuonyesha gari ambalo Prezzo anadai kuwa yake ya kwanza aliyonunuliwa na mamake mzazi alipokuwa chuo kikuu. Nikinukuu maandishi hayo, Prezzo amesema, “Old money fam, my 1st ride in uni had my lecturers looking at me in some type of way…. & u wonder why I love my mum to death. Gods son #Rapcellency.”
Tazama majibizano ya Prezzo na shabiki huyo kwenye picha hii hapa.
Makala ya: Changez Ndzai (Kenya)
Facebook: Changez Ndzai
Twitter : ChangezN
Instagram:changez_ndzai

from Blogger http://ift.tt/2o0QIFL
via IFTTT


Yanga wa Kimataifa Wafanya Kweli na Kuiondoa Simba Kileleni

Yanga wa Kimataifa Wafanya Kweli na Kuiondoa Simba Kileleni

YANGA SC imerejea kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Azam FC jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Sifa nyingi kwa mfungaji wa bao hilo, Mzambia Obrey Chirwa dakika ya 70 baada ya kumtoka beki wa Azam FC, Mghana Yakubu Mohamed kufuatia pasi ndefu ya kiungo Mnyarwanda, Haruna Niyonzima.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa wa kike mwenye beji ya FIFA, Deonesya Rukyaa wa Kagera, Yanga ilipata pigo dakika ya 30 baada ya kiungo wake Mzambia, Justin Zulu kuumia mguu wa kushoto na kushindwa kuendelea na mchezo nafasi yake kuchukuliwa na winga, Emmanuel Martin.
Zulu aliwekewa mguu na kiungo wa Azam FC, Himid Mao wakati anapiga shuti kuunga mpira uliorudi baada ya kuokolewa kufuatia krosi ya kiungo Haruna Niyonzima kutoka Rwanda.
Martin alikwenda kucheza wingi ya kulia na Niyonzima akahamia katikati kuchukua nafasi ya Zulu aliyekuwa akicheza kama kiungo mchezeshaji.
Mabadiliko hayo ambayo hayakuwa mipango ya mwalimu, yaligeuka msaada mkubwa kwa timu hiyo, kwani Niyozima alikwenda kucheza vizuri sehemu ya katikati ya Uwanja na Yanga ikaanza kushambulia.
Azam nao wakapata pigo dakika ya 43 baada ya mshambuliaji wake, Yahya Mohammed kuumia msuli baada ya kupiga shuti na kushindwa kuendelea nafasi yake ikichukuliwa na Mghana mwenzake, Samuel Afful.
Kipindi cha pili, timu zote zilirudi vizuri na zikaendelea kushambuliana kwa zamu, ingawa baada ya Yanga kupata bao dakika ya 70, wakaanza kucheza kwa kupoteza muda.
Ushindi huo unaifanya Yanga sasa ifikishe pointi 56 baada ya kucheza mechi 25 na kurejea kileleni mwa Ligi Kuu ikiwaangushia nafasi ya pili mahasimu wao, Simba SC ambao kesho watacheza mechi ya 25 pia dhidi ya Kagera Sugar mjini Bukoba.
Kikosi cha Yanga kilikuwa; Deo Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Mwinyi Mngwali, Vincent Bossou, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Said Juma ‘Makapu’, Simon Msuva/Juma Mahadhi dk90+2, Justin Zulu/Emmanuel Martin dk30, Obrey Chirwa, Deus Kaseke/Geoffrey Mwashiuya dk54 na Haruna Niyonzima.
Azam; Aishi Manula, Erasto Nyoni, Gardiel Michael, Daniel Amoah, Yakubu Mohammed, Himid Mao, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Frank Domayo, Yahya Mohmmed/Samuel Afful dk44, Shaaban Iddi/Bruce Kangwa dk75 na Ramadhani Singano ‘Messi’/Joseph Mahundi dk69.

from Blogger http://ift.tt/2nZelQP
via IFTTT


Kategori

Kategori