Showing posts with label 2017 at 02:08PM. Show all posts
Showing posts with label 2017 at 02:08PM. Show all posts
Noma Sana..Pamoja na Wakenya Kwenda Mahakamni..Madaktari 470 wa Kitanzania Wajitokeza Kuchangamkia Fursa ..!!

Noma Sana..Pamoja na Wakenya Kwenda Mahakamni..Madaktari 470 wa Kitanzania Wajitokeza Kuchangamkia Fursa ..!!

Wakati Mahakama nchini Kenya imezuia kwa muda madaktari kutoka nje kwenda nchini humo kupiga kazi, zaidi 470 wameomba kazi hizo kupitia Wizara ya Afya hapa nchini.
Serikali ya Tanzania imesema mchakato wa kupokea maombi hayo pia utaendelea kwa kuwa haijapokea maelekezo yoyote nchini Kenya.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema bado wanasubiri taarifa rasmi kutoka kwa Serikali ya nchi hiyo.
“Tunasubiri taarifa rasmi kutoka Serikali ya Kenya kwa kuwa wao ndiyo walioleta maombi kwetu. Kama kuna mabadiliko yoyote, naamini watatufahamisha rasmi,” amesema.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dk Mpoki Ulisubisya madaktari 470 wametuma maombi kati ya nafasi 500 zilizotangazwa za kwenda kufanya kazi nchini humo.
Msemaji wa wizara hiyo, Nsanchiris Mwamaja amesema: “Tumepokea maombi mengi ya kutosha, lakini ikitokea mtu akatuma tunayapokea, hivi karibuni jopo litakaa na kuanza kupitia maombi hayo kabla ya usaili na baadaye kupanga mipango ya namna gani watafika vituo vyao vya kazi.”

from Blogger http://ift.tt/2nw5CCz
via IFTTT


Mwalimu Jela miaka 4 kwa kumkashifu mwanafunzi wake

Mahakama ya Wilaya mwanakwerekwe imempeleka chuo cha mafunzo miaka 4 khamis Zahir mwalim (24) mkaazi wa Mfenesi maziziz Wilaya ya Mjini kwa kosa la kumkashifu mwanafunzi wake.
Imeadaiwa Mahakamni hapo na muendesha mashtaka wa Serikali Saidi Ali na Huda Othaman mbele ya hakimu Chausiku Kafuti Mkuya kwamba siku ya tarehe 17 disemba 2015 majira ya saa 3 asubuhi huko gulioni mshtakiwa ambe ni mwalimu wa Almadrasat Nnabiy iliyoko Gulioni alimshika na kunyonya matiti mwanafunzi wake wa kike mwenye umri wa miaka 13 jambo ambalo ni kosa kisheria
Awali aliposomewa kosa lake mshtakiwa alikataa nakupandishwa kizimbani kwa nyakati tofauti na Jana kusomewa hukumu yake.
Mshtakiwa amepelekwa chuo cha mafunzo miaka 4 ili akajifunze tabia njema na iwe funzo kwake na wengine wenye tabia kama hiyo.
Tazama video Mtoto amvua kofia
 Papa Francis

from Blogger http://ift.tt/2nmr3Fr
via IFTTT


Lipumba: Inakuaje Syria Wanapigana Vita Lakini Wanatuzidi kwa Furaha..!!!?

Profesa Lipumba ameshangazwa na ripoti iliyotolewa na umoja wa mataifa ikitaja Tanzania kuwa nchi ya 3 kutoka mwisho kwa furaha huku ikipitwa na nchi kama Burundi na Syria
Amesema hii ianaonyesha tupo katika hali mbaya sana ya maisha hadi tunapitwa na nchi zenye vita
TAZAMA HARMORAPA ALIVYO TIMUA MBIO BAADA YA KUIONA BASTOLA

from Blogger http://ift.tt/2np80O8
via IFTTT


Kategori

Kategori