Showing posts with label 2017 at 01:59PM. Show all posts
Showing posts with label 2017 at 01:59PM. Show all posts
Mohamed Thabalala wa Simba Anyakua Tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligu Kuu Msimu wa 2016/17..!!!

Mohamed Thabalala wa Simba Anyakua Tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligu Kuu Msimu wa 2016/17..!!!

Beki wa kushoto wa kutumainiwa wa klabu ya Simba, Mohamed Hussein Hussein ‘Tshabalala’ a.k.a Zimbwe Jr. amefanikiwa kutwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu uliomalizika wa 2016/17.
Zimbwe amewashinda Aishi MANULA (Azam) na Saimon MSUVA (Yanga na ameondoka na kitita cha shilingi milioni 10.
Beki huyo ambaye amecheza michezo yote ya Simba ya ligi kuu msimu huu kwa dakika zote 90 kwa kila mchezo ametangazwa rasmi katika sherehe zilizofanyika usiku wa jana Mei 24, 2017 katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.
Mbali na tuzo hiyo ambayo ndiyo kubwa, tuzo nyingine zilizotolewa ni kama ifuatavyo… 
Tuzo ya Goli Bora la Msimu inakwenda kwa Shiza Kichuya, bao alilofunga Feb. 25 katika mchezo wa marudiano dhidi ya Yanga. Kichuya, amewashinda Peter Mwarianzi na Zahoro Pazi
Tuzo ya Heshima inakwenda kwa Kitwana Manara mchezaji wa zamani wa Yanga na Taifa Stars aliyewika miaka ya 1960 hadi 1970
Tuzo ya Ismail Khalfan (U-20) inakwenda kwa Shaaban IDD (Azam) akiwashinda Abdalah MASOUD (Azam) na Mosses KITAMBI (Simba)
Mchezaji Bora Chipukizi ni Mbaraka Yusuph (Kagera Sugar), akiwashinda Shaaban IDD (Azam) Mohammed ISSA (Mtibwa)
Mchezaji Bora wa Kigeni ni Haruna NIYONZIMA (Yanga), akiwashinda Method MWANJALE (Simba) na Yusuph NDIKUMANA (Mbao FC)
Tuzo ya Kipa Bora imekwenda kwa Aishi MANULA (Azam) akiwashinda Owen CHAIMA (Mbeya City) na Juma KASEJA (Kagera Sugar)
Tuzo ya Kocha Bora imekwenda kwa Mecky MEXIME (Kagera Sugar) akiwashinda Joseph OMOG (Simba) na Ettiene NDAYIRAGIJE (Mbao FC)
Tuzo ya mwamuzi bora imekwenda kwa Elly SASII (DSM) miaka 29, amewashinda Shomari LAWI (Kigoma) na Hance MABENA
Tuzo ya mfungaji bora imekwenda kwa Saimon Msuva (Yanga) na Abdulrahman Mussa (Ruvu Shooting), zawadi yao ni Tsh. mil 5.8
KIKOSI BORA (4:4:2): Manula (Azam), Kimenya (Prisons), Tshabalala (Simba), Yakub (Azam), Mwanjale (Simba), Kenny Ally (Mbeya City), Msuva (Yanga), Niyonzima (Yanga), Abdulrahman Mussa (Ruvu Shooting), Mbaraka (Kagera Sugar), Kichuya (Simba)

from Blogger http://ift.tt/2qn3Kgd
via IFTTT


Mkanganyiko Baada ya Roho Kuachana na Mwili,Roho Huenda Wapi

Mkanganyiko Baada ya Roho Kuachana na Mwili,Roho Huenda Wapi

Haya mambo bado yanachanganya wengi kwamba roho inaenda wapi baada ya kuachana na mwili
1.Je inaenda kuzimu?
2.Je inaenda peponi? 
3.Je inazaliwa upya?
4.Je inawayawaya na kutangatanga huku na kule?
Maswali yote hapo juu yana majibu yanayofanana, kuwa roho zipo na zinakuwa kote huko kulikotajwa kutegemeana na kwenye uhai wake kidunia zilibeba/ zilifanya nini? Hebu twende moja baada ya jingine.
Kwanza, dini zote zinahimiza matendo mema na maisha baada ya kifo; hata wapagani pia. Hivyo basi, japokuwa maelezo yanatofautiana, lakini msingi unabaki kuwa ule ule wa roho kuwa sehemu husika.
1.Je, roho inaenda kuzimu? Jibu ni ndio
Kwamba bila kujali unaamini nini lakini jehanam iko hapahapa duniani , roho iliyotenda mabaya duniani baada ya kutoka katika mwili uharibikao huingia kwenye mwili mwingine uliojaa mateso tabu na mahangaiko mengi! Kumbuka ili roho iweze kubeba hisia za mateso na maumivu lazima zipate jumba/ mwili!! Hiyo ni jehanam au kuzimu.
2.Je, roho huenda peponi? Jibu ni ndio
Pepo iko hapahapa duniani, roho iliyoishi kwa kutenda mema hubaki mahali kwenye dunia hii ikiwa iko live lakini domant ikiwa haihisi wala kufanya chochote na kama ikibidi kupata mwili huingia kwenye mwili ambao haujui shida za dunia hii kila kitu kwake ni mteremko tu mpaka mwili husika unapochoka na kuharibika/ kufa!! Hii ni peponi.
3.Je, roho inazaliwa upya? Jibu ni ndio japo kimsingi sio kuzaliwa upya bali ni kupata makao/ makazi mapya hapa ndio penye dhana nzima ya reincarnation, ambapo sasa hutegemea matendo ya nyuma Kwahiyo yaweza kuwa kwenye mwili mzuri au mbaya refer pepo na kuzimu.
4.Je, roho zinatangatanga? Jibu ni ndio
kwanza roho huwa hazifi bali kuna wakati hukosa makao mapya/mwili baada ya zamani kwisha na kuharibika 
Haijulikani hasa nini hutokea lakini hizi ni roho zenye matatizo makubwa na ndio hizi huwa mashetani majini vinyamkera na viumbe vya ajabu ajabu. Ni roho hizi hizi ambazo huweza kuingia kwenye familia kikundi au mkusanyiko wowote na kuleta mirafaruku mikubwa tu ambayo mingine huleta maafa makubwa. 
Kwahiyo roho zipo na zipo sana na kamwe hazifi wala hazipotei jehanam, na pepo zao zipo hapahapa duniani na kwenye kila nyanja ya maisha yetu

from Blogger http://ift.tt/2owCFHM
via IFTTT


Kategori

Kategori