Showing posts with label 2017 at 01:29PM. Show all posts
Showing posts with label 2017 at 01:29PM. Show all posts
Timu ya Arsenal ya England Yachezea Kichapo Kingine…Kocha Arsene Wenger Hoi
Usiku wa April 10 2017 timu ya Arsenal ya England inayofundishwa na kocha Arsene Wenger ambaye kwa sasa mashabiki wengi wa Arsenal wanalalamikia aondoke katika timu hiyo kutokana na kutopatia mataji kwa zaidi ya miaka kumi sasa, usiku huo ilicheza dhidi ya Crystal Palace wakiwa ugenini.
Arsenal ambayo imezoeleka kutofanya vizuri katika Ligi Kuu England lakini haikosekani katika nafasi nne za juu ambazo inawanapata nafasi ya kucheza Champions League, usiku wa April 10 2017 wamechezea kichapo cha magoli 3-0 kutoka kwa Crystal Palace game iliyochezwa katika uwanja wa Selhurst Park.
Magoli yakitiwa wavuni na Andros Townsend dakika ya 17, Yohan Cabaye dakika ya 63 na Luka Milivojevic kwa mkwaju wa penati dakika ya 68 na kuiacha Arsenal ikimaliza mchezo huo ikiambulia kumiliki mpira kwa asilimia 73 na Crystal Palace 27, kipigo hicho kinaifanya Arsenal kufungwa kwa mara ya kwanza mechi nne mfululizo za Ligi kwa mara ya kwanza chini ya Arsene Wenger.
Mechi nne ilizofungwa mfululizo za ugenini Arsenal na Chelsea 3-1, Liverpool 3-1, West Bromwich na leo imepoteza 3-0 dhidi ya Crystal Palace lakini hicho kinakuwa ni kipigo cha kwanza toka Arsenal ipate ushindi wa kwanza wa EPL April 6 2017 dhidi ya West Ham United baada ya siku 53 bila kupata ushindi, mfululizo wa matokeo hayo kuna hatarisha nafasi ya Arsenal kucheza Champions League msimu ujao.
from Blogger http://ift.tt/2poxdGB
via IFTTT
Kimenukaa..Gwajima Azidi Kumchanganya Makonda,Adai Atasema Ukweli Hadi Kieleweke…!!!!
Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amesema ataendelea kusema ukweli na hataogopa chochote.
“Nitaendelea kusema ukweli fitina kwangu mwiko” alisema hayo katika mahubiri yake ya jana kanisani kwake Ubungo.
Pamoja na mambo mengine, Askofu huyo, alisema Clouds Media ni rafiki zake kwa sababu wamewaeleza ukweli watanzania.
Alisema hata waislamu ni rafiki zake kwani ndiyo waliomlea baada ya kutelekezwa akiwa mdogo.
Wasanii maarufu wa redio ya EFM, Mkude Simba na Stanley walikuwa kanisani hapo jana huku Mchungaji Gwajima akiongoza misa kwa mada ya vipaji na vipawa.
TAZAMA HARMORAPA ALIVYO TIMUA MBIO BAADA YA KUIONA BASTOLA
from Blogger http://ift.tt/2onoEeE
via IFTTT
Rais John Magufuli: Nikisema Ukweli, Watanzania Wenye Uchungu Mtalia!!!
Rais wetu kipenzi, Mheshimiwa John Pombe Magufuli, jana alifanya yale ambayo huwa anayapatia kweli kweli!!
Kwa kutumia umahiri mkubwa kabisa, bila shaka aki-apply mbinu za kijeshi alizowahi kujifunza JKT, Mheshimiwa Magufuli aliingia bandarini kwa kushitukiza hali iliyowafanya watu wa pale wapigwe butwaa huku wengine mioyo yao ikipiga mkamba kwa sababu hawakutarajia kutokea Mheshimiwa huyo!!!
Mbinu hizi za kijeshi, na bila shaka zikichanganyika na mbinu za kijasusi; zilimwezesha Mheshimiwa Rais wetu aweze kukamata makontena kadhaa yaliyojaa dhahabu!!!
Huku akionekana kujawa na uchungu kwa nchi yake, Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli alisema:
Kwa taarifa nilizonazo, nikizisema hapa mnaweza mkalia! Dhahabu iliyopo humu ndani! Kwa Mtanzania yeyote anayeipenda Tanzania… atalia! Kwa mali zilizomo humu…!
TAZAMA JAMAA HUYU ALIVYOKOSWA KOSWA NA KIFO KWA AJARI MTONI
from Blogger http://ift.tt/2nuXl4S
via IFTTT
Hassan Kabunda kutoka Mwadui FC awa mchezaji bora wa ligi kuu ya Vodacom wa mwezi Februari
Mchezaji wa timu ya Mwadui FC, Hassan Kabunda amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom wa mwezi Februari kwa msimu wa 2016/2017.
Kabunda aliwashinda wachezaji Laudit Mavugo wa Simba SC na Ibrahim Ajib pia wa Simba SC.
Katika mechi tatu ambazo Mwadui ilicheza kwa mwezi huo, Kabunda alicheza kwa dakika zote 270 na kuisaidia timu yake kukusanya jumla ya pointi sita zilizoifanya ipande kwa nafasi mbili katika Msimamo wa Ligi kwa mwezi huo wa Februari (kutoka nafasi ya nane hadi ya sita).
Kabunda alifunga jumla ya mabao manne katika mechi hizo tatu kati ya sita iliyofunga timu yake. Kiungo huyo mshambuliaji alionesha nidhamu ya hali ya juu, hivyo kutopata onyo lolote la mdomo au kadi kutoka kwa waamuzi.
Kwa kushinda tuzo hiyo, Kabunda atazawadiwa kitita cha sh. 1,000,000 (milioni moja) kutoka kwa wadhamini wa Ligi hiyo, kampuni ya Vodacom Tanzania
from Blogger http://ift.tt/2m9edyH
via IFTTT
Subscribe to:
Posts (Atom)
