WATU watano wa kazi wa Ludewa kutoka familia moja wamefariki
dunia katika ajali ya gari ambayo iliacha njia na kutumbukia mtoni akiwemo
mwanafunzi wa chuo cha uuguzi Lugalawa wilayani Ludewa.
Akizungumza na waandishi wa habari mkoa wa Njombe Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Wilbrod Mtafungwa (Pichani) alisema kuwa watu watano wa familia moja walifariki duni katika ajali ya Gari yenye usajili T 613 AKA iliyotokea katika mto baada ya gari hiyo kuacha njia.
Mtafungwa alisema kuwa marehemu walikuwa wakisafiri kutoka Lugalawa
na kuelekea Shaulimoyo gari waliyo kuwa wakisafiria kutokana na mwendo kasi wa
gari hiyo dereva Halon Haule alishidwa kuimudu gali hiyo na kuingiza mtoni.
Aliwataja marehemu katika ajali hiyo kuwa ni pamoja na
dereva Haule, Winslaus mtweve (40) Upendo Malawa (29), Editor Mtega, (35) Pascko
Mlwilo, (22) Mwanafunzi wa chuo cha uuguzi Lugalawa.
Alisema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa dereva
huyo na kusababisha vifo vya wanafamili hao watano ambao walifariki papo hapo.
Alisema kuwa kasi ya dereva huyo alishindwa kulimudu gali
hiyo na kusababisha kuingiza katika korongo lililopo katika eneo la Lugalawa
ambapo chini yake kulikuwa na mto.
Aliongeza kuwa katika tukio lingine limetokea katika kijiji
cha Malimbuli, Kata ya Manguti, wilaya Makete afisa mtendaji wa Alex Josephat, kijiji
aligundua kuuwawa kwa kuungua moto mtoto Joshua Seth (2)mkazi wa kijiji hicho.
Alisema kuwa marehemu aliungua kwa moto mpaka kufa akiwa
amelala nyumbani kwake na huku akituhumiwa Magreth Msigwa ambaye alikimbia mara
baada ya tukio hilo.
Alisema kuwa chanzo cha tukio hilo ni kuwapo kwa wivu wa
kimapenzi baina ya mtuhumiwa na marehemu kwa kuhisi kuwa kuna uhusiano wa kimapenzi
baina ya Mama wa marehemu na mume wa
mtuhumiwa.
Aidha jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo
ili kumkamata mtuhumiwa na kujibu mashiutaka yanayo mkabili.