Showing posts with label 2017 at 02:36PM. Show all posts
Showing posts with label 2017 at 02:36PM. Show all posts
Noa Sana Aisee..Zitto Kabwe na Waitara Walilia Fedha Bungeni..Wadai Wabunge Hawapati Posho Kama Zamani..!!!

Noa Sana Aisee..Zitto Kabwe na Waitara Walilia Fedha Bungeni..Wadai Wabunge Hawapati Posho Kama Zamani..!!!

Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT –Wazalendo), Zitto Kabwe amesema tangu Serikali ya Awamu ya Tano iingie madarakani, taasisi za uwajibikaji ikiwamo Bunge zinashindwa kufanya kazi kutokana na kutopewa fedha za kutosha.
“Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) amenyimwa fedha. Hii inaonyesha kuwa Serikali haina dhamira ya kweli ya kuwezesha Bunge kufanya kazi yake kinyume kabisa na hotuba ya Rais John Magufuli wakati akifungua Bunge Novembea 2015,” amesema Zitto ambaye ni kiongozi wa chama hicho.
Zitto alikuwa akizungumzia taarifa kwamba, chombo hicho cha kutunga sheria kimekumbwa na ukata, kiasi kwamba kina fedha za muda mfupi ujao.
Mbuge wa Ukonga (Chadema), Mwita Waitara ameunga mkono kauli ya mbunge wa Mtwara vijijini, Hawa Ghasia akisema shughuli za Bunge zimedorora.
“Ni kweli kama alivyosema Ghasia kuwa Serikali imeshindwa kutoa fedha za miradi ya maendeleo kwa wizara mbalimbali. Hata kwenye Bunge imeathiri utendaji,” amesema Waitara.
“Kwa mfano katika kamati wabunge wanakwenda kwenye ziara, lakini hawalipwi posho. Wabunge wanakwenda kwenye ziara hawalipwi posho, mwisho kazi zinashindikana kufanyika.
‘Kamati za Bunge zilitakiwa kukaa kwa wiki tatu, lakini zimeishia kukaa wiki moja kwa sababu ya ukata. Wabunge wanashinda mchana kutwa bila kula. Tumemuuliza Spika akasema hakuna hela.”
Juzi, Ghasia ambaye ni mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, alisema wakati ikiwasilisha maoni kuhusu bajeti ya ofisi ya Waziri Mkuu kuwa kumeonekana changamoto kubwa ya Bunge kupewa fedha kwa wakati na hivyo kuathiri utekelezaji wa baadhi ya majukumu.

from Blogger http://ift.tt/2npCgd3
via IFTTT


Hatarii…Jaji Mkuu Mstaafu Chande Othmani Aibuka na Kutoa Mazito ya Moyoni,Afunguka Makubwa Kuhusu..!!!!

Hatarii…Jaji Mkuu Mstaafu Chande Othmani Aibuka na Kutoa Mazito ya Moyoni,Afunguka Makubwa Kuhusu..!!!!

JAJI Mkuu mstaafu, Mohamed Chande Othman amesema mahakama nchini ziko huru, hazipendelei upande wowote wala kushinikizwa na mtu tofauti na baadhi ya watu wanavyofikiri au wakati mwingine kupotosha.
Katika mahojiano ya kwanza tangu astaafu aliyoyafanya hivi karibuni, Jaji Othman alitoa mfano wa jinsi Mahakama ilivyoshughulikia kwa haraka kesi za uchaguzi wa mwaka 2015 uliokuwa na mvutano mkubwa.
Jaji huyo aliyefanya kazi za sheria nje na ndani ya nchi pamoja na taasisi kadhaa za kimataifa, alieleza kuwa kesi za uchaguzi za ubunge na udiwani zimemalizika bila malalamiko ya upendeleo.
Hata hivyo, anasema bado mahakama ina changamoto nyingi ikiwamo kila mkoa kuwa na Mahakama Kuu, kuongeza idadi ya mahakama za mwanzo na uboreshaji wa miundombinu huku akisikitishwa na baadhi ya mahakama kutokuwa na umeme.
Jaji Othman ambaye alisoma sheria darasa moja na Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda, angependa kuona watendaji wa mahakamani wakipambana ili kuhakikisha wanamaliza kabisa mlundikano wa kesi.
Ukimuliza kitu anachokikumbuka zaidi, Jaji Chande anasema katika utumishi wake mahakamani hatosahau kesi ya mtoto aliyechunwa ngozi mkoani Mbeya iliyofikishwa mbele yake.
Credit – Habari Leo

from Blogger http://ift.tt/2nvYVzM
via IFTTT


Israel: Muuguzi achomwa moto hadi kufa na mgonjwa kwa madai alipewa huduma mbaya

Israel: Muuguzi achomwa moto hadi kufa na mgonjwa kwa madai alipewa huduma mbaya

Muuguzi mmoja nchini Israel amefariki baada ya kuchomwa akiwa hai na mgonjwa katika eneo la Holon kusini mwa Tel aviv.
Tova Kararo mwenye umri wa miaka 56 alimwagiwa mafuta na kuchomwa baada ya kujibizana na mgonjwa ambaye alikuwa hajaridhika kulingana na afisa mmoja wa polisi.
Mshukiwa huyo ambaye yuko katika umri wa miaka 70 alitoroka eneo la mkasa huo kwa kutumia gari lakini akakamatwa baadaye.
Vyombo vingi vya habari nchini Israel vimeripoti kwamba mshukiwa huyo alikuwa manusura wa holocaust anayeugua ugonjwa wa akili.
Mkuu wa polisi katika eneo hilo Sigal Bar Tzvi alisema kuwa mtu huyo aliwasili katika kituo hicho cha afya na alidaiwa kwamba hakuridhishwa na matibabu aliyopata.

from Blogger http://ift.tt/2mCgtuv
via IFTTT


Kategori

Kategori