Showing posts with label 2017 at 02:54PM. Show all posts
Showing posts with label 2017 at 02:54PM. Show all posts
NUHU Mziwanda Kuula Kwenye Lebo ya Ali Kiba…….

NUHU Mziwanda Kuula Kwenye Lebo ya Ali Kiba…….

MKALI wa Bongo Fleva, Naftal Mlawa ‘Nuh Mziwanda’ yupo kwenye hatua za mwisho za mchakato wa kuingia mkataba na ‘record label’ ya Rockstar4000 ambayo pia ina msanii, Ali Kiba.
Akichonga na Over Ze Weekend, Nuh alisema kuwa, haitakuwa busara kila kitu kikawekwa wazi kabla ya makubaliano ya kusaini lakini mashabiki wakae wakijua yupo njiani kujiunga na lebo hiyo.

“Ni kweli nipo kwenye mazungumzo na lebo ya Rockstar4000 ambayo yupo Kiba na soon nitasaini mkataba. Nimekubali kufanya hivyo kwa sababu Kiba ni mtu wangu wa karibu na ninamheshimu kama kaka yangu, naamini tutafanya kazi vizuri tukiwa pamoja huko na hakuna nitakacho-pungukiwa kwa kuminywa kivyovyote vile,” alisema Nuh.

Lebo hiyo pia ina wasanii wengine akiwemo Lady Jaydee, Ommy Dimpoz pamoja na Barakah The Prince.
Mayasa Mariwata

from Blogger http://ift.tt/2uuNTlw
via IFTTT


U-HEARD: Shamsa Ford ameelezea kisa cha kupigwa ngumi

U-HEARD: Shamsa Ford ameelezea kisa cha kupigwa ngumi

April 19, 2017 kupitia U heard ya XXL ya Clouds FM mtangazaji Soudy Brown ametuletea stori inayomuhusu staa wa Bongo movie Shamsa Ford ambaye amepata majeraha jichoni baada ya kupigwa.
Inadaiwa kuwa Shamsa alipata majeraha hayo baada ya kupigwa ngumi wakati anaamulia ugomvi wa 
mtumishi wake wa ndani ambaye alikuwa anazozana na mwanaume aliyemdhalilisha kwa kumshika mwili wake bila ridhaa yake.
Ili kujua undani wa tukio hilo, Soudy alipiga story na Shamsa ambaye alisema: >>>“House girl wangu alichokozwa na mwanaume, so wakawa wanagombana, nikaenda kuamulia basi, ngumi ikanipata. Nilipelekwa hospitali na mume wangu.” – Shamsa Ford.

from Blogger http://ift.tt/2piDI1A
via IFTTT


Hataree..Maalim Seif Atoa ya Moyoni Kuhusu Cuf ,Afunguka Haya Mazito Juu ya Kufukuzwa Ukatibu Mkuu..!!!

Hataree..Maalim Seif Atoa ya Moyoni Kuhusu Cuf ,Afunguka Haya Mazito Juu ya Kufukuzwa Ukatibu Mkuu..!!!

Sarakasi za kisiasa zinaendelea kutawala ndani ya chama cha CUF baada ya Katibu Mkuu wake, Maalim Seif Sharif Hamad, kudai kuwa Profesa Ibrahim Lipumba anatumiwa kukihujumu chama hicho.
Maalim Seif alimtuhumu Profesa Lipumba ambaye ni Mwenyekiti wa CUF, anayetambuliwa na ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini kuwa anakihujumu chama ili kishindwe kudai haki waliyoipata katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 mwaka juzi.
Aliyasema hayo jana katika kijiji cha Tumbatu Mkoa wa Kaskazini Unguja alipozungumza na wanachama wa chama hicho, ikiwa ni ziara maalumu ya uimarishaji wa chama katika mikoa yote ya Kisiwa cha Unguja.
Maalim Seif alisema pamoja na Profesa Lipumba kupata nguvu kutoka vyombo vya dola na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa katika kukihujumu chama hicho, lakini hawataweza kufikia malengo hayo.
Alisema taasisi hizo kwa pamoja zimekuwa zikimuunga mkono Lipumba kwa kumpa kila nguvu anayohitaji ili kuona anafanikisha malengo ya CCM ya kuitawala nchi bila ya kuwepo kwa chama kikuu pinzani, ila nguvu zao hizo zitagonga mwamba.
“Nashangaa sana kuona Lipumba amekubali kutumika na CCM kwa kukihujumu chama kwa masilahi binafsi, lakini nataka muelewe wananchi kuwa pamoja na nguvu zao zote hizo katu hawataweza kuwakatisha tamaa Wazanzibari ya kudai haki yao waliyoipata katika uchaguzi uliopita,” alisema.
Alishangazwa kuona Ofisi ya Msajili kwa kushirikiana na vyombo vya dola badala ya kufuata Katiba na sheria za nchi, wao wamekuwa wakikihujumu chama hicho.
“Pamoja na hujuma hizi zinazofanywa na Lipumba katika chama chetu, lakini nashangaa Rais (John) Magufuli anatumbua watendaji wabovu, lakini humu mrajisi (Msajili) wa Vyama vya Siasa anamuachia,” alisema.
Kuhusu kuondolewa kwenye nafasi yake, Maalim Seif alisema kwa mujibu wa katiba ya CUF, Lipumba hana uwezo wa kumvua nyadhifa hiyo hata kama angekuwa ni mwenyekiti halali.
Alisema kwa mujibu wa katiba yao ili Katibu avuliwe wadhifa wake lazima mkutano mkuu uhudhuriwe na zaidi ya nusu ya idadi wajumbe.
Alisema kikao kilichofanyika chini ya Profesa Lipumba kilihudhuriwa na wajumbe wasiokuwa na ujumbe kihalali, ambao walipandikizwa kuonesha kama kikao hicho kilikuwa halali.
“Ikiwa mimi nimefukuzwa chama kutokana na madai kuwa sihudhurii vikao vinavyofanywa na ofisi za chama hicho jijini Dar es Salaam, mbona yeye Lipumba tangu mwaka 2015 hawajawahi kuja ofisi kuu ya chama ambayo ni mtendeni hadi leo, kwa hiyo naye alitakiwa kufukuzwa,” alihoji.
Maalim Seif alisema kuwa kinachosikitisha ni kuona Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nayo kuidhinisha kuwa wamekubaliana na mageuzi hayo yaliyofanywa na Lipumba kwa kushirikiana na wajumbe wake.
“Ninachokifahamu mimi ndani ya katiba yetu inasema kuwa ili uamuzi wa kuvuliwa nafasi ya uongozi ni lazima anayedaiwa kufanya kosa aitwe na uongozi kujieleza, lakini mimi sijaitwa kujieleza,” alihoji Maalim Seif.
Akizungumzia madai ya kushinda Uchaguzi Mkuu uliopita, Maalim Seif alisema waliwataka wananchi wa Zanzibar kutokata tamaa na haki yao, huku akidai hivi karibuni dola ya Zanzibar itakuwa chini ya CUF.
Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui, alisema uongozi wa CUF unasikitisha kuona vyombo vya dola kuingilia mamlaka ya chama hicho na kusahau wajibu wao.
Alisema kuwa wajibu wa vyombo hivyo ni kusimamia amani ya wanachama na viongozi wake, lakini ni jambo la kushangaza kwa viongozi wa vyombo hivyo kuwa ni miongoni mwa wanaongoza kuonesha chuki dhidi ya CUF.
Alisema pamoja na hujuma hizo, lakini viongozi wakuu wa chama hicho chini ya Maalim Seif, hawatosita kudai haki yao hadi kieleweke.
Akijibu tuhuma hizo, Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho bara na anayemuunga mkono Profesa Lipumba, Magdalena Sakaya alimtuhumu Maalim Seif kuwa ndiye anakula njama za kukidhoofisha chama.
Alisema Seif amekataza ruzuku zisifike kwenye wilaya, hakuna mikutano na hakuna hata pikipiki huku wenzao Chadema waliokuja juzi wamekuwa chama kikuu cha upinzani kutokana na kuwa wamoja.
“Malalamiko anayotoa ajikite kwenye katiba, aichambue kifungu kwa kifungu atabaini anakosea wapi.
“Hii ni taasisi chama, siyo kampuni ya mtu, lazima tufuate katiba tuliyojiwekea ambayo ipo wazi inatoa maelekezo ya kila kitu, anayekengeuka anafanya makusudi na sisi hatuwezi kukaa kimya bila kuchukua hatua ikiwa ni pamoja na kuteua watakaofanya kazi alizotakiwa kufanya yeye,” alisema Sakaya.
Alieleza kuwa badala ya kujenga chama, ameamua kukidhoofisha na anatumiwa kufanya hivyo akijificha kwenye mwamvuli wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
“Amekuwa bwana kesi, kila kukicha anafungua mpya, mimi nina kesi, Lipumba ana kesi, Msajili wa Vyama ana kesi, mwanasheria ana kesi, akae kimya asubiri ziishe, ”alisema Naibu katibu mkuu huyo.

from Blogger http://ift.tt/2osGL6l
via IFTTT


Kuhusu Nape Nnauye, CUF kutangaza hatua nzito

TAARIFA KWA UMMA NA VYOMBO VYA HABARI
Chama cha Wananchi CUF kimepokea taarifa ya hatua ya Rais Magufuli kufanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri na kumuondoa Mheshimiwa Nape Nnauye katika nafasi ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, kwa mshtuko na masikitiko makubwa.
Image result for CUF
Mhe. Nape ameondolewa kwenye Baraza la Mawaziri kibabe na bila aibu kutokana na kusimamia Haki, Uhuru, Uwajibikaji, Nidhamu na Maadlili ya uendeshaji wa vyombo vya habari nchini jambo ambalo ni jukumu la msingi la Wizara yake.
Sote tunatambua kwamba Utenguzi huo unatokana na Mhe. Nape kufuatilia tukio la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kuvamia kituo cha Clouds Media Group kinyume na taratibu, maadili na Nidhamu ya utendaji wa majukumu yake. kitendo hicho pia ni kosa la jinai lisilovumilika.
Kwa niaba ya Chama cha Wananchi CUF, napenda kutumia fursa hii kulaani mwenendo wa Rais Magufuli wa kuitumia nafasi yake kwa namna inayokosa BUSARA na HEKIMA ya uongozi kwa TAASISI ya URAIS.
Kitendo cha Rais kumlinda mtuhumiwa ambaye amefanya makosa ya wazi kabisa kinadhihirisha namna Rais asivyo na utayari wa dhati na uwezo wa kusimamia nidhamu ya watendaji serikalini.
Huko nyuma na mara kadhaa, Rais Magufuli alichukua hatua za haraka sana kuwafuta kazi watumishi na watendaji wa serikali waliofanya makosa madogo mno hata kama ilikuwa ni kimatamshi tu au maamuzi ya bahati mbaya.
Mifano mizuri ni pamoja na Mhe. Anne Killango (aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga), Dr. Mwele Malecela (aliyekuwa anaongoza taasisi muhimu ya utafiti wa magonjwa ya binadamu), Wilson Kabwe (Mkurugenzi wa Jiji la Dar Es Salaam) ambaye alituhumiwa mkutanoni na kufukuzwa hapo hapo bila kuwepo wala nafasi ya kujitetea.
The Civic United Front (CUF) inashangazwa na maamuzi ya sasa ya Rais Magufuli ya kumlinda mtuhumiwa wa makosa makubwa na ya wazi kabisa na kisha kumfukuza kazi Waziri aliyekuwa akitekeleza wajibu wake ili kulinda heshima ya serikali.
Kwa kitendo hiki cha Rais, CUF inaungana na watanzania wote kuamini kuwa Rais Magufuli hana nia njema ya kurejesha nidhamu serikalini, na kwamba yuko tayari kuwalinda vijana wake wachache kuliko kuilinda serikali na heshima ya nchi na Taasisi ya Urais. Rais anashusha hadhi ya Ikulu na sasa ikulu imegeuka kuwa mtetezi mkuu wa watumishi waovu wa umma.
CUF itatangaza hatua nzito hapo baadaye, kwa niaba ya chama natumia fursa hii kumfariji na kumtia nguvu Mhe. Nape kwa ujasiri aliouonyesha na kusimamia kile ambacho ni haki kwa Taifa, wananchi na sekta ya habari.
Namuomba asirudi nyuma kutetea haki za watanzania wote na kamwe asikatishwe tamaa na kitendo hicho kilichokosa utu na heshima, na kujali mchango mkubwa wa kisiasa ndani ya Chama chake na serikali ya awamu ya Tano.
CUF inaungana na watanzania wote kulaani kitendo hicho na kwamba tutakutana pia na vyama washirika katika UKAWA ili kuamua hatua kubwa za pamoja dhidi ya ukosefu wa haki na Demokrasia nchini na matumizi mabaya ya mamlaka.
“CUF NI TAASISI IMARA YENYE VIONGOZI MAKINI”
HAKI SAWA KWA WOTE
JULIUS MTATIRO
MWENYEKITI WA KAMATI YA UONGOZI 
CUF-TAIFA.
23 Machi, 2017.
TAZAMA JAMAA HUYU ALIVYOKOSWA KOSWA NA KIFO KWA AJARI MTONI

from Blogger http://ift.tt/2o86oWD
via IFTTT


Kauli ya TFF Baada ya Mwakyembe kupewa uwaziri wa Michezo

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limempongeza Mheshimiwa Dk. Harrison Mwakyembe kwa kuteuliwa kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Katika taarifa iliyotolewa leo kwa wana habari, imesema kuwa shirikisho hilo linaamini chini ya uongozi wake mahiri Tanzania itapiga hatua kubwa zaidi katika maendeleo ya michezo.
Naye Rais wa TFF, Jamal Malinzi kupitia mtandao wa twitter amesema “TFF inampongenza Dkt. Harrison Mwakyembe kwa kuteuliwa kuwa Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo.Tunakuombea mafanikio makubwa.Amina.”
TAZAMA JAMAA HUYU ALIVYOKOSWA KOSWA NA KIFO KWA AJARI MTONI

from Blogger http://ift.tt/2nqNE7q
via IFTTT


Kategori

Kategori