Showing posts with label 2017 at 10:37AM. Show all posts
Showing posts with label 2017 at 10:37AM. Show all posts
CMSA NA KIGUGUMIZI CHA TAARIFA KWA WANUNUZI WA HISA ZA VODACOM

CMSA NA KIGUGUMIZI CHA TAARIFA KWA WANUNUZI WA HISA ZA VODACOM

Sheria ya Fedha 2017 inalenga kuwawezeshaje watanzania kama Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) imekuwa kimya kuhusu hatma ya fedha zetu toka kufungwa kwa uuzaji wa hisa wa awali (IPO) wiki saba zilizopita?
Wengi wetu tulivunja vibubu vyetu ili kununua hisa za Vodacom lakini mpaka leo Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) imekuwa kimya juu ya hatma za fedha zetu. Tuna haki ya kufahamishwa nini kinaendelea.
Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) iliongeza siku 10 za uuzwaji wa hisa (IPO) ili kuwanufaisha wageni lakini imekuwa kimya kuhusu wazawa walionunua hisa zao wiki saba zilizopita.
CMSA ijifunze kutoa taarifa kwa wakati ili kusaidia kujenga imani kwa watanzania vinginevyo IPO za makampuni mengine ya simu zitakwama.
Airtel imetanga IPO yao lakini bado kuna sintofahamu ya IPO ya Vodacom inayosababishwa na ukimya wa CMSA kuhusu ziliko fedha zetu.
Hawa CMSA wanatuchelewesha kupata gawiwo letu kutoka Vodacom. Tueleweze kitu gani kinaendelea.
Leo nimekutana na mwanafunzi ambaye ametumia akiba yake TZS 300,000 aliyoikusanya kwa zaidi ya miaka mitatu kununua hisa za Vodacom lakini hana taarifa kuhusu uwekaji huo.
Wiki saba zimepita lakini watu wote tulionunua hisa za Vodacom hatujapata ‘share certificates’ zetu. CMSA imekaa kimya. Ni haki yetu kupata taarifa kuhusu uwekezaji tulioufanya.
Nimepiga simu CMSA kuomba taarifa za IPO ya Vodacom baada ya kupata wasiwasi na ukimya wao. Nimejibiwa nisubiri wakati nimeshasubiri kwa wiki nane. Kulikoni CMSA?

from Blogger http://ift.tt/2thbH81
via IFTTT


Baba Mzazi akamatwa kwa Tuhuma za Penzi la Mwanaye wa Kumzaa

Baba Mzazi akamatwa kwa Tuhuma za Penzi la Mwanaye wa Kumzaa

PWANI: Dunia ime­kwisha! Fadhil Msha­mu, mkazi wa Kibaha Kwa Mfipa mkoani Pwani, Jumanne iliyopita ali­kumbwa na aibu kubwa, baa­da ya kubambwa na polisi, akidaiwa kumshawishi binti yake wa kum­zaa ili ampe penzi.
…Baba huyo akiwa na mwanaye aliyekuwa akimfosi penzi.
UANZE MKASA HUU KWA UMAKINI
K i t e n g o Maalum cha Oparesheni Fi­chua Maovu (OFM) cha Glo­bal Publishers, mwanzoni mwa wiki hii kilipokea simu kutoka kwa mwanam­ke mmoja, ali­yedai wanahitaji msaada kwani katika familia yao, kuna tatizo kubwa ambalo limewasumbua kwa muda mrefu.
… Akiwa katatiwa na polisi.
M w a n ­amke huyo a l i y e d a i a n a i s h i Buguruni jijini Dar es Salaam, alipotakiwa k u d o k e z a tatizo hilo, alidai kuwa ka­tika familia yao, kuna baba anataka kuvunja amri ya sita na binti yake!
OFM WASHTUKA, WATUA BUGURUNI
Kwa taarifa hiyo ya kush­tusha, makamanda wa OFM walilazimika kufika Buguruni ili kupata habari kamili na ku­fika huko, walikutana na mwa­namke aitwaye Tatu Mshamu waliyezungumza naye kwa simu, ambaye alijitambuli­sha kama shangazi wa binti anayetakiwa kutenda dhambi hiyo na baba yake!
HUYU HAPA SHANGAZI
“Huyu ni mtoto wa kaka yangu, kila siku anatuambia baba yake anamsumbua, an­amtaka kimapenzi. Tumejari­bu kukaa naye na kuzungum­za, lakini anatuambia watoto wanamsingizia tu, siyo kweli. Tunajiuliza kwa nini kila siku wakusingizie wewe tu?
“Sasa leo tukaona labda kweli hawa watoto huenda wana lao jambo, tukamwam­bia huyu binti, hebu tuthibi­tishie kama unachoongea ni cha kweli, akasema ngoja apige simu kwa baba yake, akaweka laudi spika!
“Akampigia mbele yetu, tukawa tunamsikia anavyo­mbembeleza. Sasa sisi tu­mechoka, tunataka hili jambo bora lijulikane, maana tume­zungumza naye haelewi, kama mbwai na iwe mbwai tu!”
FAMILIA YAJIPANGA KUMNASA BABA
Wanafamilia hao wali­waambia makamanda wa OFM kuwa walikuwa wame­andaa mtego wa kumkamata baba huyo, kwani tayari al­ishaanza mawasiliano na mwanaye, akimtaka kwenda Kibaha Kongowe ili kwenda kujivinjari naye.
Baada ya kusikia madai hayo mazito na jinsi ya kukutana eneo la tukio, makamanda wetu wakitumia usafiri wao wa mwendokasi, wali­wasili Kibaha Kongowe salama salimini kabla ya kupokea simu kutoka kwa shangazi mtu, aki­waelekeza jina la gesti ambayo baba mzazi alikuwa akimsubiri binti yake.
NEW KILAWENI GUEST HOUSE
Kwa kuwa maka­manda hao walikwi­shamtambua binti huyo anayedai baba yake ku­taka afanye naye ufuska huo, walipofika eneo la tukio, njia ya Soga eneo la Kwa Mmbaga, wal­imuona akiwa amekaa kwenye kiti na meza am­bayo pia aliku­wepo mwa­naume akinywa bia, ambaye kwa harakaha­raka waliamini alikuwa ndiye baba yake mzazi.
POLISI WAIBU­KA, K I Z A A Z A A CHAZUKA
OFM waki­wa hawana hili wala lile, ghafla wakaona kundi la askari zaidi ya nane waki­ibukia eneo hilo, wakiwa w a m e o n ­gozana na shangazi wa binti, Tatu Mshamu na mama mzazi wa binti, An­tonia Mango.
K i t e n d o cha watu hao kuibuka eneo hilo ghafla, kilim­fanya baba mtu kuha­maki, hasa baada ya k u amb iwa kuwa yupo chini ya ulinzi kwa tuhuma ya kufosi penzi kwa binti yake.
ETI WALISHAZAMA GES­TI
Katika hali ya kush­angaza, binti huyo aliua­mbia umati uliokusan­yika hapo kuwa kabla hawajatokea, baba huyo alimpeleka katika chum­ba cha gesti hiyo na ku­taka walale lakini akam­kimbia.
“Alinipeleka chumba namba moja, kulikuwa na kitanda tu, akawa anata­ka tulale, mimi nikakataa, akanifichia viatu vyangu, nikamponyoka nikaja hapa, ndiyo akanifuata akawa ananibembeleza,” alidai binti huyo na ku­waacha watu midomo wazi.
MHUDUMU WA GESTI ASIMULIA
Mhudumu wa gesti hiyo ambaye jina lake ha­likupatikana mara moja, aliwathibitishia polisi kuwa baba huyo alikodi chumba na kuingia na binti huyo chumbani.
AKUTWA NA FUNGUO, ATAITIWA
Huku akiendelea ku­bisha kuwa hakuingia na binti yake chumbani, mzee huyo alikutwa na ufunguo wa chumba namba moja wa gesti hiyo, kitu kilichosababi­sha akose la kusema.
Polisi walimtaiti na kumtaka waelekee chumba walichoingia, ambacho kilikuwa na kitanda tu na kulaz­imishwa kuonyesha alikoweka viatu vya bin­tiye, ambavyo baadaye vilikutwa vikiwa katika kona ya chumba hicho.
SHANGAZI, MAMA
WAZUA TIMBWILI
Kuona hivyo, shangazi na mama mzazi wa binti huyo ambaye kwa sasa alishaachana na mwa­naume huyo, walianza kumshambulia, wakim­tuhumu kuwa anafanya mambo ya aibu.
Timbwili hilo lililoam­batana na maneno maz­ito kutoka kwa mama na shangazi huku baba mtu akijibu mashambulizi, lilichukua muda mrefu kabla ya mtuhumiwa kugeuka ‘mdogo kama piritoni’ kwa aibu.
WASOMBWA POLISI
Kufuatia sakata hilo, maafande hao waliwa­chukua mama, shangazi, binti huyo na baba yake na kuwapeleka Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Kibaha ambapo baada ya mahojiano walimfun­gulia jadala la uchun­guzi lenye namba KBA/ RB/4067/2017.
Baadaye baba huyo alihamishiwa Kituo Kikuu cha Mkoa na ku­funguliwa jalada ling­ine lenye namba KBA/ IR/2278/2017 JALADA LA UCHUNGUZI.
Mpaka gazeti hili linakwenda mtamboni haikufahamika kili­choendelea baada ya hapo ila tunaahidi ku­waletea muendelezo wa habari hii kwenye maga­zeti yanayofuata ya Glo­bal Publishers.
chanzo: GPL
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2tdYpec
via IFTTT


Tazama Diamond alivyo Copy Na Ku-Paste Video ya Jason Darulo

Tazama Diamond alivyo Copy Na Ku-Paste Video ya Jason Darulo

SOKO la nyimbo katika dunia ya sasa linakuzwa na video za muziki, ubora wa video umekuwa ukichangia kuufanya wimbo kuwa mkubwa hata kama ni wa kawaida.
Kuna vitu vingi vinavyochangia video kuwa bora, baadhi ni ubora wa picha, ubora wa mandhari na ubora wa ubunifu wa kile kinachoonekana katika video husika.
Msanii wa Tanzania, Diamond Platnumz anajulikana kwa kuwekeza nguvu kubwa kwenye kutengeneza video zenye kiwango cha juu, hilo halina ubishi.
Pamoja na sifa hizo, imekuwa ni kawaida kuona Diamond akiiga matukio kadhaa ya video za wasanii wa Marekani na kuziingiza kwenye video za nyimbo zake.
Mfanano wa video au jambo lolote ni kitu cha kawaida lakini kuna mazingira ambayo yanaweza kumfanya mpaka shabiki au mtazamaji wa video akaelewa kuwa hakuna mfanano wa bahati mbaya bali ni makusudi.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2tAxgFs
via IFTTT


Sababu za Wanawake Kuvutiwa na Wanaume Wenye Uwezo Mkubwa Kiakili

Sababu za Wanawake Kuvutiwa na Wanaume Wenye Uwezo Mkubwa Kiakili

  • Mwanamke akiwa na uwezo mkubwa kiakili, lazima atahitaji mwanaume anayeufikia au kuzidi uwezo huo ili waweze kujadiliana mambo mbalimbali.
  • Wanaume wenye akili sana hawazungumzii ngono wakati wote, wana mambo mengi sana ya kuzungumzia. Mwanamke mara zote huvutiwa sana na uwezo wa mwanaume kumudu mazungumzo ya kina kwa mada mbalimbali.
  • Wanawake wanapenda kuwa na mwanaume atakayevutiwa naye mara zote. Mwanaume mwenye uwezo mkubwa kiakili anavutia wanawake kirahisi sana.
  • Mvuto wa kingono unaazia akilini mwa mtu, mwanaume mwenye akili nyingi ana uwezo wa kuingia akilini mwa mwanamke mwenye uwezo mkubwa kiakili.
  • Uwezo mkubwa wa akili kwa mwanaume unaothibitisha kuwa unatafiti kutaka kujua na kujifunza mambo mbalimbali, njaa hiyo hiyo ya kutaka kujua mambo ndio atakayoionesha au atakayokuwa nayo kutaka kumjua mwanamke wake, vitu anavyothamini na pia katika kuujua mwili wa mwanamke wake. Mwanamke mwenye akili anapenda sana achunguzwe na mwanaume wake.
  • Mwanamke ni zaidi ya chombo cha kumstarehesha kingono mwanaume wake; bali ni kiumbe mwenye akili zake, mwenye imani, mwana jamii, mbunifu na kiumbe ambaye haeleweki kirahisi. Mwanaume mwenye uwezo mkubwa kiakili ana uwezo wa kuchunguza na kujua vitu vyote kuhusu mwanamke wake.
  • Mwanaume mwenye uwezo mkubwa kiakili ni chachu kubwa ya kufanikisha maendeleo ya kimaisha kwa mwanamke. Mwanamke anapenda kuwa na mwanaume ambaye anaweza kujifunza mengi kutoka kwake au watakaofanya maendeleo ya pamoja. Mwanamke akiwa na mwanaume wa aina hii atajikuta anapenda mara zote kuwa karibu na mwanaume wake. Atakubali starehe na shida zote watazozipata pamoja akiichukulia kama ni kutengeneza hadithi ya maisha yao.
  • Mwanaume mwenye uwezo mkubwa kiakili ambaye pia hana majivuno au kiburi ni rahisi kuishi naye, ni rahisi kufanya naye kazi na ni rahisi kuzungumza naye. Wanawake huwa wanasisimka wakiwa katika maongezi ya kimapenzi na mwanaume wa aina hii. Mhusishe mwanamke wako kwenye mazungumzo mazuri na yeye atakupatia mapenzi kwa kiwango kitakachokushangaza kabisa.
  • Mwanaume mwenye uwezo mkubwa kiakili anakuwa amepevuka kiasi kwamba uso wake, macho na muonekano wake wa nje tu unaweza kumuelezea alivyo. Mara nyingine jambo pekee unalotakiwa kufanya ni kumuangalia tu na yeye atapata hisia na ujumbe wa kutakwa kimapenzi na mwanaume wake.
  • Mwanaume mwenye uwezo mkubwa kiakili ana “kidunia chake” kila anapokuwepo. Anaingia sehemu akiwa anajiamini sana na uwepo wake lazima uonekane. Ni mtu imara mwenye akili thabiti inayojua mambo mengi. Akiwa karibu na mpenzi wake, mwanamke huyo mara moja atataka aendelee kuwepo sehemu hiyo.
Uwezo mkubwa wa kiakili unatokana na ukomavu wako tu, haijalishi kama una elimu za juu sana kama digrii ya chuo kikuu au PhD. Ni hali ya mtu kuwa na busara, kuwa na fikra kubwa, kuwathamini wanawake wote na kumuwezesha na kumuinua mwanamke pekee unayempenda maishani mwako.
 ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2sJcdj6
via IFTTT


Msimu ujao Paul Pogba atakuwa hashikiki

Msimu ujao Paul Pogba atakuwa hashikiki

Japokuwa katika msimu wake wa kwanza Epl baada ya kununuliwa kutoka Juventus hakuwa na kiwango bora sana kama mashabiki walivyotegemea lakini alicheza vizuri na akiisaidia United kubeba kombe la Europa.
Msimu ujao hakika anaweza kuwa bora sana na mashabiki wa Manchester United wakamfurahi sana Paul Pogba kama ambavyo mchezaji mkongwe wa timu hiyo ambae sasa ni mchambuzi wa soka Ryan Giggs anavyoamini.
Giggs anaamini kwamba msimu ujao wa ligi kuu ya Epl huenda wapinzani wa Paul Pogba wakawa katika wakati mgumu sana kwani kiwango cha Mfaransa huyo kinaweza kurudi katika level aliyokuwa nayo wakati akiwa Juventus.
Imani ya Giggs imekuja baada ya kiwango bora sana ambacho Pogba alikionesha wakati wa pambano la kimataifa la kirafiki kati ya Ufaransa na Uingereza pambano ambalo liliisha kwa Ufaransa kushinda mabao 3 kwa 2.
“Ukimuangalia alivyocheza dhidi ya Uingereza lazima utasisimkwa kama wewe ni shabiki wa United haswa ukiwaza kwamba huyu mchezaji atacheza hivi katika msimu ujao wa ligi anaweza kuwa hashikiki” alisema Giggs.
Wachambuzi wengine akiweomo Ian Wright ambaye naye alikuwa akiangalia mchezo huo alikiri kwamba kama kiwango alichokionesha Paul Pogba dhidi ya Uingereza atakileta katika ligi ya Epl baasi atawasha moto.
 ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2t8Ewoz
via IFTTT


Rais Magufuli Azidi Kumuumbua Dk Mwakyembe….!!!

Uamuzi wa Rais John Magufuli kufuta agizo lililotolewa na Dk Harrison Mwakyembe la kuweka sharti la vyeti vya kuzaliwa katika ndoa, unamuweka njiapanda waziri huyo wa sheria na katiba, huku wachambuzi wakisema hakufanya mawasiliano kabla ya kuagiza.
Mbali na kufuta, Rais amesema alishtushwa na agizo hilo kutokana na ukweli kwamba halikujadiliwa katika vikao vya Baraza la Mawaziri.
Mwakyembe, ambaye kitaaluma ni mwanasheria, aliagiza ofisi za wakuu wa wilaya, viongozi wa dini na wa kimila kutofungisha ndoa iwapo wahusika hawana vyeti vya kuzaliwa kuanzia Mei mosi.
Alitoa agizo hilo juzi mjini Morogoro alipozungumza na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya na wawakilishi wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (Rita) wakati akiwa katika ziara ya siku mbili mkoani humo.
“Serikali ya Dk John Magufuli imekusudia kukuza uchumi wa nchi kupitia viwanda. Hatuwezi kufanikiwa bila ya kuwa na takwimu sahihi,” alisema Mwakyembe.
Lakini jana, Rais Magufuli alifuta agizo hilo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi kabla ya kuondoka Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma kurejea Dar es Salaam, akisema kuwa sharti hilo linanyima haki ya kuoa na kuolewa kwa watu wasio na vyeti vya kuzaliwa.

from Blogger http://ift.tt/2nnoB5C
via IFTTT


Baada ya Kuwa Muathirika wa Dawa za Kulevya kwa Muda Mrefu,Chidi Benzi Amefunguka Haya Makubwa..Amemtaja Joh Makini…!!!!

Rapa Chid Benz amedai kolabo yake na Joh Makini ilishindikana baada ya kushindwa kuwasiliana na msanii huyo baada ya kumaliza Kilimanjaro ‘Tour’ na baadae mambo mengine kutokea ambayo yalikwamisha yeye kukutana na Joh Makini. 
Chid Benz Chuma amezungumza hayo kwenye kipindi cha Bongofleva Top 20 leo na kusema siku zote alikuwa na mipago ya kufanya kazi na msanii huyo kutoka kundi la Weusi na hata walipokutana kwenye kazi walikubaliana wakirudi Dar es salaam wafanye kazi.ie kazi”.

from Blogger http://ift.tt/2mIx7Zg
via IFTTT


Kategori

Kategori