Showing posts with label 2017 at 12:30PM. Show all posts
Showing posts with label 2017 at 12:30PM. Show all posts
Mwalimu afumwa akifanya mapenzi na mwanafuzi wake darasani

Mwalimu afumwa akifanya mapenzi na mwanafuzi wake darasani

Mkuu wa Wilaya ya Wanging’ombe, Mkoani Njombe, Ally Kasinge ameagiza kushikiliwa kwa Makamu Mkuu wa shule ya sekondari Wanike, iliyopo katika wilaya hiyo baada ya kukamatwa akifanya mapenzi na mwanafunzi wake darasani usiku.
Kasinge ametoa agizo hilo baada ya kuwepo taarifa ya kuwepo kwa watu wanaotaka kumsaidia mwalimu huyo kuvuruga ushahidi kwa kupanga na wanafunzi wenye ushahidi huo kuongea tofauti na tukio.
“Kuanzia wanafunzi walitimuliwa wahojiwe na polisi na wale wanafunzi wengine waliotajwa pia wahojiwe na polisi na mwalimu mwenyewe pia aendelee kushikiliwam huyo ambaye anatuhumiwa aendelee kushiliwa na polisi mpaka tupate majibu, kwa sababu akibaki nje ataendelea kutengeneza mazingira ya kutengeneza mtandao wa kutaka kumsaidia na kupotosha ushaidi” alisema Mkuu wa Wilaya Ally Kasinge
Mbali na hilo shule ya sekondari ya Wanging’ombe pamoja na Wanike zimepandishwa hadhi na sasa zitapokea wanafunzi wa kidato cha tano, walimu wa shule hizo wameweka wazi kuwa shule hizo zinachangamoto ya walimu wa sayansi ambao ni wachache ukilinganisha na walimu wa masomo ya sanaa.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2twHiHE
via IFTTT


Wamachinga Sasa Kupewa Vitambulisho vya Kazi Yao….

Wamachinga Sasa Kupewa Vitambulisho vya Kazi Yao….

KATIKA mwaka wa fedha 2017/18, serikali imesema itawatambua rasmi wafanyabiashara wadogo wadogo wasio rasmi kwa kuwapatia vitambulisho maalumu vya kazi wanazozifanya.
Akiwasilisha Bungeni mapendekezo ya serikali kuhusu makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2017/18, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, alisema jana mbali na kupatiwa vitambulisho maalum pia watatengewa maeneo.
Alisema wafanyabiashara hao ni pamoja na mama lishe, wauzaji mitumba wadogo, wauza mazao ya kilimo wadogo kama mboga mboga, ndizi, matunda na kadhalika.
Biashara zafungwa
Akizungumzia kuhusu kufungwa kwa biashara, Dk. Mpango alisema jumla ya biashara 7,277 zilifungwa katika mikoa mbalimbali nchini kwa mwaka wa fedha unaomalizika Juni 30.
Alisema suala hilo lilizungumzwa sana na wananchi na wabunge kutokana na kasi ya kufungwa kwa biashara hususan eneo la Kariakoo katika Jiji la Dar es salaam na katika miji mingine.
“Kwa mujibu wa taarifa zilizofikishwa TRA, katika kipindi cha kuanzia julai 2016 hadi machi 2017, jumla ya biashara 7,277 zilifungwa katika mikoa mbalimbali nchini,” alisema.
Alibainisha kuwa mwenendo huo kwa ujumla siyo mzuri kwasababu wananchi wanapoteza ajira na kipato, serikali inakosa mapato ya kodi na uchumi unadorora.
Alisema ni muhimu pale wimbi la kufungwa kwa biashara linapotokea jitihada zifanyike kuelewa aina gani za biashara zinafungwa, kwanini zinafungwa na hatua gani zichukuliwe kudhibiti hali hiyo.
Aidha alisema zipo sababu nyingi zinazoweza kuwa zimepelekea hali hiyo, ikiwa ni pamoja na ushindani mkali wa kibiashara, usimamizi dhaifu wa biashara, kuongezeka kwa gharama za kufanya biashara kama vile usafirishaji, kodi na tozo mbalimbali

from Blogger http://ift.tt/2sK1pym
via IFTTT


Mume Ashtukia Mke Wake Unaliwa na Bosi Wake…Hichi Ndicho Alichoamua Kufanya

Mume Ashtukia Mke Wake Unaliwa na Bosi Wake…Hichi Ndicho Alichoamua Kufanya

Huko nchini Kenya jamaa mmoja aliyekuwa na uhusiano wa kimapenzi na mfanyakazi wake ambaye ni mke wa mtu ameadhibiwa kwa style ya aina yake. Inaelezwa kuwa mwanamke huyo aliyekuwa akitembea na bosi wake alishtukiwa na mumewe na kuonywa lakini hakusikia. Kilichofuata ni mumewe kuvizia gari la bosi huyo na kuliandika kwa maandishi makubwa ya rangi nyeupe maneno yasemayo ‘Achana na mke wangu’.

from Blogger http://ift.tt/2sN78T7
via IFTTT


Kimenukaa..Zari na King Lawrence Wagombania Mali za Ivan,,King Lawrence Amchana Bila Chenga Zari Kuhusu Kuachana na Ivan,Amwambia Hana Chake..!!!

Kimenukaa..Zari na King Lawrence Wagombania Mali za Ivan,,King Lawrence Amchana Bila Chenga Zari Kuhusu Kuachana na Ivan,Amwambia Hana Chake..!!!

Kufuati kifo cha mfanyabiashara maarufu nchini Uganda na Afrika Kusini, Ivan Ssemwaga, familia na marafiki wa marehemu wamepinga vikali kuhusu aliyekuwa mkewe, Zarina Hassan kutaka kurithi mali za marehemu.
Hali hiyo imebainishwa na Mtandao wa Big Eye wa Uganda ambao ulimhoji mmoja wa marafiki wa Ivan aliyeeleza hali halisi ilivyo. Chanzo cha habari hii kilisema kuwa Zari amevutana sana na Lawrence Kiyingi ‘King Lawrence’ ambaye alitaka kupora mali za Ivan likiwemo gari la bei mbaya aina ya Lamborghini.
King Lawrence alikuwa rafiki wa karibu wa Ivan na pia ni mwanachama wa kundi la Rich Gang ambalo ni maarufu nchini Uganda kwa kuandaa na ku-host shoo za nguvu.
Chanzo hicho kilieleza kuwa ilifikia wakati madaktari wakawatimua Zari na King Lawrence hospitalini alipokuwa amelazwa Ivan kwa sababu walizua mtiti wakigombana kuhusu mali za Ivan.
“At one point, these fights reached hospital and the two together with other family members had to be thrown out of hospital for the peace and sanity of the sick person. Ivan saw these fights, read some on Facebook but he just could not reply to anything. Someone had to hold the phone for him. And he had no reply just the hissing sounds. Deep down, he must have felt betrayed, used and abandoned by those he considered his closest,” chanzo hicho kilisema.
Zari alionekana kwenye video Instagram akigombana huku akisema kuwa mali za mumewe wa kitambo ni za watoto wake watatu aliowazaa akiwa bado ni mke wa Ivan. Hii ilikuwa siku moja kabla ya Ivan kuaga dunia.
Chanzo hicho pia kilisema kuwa Zari aliwaomba madaktari kuahirisha kutangaza kifo cha Ivan ili aweze kujipanga kabla ili kuwadhibiti wanaopanga kuiba mali za mume wake huyo wa zamani.
Mwanasheria wake aliyetakiwa kuwasiliana naye ili kuweka mipango sawa, alikuwa amesafiri kuelekea Ufaransa ndipo akaomba madaktari wampe siku moja ili kujipanga kabla ya kutangaza msiba huo.
Mrembo huyo alitangaza mwenyewe kifo cha mumewe usiku wa kuamkia juzi Alhamisi baada ya kumaliza kuondoa vitu vyote ndani ya nyumba na kuvihamishia kwingine.
Inasemekana Ivan aliaga dunia Jumanne asubuhi baada ya madaktari kudhibitisha kuwa viungo vyake vya mwili vilishindwa kufanya kazi.
Inasemekana ugomvi wa Zari na familia ya Ivan siyo mpya, ulianza kitambo na chanzo chake ilikuwa ni hizo mali na alichokuwa akiwaeleza ni kwamba mali hizo ni za watoto watatu ambao Zari amezaa na Ivan wakiwa mke na mume.
Kutokana na ugomvi huo, mmoja ya mashabiki kupitia Facebook, alimjibu King Lawrence;
“King Lawrence tafuta maisha yako. Ivan Ssemwanga siyo baba yako. Ivan ana watoto na bado ni wadogo kurithi na kuendeleza mali za baba yao, Zari anaweza kuwasaidia. Ndugu wa Ivan wanaweza kufanya kazi zao wenyewe, acheni kuwa wavivu kugombania mali zisizo za kwenu. Mnataka Zari aachane na mpenzi wake (Diamond) kwa sababu ya mali. Anaweza kuwa na dunia yote……”

from Blogger http://ift.tt/2r3CpDo
via IFTTT


MWANAMKE AWAGONGA POLISI KWA GARI

Polisi mjini Washington nchini Marekani, wamemfyatulia risasi mwanamke mmoja aliyekuwa ndani ya gari, baada ya kugonga gari la polisi lililokuwa karibu na Bunge la Marekani na baadaye kujaribu kuwagonga maafisa kadhaa wa polisi.
Tukio hilo lilitokea wakati maafisa wa polisi walipojaribu kumsimamisha dereva huyo mwanamke aliyekuwa akiendesha gari kwa njia isiyo ya kawaida. Ndipo dereva huyo alipogeuza gari kwa haraka nusura awagonge baadhi ya Polisi.
Kwa mujibu wa msemaji wa polisi mjini Washington, Mwanamke huyo hakupigwa risasi lakini alikamatwa na tukio hilo likasababisha kufungwa kwa moja ya majengo ya Bunge.
Mwanamke huyo bado hajatambuliwa wala lengo lake kutambuliwa.
Kisa hicho kinajiri baada ya kushuhudiwa mashambulizi kadha ya watu kugonga wengine kwa magari katika miji ya London na Brussels. Msemaji wa Polisi, Eva Malecki, amesema kuwa mshukiwa ni mwanamke na anatuhumiwa kwa kufanya tukio la uhalifu.
Vikao vya bunge vinaendelea kama kawaida na watalii wameruhusiwa kurudi eneo hilo.
Tazama video Mtoto amvua kofia
 Papa Francis

from Blogger http://ift.tt/2nROXfL
via IFTTT


HALI YA UCHUMI: KAMPUNI NYINGINE YATANGAZA KUWAFUTA KAZI WAFANYAKAZI 50

Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) limeitisha majadiliano kuhusu hali ya uchumi wa nchi inavyokwenda na kupelekea wafanyakazi kwenye makampuni mengi kupoteza ajira zao kutokana na kushindwa kulipwa stahiki zao.
Rais wa TUCTA, Tumaini Nyamhokya alisema kuwa watafanya mkutano wa siku mbili na wadau kuhusu hali ya uchumi kujadiliana njia na hatua za kuchukuliwa ili kuzia watu kupoteza ajira zao hasa kwenye sekta binafsi.
Wakati hayo yakiendelea, Tanzania Distilleries Limited ambayo ni kampuni tanzu ya Tanzania Breweries Limited imetangaza kupunguza wafanyakazi wake wasiozidi 50 ili kuweza kukabiliana na hali ya kiuchumi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Machi 27 na kampuni hiyo, wale wote watakaoathiriwa na uamuzi huo wataliwa stahiki zao zote.
Tazama video Mtoto amvua kofia
 Papa Francis

from Blogger http://ift.tt/2oG3V5K
via IFTTT


Usijipe Presha, Kama Unampenda Muamini Kisha Ziba Masikio!

ili uweze kudumu katika uhusiano wako unatakiwa kujenga mazingira ya kumuamini sana mpenzi wako. Nasema hivyo kwa kuwa, mapenzi ni imani. Ni sawa na kuamini Mungu yupo licha ya kwamba hujawahi kumuona.
Vivyo hivyo, amini tu kwamba mpenzi wako anakupenda kwa dhati licha ya kwamba hujaufungua moyo wake na kathibitisha kwamba ndani yake uko wewe peke yako.
Mpende, muamini na weka akilini mwako kwamba, kamwe hawezi kukusaliti licha ya kwamba kinyume chake pia ni sawa. Hiyo itakusaidia wewe kuendelea kuishi maisha ya furaha na amani bila kuwa na presha.
Jiulize, ni wanaume wangapi ambao wake zao wanagawa penzi nje ya ndoa lakini wao wanawaamini kupita maelezo?
Ni wanawake wangapi ambao waume zao ni viwembe kwelikweli lakini wanawaamini kupindukia? Unadhani ni kwa nini?
Ni kwa sababu wamejijengea mazingira ya kuwaamini wenzao wao wa kiwango kikubwa na kuziba masikio yao kukwepa wambeya.
Tutambue tu kwamba, katika maisha kuna kitu kuridhika. Unapokuwa na mtu ambaye anakupa kila aina ya furaha maishani mwako bila kuonesha tabia zozote zinazokutia mashaka juu ya penzi lake, huyo mpende, mheshimu na muamini.
Hata kama kuna uwezekano wa yeye kuwa anaficha makucha yake na kuyachomoa pale anapokuwa mbali na wewe, kwa sababu huna uhakika na hujawahi kumuona, chukulia kwamba yeye ni msafi kisha yaache maisha yenu yaendelee kuwepo.
Nasema hivyo kwa sababu, tukianza kuchunguzana hakuna ambaye ni msafi kwa asilimia mia moja. 
Kila mtu anajiamini mwenyewe lakini huwezi kuiamini nafsi ya mwenzako kwa asilimia zote.
Ndiyo maana nikasema, unapoingia katika uhusiano na mtu ambaye umetokea kumpenda sana, ongea na moyo wako. 
Moyo wako ndiyo utakueleza kama mpenzi wako ni muaminifu ama siyo na pindi utakapoona dalili za kwamba ni tapeli wa mapenzi mwenye lengo la kutaka kukuchezea kisha kukuacha solemba, usimng’ang’anie eti tu kwa sababu umeoza kwake, muache!
Tatizo tulilonalo wengi ni kutokuwa tayari kuwakosa wale ambao tumetokea kuwapenda sana bila kujua kwamba unaweza kutokea kumpenda mtu lakini yeye akawa hana mapenzi ya dhati moyoni mwake dhidi yako.
Ifike wakati tukubaliane na uhalisia kwamba, unapoona uliyenaye anakuzingua, yupo mwingine mwenye penzi la dhati kwako ambaye anasubiri umuache huyo uliyenaye ili awekeze penzi lake kwako.
Kwa kumalizia naomba niseme kwamba, mapenzi ya siku hizi usipoangalia yanaweza kukufanya ukawa chizi. 
Hii ndiyo inayosababisha baadhi ya watu kufikia hatua ya kusema kwamba, hawahitaji kuwa na wapenzi katika maisha yao. Kwa nini? Kwa sababu kila uhusiano wanaoingia wanakutana na usanii.
Elewa kwamba, una haki ya kupenda na kupendwa, ukishampata yule unayedhani atayafanya maisha yako kuwa ya furaha, mpende kwa dhati na muamini kwamba hawezi kukusaliti lakini, wakati huo hutakiwi kubweteka, chunguza nyendo zake na kama utabaini kwamba anajiheshimu, ongeza mapenzi kwake lakini kama utabaini kuwa hajatulia, muache.

from Blogger http://ift.tt/2mCQ8LY
via IFTTT


Kategori

Kategori