Showing posts with label 2017 at 01:50PM. Show all posts
Showing posts with label 2017 at 01:50PM. Show all posts
Ni rahisi sana Sana Kwa Mwanandoa Aliyeajiriwa Hapa Mjini Kuchepuka, Hivi Ndivyo Wanavyofanya

Ni rahisi sana Sana Kwa Mwanandoa Aliyeajiriwa Hapa Mjini Kuchepuka, Hivi Ndivyo Wanavyofanya

Nina uzoefu kidogo na mambo ya kazi za ajira maofisini, nimefanya hivi kwa muda mrefu. Wakati flani nilifanya kazi katika ofisi zilizo katikati ya jiji, kule mitaa ya Posta jijini Dar es Salaam.
Ofisi nyingi za serikali na watu binafsi zinapatikana mitaa ile. Kutokana na sababu hiyo, kuna idadi kubwa pia ya migahawa, hoteli, mama ntilie, pub na kadhalika.
Kuna mambo mawili makubwa yenye ushawishi mkubwa wa usaliti. Ofa za chakula au vinywaji na usafiri. Kwa kawaida, wafanyakazi wa ofisi moja hupenda kutoka pamoja wakati wa chakula cha mchana, wenyewe tunapendelea zaidi kusema lunch!
Kila mmoja ana sehemu yake anayokula kulingana na kipato chake, wapo wanaokwenda Southern Sun kupata chakula cha mchana, na wapo wanaowafuata mama ntilie wanaojibanza kwenye vichochoro vingi vilivyopo mjini.
Huko ndiko tunakokutana na akina dada waliovalia vizuri na kupendeza, wakitokea katika maofisi mbalimbali, huwezi kujua yupi ni mhudumu wa chai, yupi ni bosi, wote wanang’ara. Na hapa ndipo ofa za misosi zinapoanza kushawishi ngono.
Kijana mmoja mwenye kipato kikubwa ofisini kwake, atavutiwa na msichana mrembo mwenye mshahara wa wastani. Ili kumsogeza karibu, atalipia chakula cha siku hiyo na kumualika kwa kesho yake. Kulipiwa chakula ni jambo dogo, lakini lenye thamani kubwa sana. Si rahisi mtu aliyekulipia chakula kwa nia njema, ukaacha kumshukuru na hata kumwelekeza unapofanya kazi.
“Mimi nipo pale Oj Traders,” msichana anaweza kujita mbulisha jina na kusema anapofanyia kazi huku mkaka akimweleza kuwa yeye ni mhasibu katika ofisi flani. Watakapo
kutana mara ya pili, wataachiana namba za simu.
Baada ya hapo, mkaka atafanya mbwembwe za kuhamahama maeneo ya lunch ili mradi tu mdada wa watu aingie kwenye laini. 
Ukimaliza suala la lunch, kuna hii kitu foleni, hasa kwa wakazi wa Dar es Salaam. Raha ya kufanya kazi katikati ya jiji inaingia shubiri kadiri jioni inavyozidi kusogea. Kuanzia saa kumi, ni vurugu katika vituo vya daladala na hasa wakati kama huu ambao bodaboda zimezuiliwa kuingia mjini.
Wenye magari binafsi ndiyo wakati wao wa kujidai, ingawa foleni inawakumba wote. Lakini ni afadhali ukiwa kwenye foleni ndani ya gari dogo, mko wawili kuliko foleni, umeshika bomba kwenye daladala.
Siyo rahisi kwa mdada kukataa lifti ya kijana mwenye gari. Na katika foleni ndefu, ni wazi kwamba hadi mwisho wa safari, watakuwa wameshabadilishana namba. Kwa msichana, kuwa na uhakika wa usafiri kila siku ni ukombozi.
Tusidanganyane, hakuna msichana ambaye hatajua kuwa lunch au usafiri anaopewa unahitaji malipo maalum, ambayo ni penzi. Hali hii haiko Dar tu, bali nchi nzima na pengine duniani kote.
Mwanamke aliyeajiriwa anakuwa katika mitihani mikubwa zaidi ya kusaliti ndoa au uhusiano wake, kwa sababu hata kama haitakuwa kwenye chakula au usafiri, bado watu anaokutana nao katika utendaji wake, wanaweza kumghasi. Fikiria anakutana na mabosi, marafiki wa mabosi wake, wafanya biashara, atapona kweli?
Hata hivyo, simaanishi kama tabia hii inawakumba waajiriwa wote, isipokuwa nadhani ni sehemu kubwa wanahusika!
By Mike Tee
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2uFRaeu
via IFTTT


Maneno ya Babu Tale kwa DJ Choka Baada ya Kuweka wazi Kuwa Aliugua TB

Maneno ya Babu Tale kwa DJ Choka Baada ya Kuweka wazi Kuwa Aliugua TB

Meneja wa kundi la Tip Top Connection pamoja na mwimbaji staa wa Bongofleva Diamond Platnumz, Babu Tale ameizungumzia issue ya DJ Choka kuweka wazi kuwahi kuugua ugonjwa wa Kifua Kikuu (TB) mpaka alivyopata matibabu na kupona.
Babu Tale alitumia ukurasa wake wa Instagram kumpongeza DJ Choka kwa kuamua kuweka wazi alichokuwa anaumwa akisema ni mfano wa kuigwa kwani watu wengi wamekuwa wanaficha juu ya magonjwa yanayowakibili.
“Wahenga walisema mficha uchi hazai, wakazidi kusema mficha maradhi kifo humuumbua, kwanza kabisa nimeguswa na kufurahishwa na kitendo cha kijasiri alicho kifanya ndugu yangu @chokadj kwa kuiwekea wazi jamii nini alikwa anaumwa na kwa kudra zake Mungu akapona.
“Imekuwa ni jadi sikuhizi kwa vijana wengi alwatan kuficha maradhi yao huku wakisahau hofu na wasiwasi pia nayo ni ugonjwa, na kadri unavo zidi kuficha ndivyo kadri ugonjwa unazidi kukomaa.
“@chokadj kawa mfano mzuri kwa jamii yetu ya sasa kudhihirisha kuwa kuficha maradhi si suluhisho wa tiba ya ugonjwa wako, ni wangapi jana walikuwa wamejifungia ndani wakiugulia TB huku mioyo yao ikiamini TB haitibiki lakini baada ya @chokadj kujitokeza na kuiambia jamii ameuguwa ugonjwa huo na kupona leo wagonjwa hao hao wapo kwenye foleni hospitalini wakingojea huduma ya matibabu.
Ndugu zangu halimpati mtu jambo isipo kuwa Mungu kutaka kwan kwa hakika ni yeye pekee atupae mitihani na majibu yake akakupatia. Sasa nazidi kuaminu TB ina tibika. #AsanteChoka“ – Babu Tale.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2tx0bKe
via IFTTT


TAARIFA MPYA KUHUSU KESI YA VIGOGO WA ESCROW NA MALI ZAO

TAARIFA MPYA KUHUSU KESI YA VIGOGO WA ESCROW NA MALI ZAO

Serikali imekamata mali za wafanyabiashara Harbinder Singh Sethi na mwenzake James Rugemalira wanaohusishwa na uchotwaji wa zaidi ya Sh bilioni 300 katika Akaunti ya Tegeta Escrow.
Mali hizo zimekamatwa siku chache baada ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (Takukuru) kuwafikisha watuhumiwa hao mahakamani.
Kwa mujibu wa gazeti la MTANZANIA Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Biswalo Mganga hakuweza kupatikana kutoa ufafanuzi wa kina wa hatua ya ofisi yake kushikilia mali za Sethi na Rugemalira.
Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), iliiambia MTANZANIA jana kuwa Serikali imelazimika kukamata mali zote za wafanyabiashara hao kama hatua ya kuzuia kuuzwa au kuhamishwa umiliki wake wakati wakiendelea kusota rumande.
“Ni jambo la kawaida katika kesi kama hii, huwezi kuacha mali ambazo ndizo kielelezo katika suala hili. Hivyo hatua ya kwanza ni kumkamata mshtakiwa na kisha ni lazima udhibiti mali zake kwani ndiyo kielelezo muhimu kinachobishaniwa katika kesi husika.
“Unaweza ukaiacha mali halafu mshtakiwa huku akiwa yupo ndani bado akaendelea kutoa maelezo na mali kuhamishwa umiliki wake au hata kuuzwa, kwa hali hiyo ndiyo hulazimika kushikilia mali hizo,” alisema mtoa taarifa huyo ambaye hakupenda kutajwa jina lake .
Ofisi ya DPP inaelezwa imezuia mali zote za Sethi na Rugemalira kwa kuziweka chini ya ulinzi mkali pamoja na kufunga kwa muda akaunti zao za benki.
Sethi ambaye ni Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL)/Pan Africa Power (PAP) na Rugemalira wa Kampuni ya VIP Engineering and Marketing Ltd, walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam Juni 19.
Watuhumiwa hawa tayari wamesomewa mashtaka sita, yakiwamo ya uhujumu uchumi.
Mbali na hayo imeelezwa kuwa orodha ya waliopata mgawo wa fedha hizo za Escrow imezidi kuongezeka, wakiwamo vigogo kutoka wizara nyeti, taasisi, viongozi wa dini na mashirika yasiyo ya kiserikali na tayari baadhi yao wameanza kuhojiwa na Takukuru mapema wiki hii.
Taarifa za ndani zinaeleza kuwa idadi ya waliohojiwa imefika zaidi ya watu 30 hadi sasa.
Miongoni mwa wanaotajwa kuhojiwa na Takukuru wamo baadhi ya mawaziri wa Serikali ya Awamu ya Nne na mtoto wa kigogo wa Serikali, ambao inaelezwa kuwa huenda wakafikishwa mahakamani Jumatatu, huku wengine wakiendelea kuhojiwa zaidi.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2t91PBw
via IFTTT


RC Gambo Ameivua Nguo Serikali na Mamlaka Iliyomteua..!!!

RC Gambo Ameivua Nguo Serikali na Mamlaka Iliyomteua..!!!

Kwa baadhi ya vitendo au maamuzi yanayofanywa na huyu kiongozi kwa kutumia cheo chake yananifanya niamini kumbe hata mimi naweza kuongoza vizuri na kwa busara kuliko huyu.
Kitendo cha kukamata watu walioenda kufarijiana kwa msiba uliotokea eti ni mkusanyiko usio halali eti hauna kibali, hata atumie hoja nyingi kias gani kujisafisha ukweli utabaki palepale
Ameivua nguo serikali na mamlaka iliyomteua. 
Kitendo hiki kimepanda chuki juu yake kwa sababu kuna watu wengi wapo nyuma ya waliokamatwa mfano wale viongozi wa dini. Yaani hapo wisdom empty hata kama itatumika jiki kusafisha hilo halitoki kwenye mioyo ya watanzania.
Hata kama nitakamatwa mimi mtoa hoja, bado ukweli utabaki hapo na cheo chako ni dhamana tu kesho tutakuwa wote huku mtaani. Sidhani kama alifikiri vizuri impact ya kitendo hiki, bado najiuliza hivi asingewakamata na kuwalaza polisi kwani kuna madhara yangetokea?
Jambo la pili ni kuhusu rambi rambi..
Najiuliza; Je, kama serikali inatumia rambirambi kinyume na matakwa ya waliotoa rambirambi na yenyewe ipo tayari fedha inazotuma kwenye halmashauri nchini zitumike kinyume na maelekezo?
Nakumbuka mara kadhaa waziri mkuu amekuwa akitoa onyo kali kwa viongozi kunapokuwa na fungu fulani limetolewa kwa shughuli fulani kwamba zitumike kama ilivyopangwa.
Chanzo – JF

from Blogger http://ift.tt/2qfdzxG
via IFTTT


CCM Wairuhuu CHADEMA Kutumia Ukumbi Wao wa Mikutano wa Dodoma Conventio Center..!!!

CCM Wairuhuu CHADEMA Kutumia Ukumbi Wao wa Mikutano wa Dodoma Conventio Center..!!!

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi, Humphrey Polepole amesema kuwa ni ruksa kwa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo ( CHADEMA) kutumia ukumbi wao wa mikutano maarufu kama ‘Dodoma Convention Centre’.
Kauli hiyo imetolewa na Polepole kufuatia mazungumzo aliyofanya kwa njia ya simu na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Aikael Mbowe tarehe 14 Mei 2017 juu ya uwezekano wa chama hicho kutumia ukumbi huo. Polepole amemwambia Mbowe kuwa CCM haioni uzito wa kutoa kibali kwa CHADEMA kutumia ukumbi huo ikiwa watawasilisha maombi rasmi kwa Katibu Mkuu Abdulrahman Kinana.
Hata hivyo, Polepole amemweleza Mbowe kuwa wataruhusiwa tu kuutumia ukumbi huo ikiwa watakubali masharti ya kutoweka alama za chama chao nje ya ukumbi huo isipokuwa sehemu ya ndani.
Tarehe 27 Mei 2017, CHADEMA watafanya Mkutano wa Kamati Kuu Mjini Dodoma na taarifa iliyotolewa na Msemaji wa chama hicho Boniface Makene haijabainisha ukumbi watakaotumka. Upo uwezekano kuwa Mbowe ametekeleza masharti aliyopewa na huenda mkutano huo utafanyika ndani ya ukumbi wa CCM.

from Blogger http://ift.tt/2qfuJLA
via IFTTT


Harmonize Jifunze Kwa Diamond Utafanikiwa

Kufuatia mapovu anayoyatoa kwenye mitandao pale anaporushiwa vijembe Harmonize ameshauriwa haya:
HARMONIZE JIFUNZE KWA DIAMOND UTAFANIKIWA:Nadhani @harmonize_tz atambue kuwa boss wake @diamondplatnumz mpaka hapo alipofika ameruka madaraja mengi sana mfano:diamond alitoa wimbo wa nataka kulewa wakajitokeza watu wakasema kaiba idea yote tena wakawa wanazunguka kwenye media kulalamika diamond ndani ya miezi kama miwili hakuwajibu kwa maneno bali aliachia ngoma kali ya kesho ikawazima wote waliokuwa wanalalamika.
@richmavoko alifanya show mbovu ya fiesta akasema amelogwa na diamond ila diamond hakumjibu chochote alimuacha tu afurahishe nafsi yake mana aliona akijibu ataonekana ndio mbaya leo hii mavoco huyo huyo yuko w.c.b ya diamond. @diamondplatnumz alitamka waziwazi kuwa anampenda @qchief sana tena baadae q.chief akasema diamond anamuibia nyota yake ila leo q.chief huyo huyo amerudi na yuko na diamond vizuri tu.@harmonize_tz hebu jiulize diamond angekuwa watu wote wanaomkera anajibu mitandaoni basi account yake ingejaa majibizano na watu ila yeye alichagua kuwajibu kwa kazi na hayo ndio majibu mazuri sana kwa haters.Ishi kwenye misingi hii ya @diamondplatnumz kujibu watu kwa kazi utafanikiwa sana.
USIWAJIBU SANA KWA MANENO JIBU KWA VITENDO.WEWE BADO NI MTAFUTAJI.
KUNA WATU KATIKA MAISHA WAPO KWA AJILI YA KURUDISHA NYUMA JUHUDI ZA WATU NA KUNA WATU AMBAO UKIPATWA NA BAYA KWAO NDIO FURAHA JIFU
Tazama video Mtoto amvua kofia Papa Francis

from Blogger http://ift.tt/2nCWjDp
via IFTTT


Kategori

Kategori