Showing posts with label 2017 at 11:06AM. Show all posts
Showing posts with label 2017 at 11:06AM. Show all posts
Kamanda wa Trafiki mkoani Pwani asimamishwa kazi

Kamanda wa Trafiki mkoani Pwani asimamishwa kazi

NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, amelitaka Jeshi la Polisi kumuondoa katika nafasi ya Mkuu wa Polisi, Usalama Barabarani (RTO) Mkoa wa Pwani na kuchukuliwa hatua za kinidhamu kutokana kwa kushindwa kusimamia sheria za usalama barabarani mkoani humo.
Masauni akiwa ameambatana na Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Fortunatus Musilimu, alitoa agizo hilo katika Kituo cha Mabasi cha mjini Kibaha Maili Moja baada ya kufanya ziara ya kushtukiza kituoni hapo leo, kwa ajili ya kufuatilia maelekezo yake aliyoyatoa alipofanya ziara kama hiyo mwaka jana.
“Mwaka jana nilipofanya ziara kituoni hapa nilitoa maelekezo nilipokuta kuna mapungufu katika ukaguzi wa magari, tukakubaliana atayafanyia kazi haraka iwezekanavyo, lakini hakuna mabadiliko yoyote, magari hayakaguliwi, huku ni kuhatarisha usalama wa abiria,” alisema Masauni na kuongeza kuwa;
“RTO ameshindwa kuendana na kasi ya awamu ya tano, nataka aondolewe katika nafasi hiyo na achukuliwe hatua ya kinidhamu, hatutati uzembe, hatutaki kucheza na maisha ya watanzania.”
Masauni mara baada ya ukaguzi wa kituo hicho, aliendelea na ziara yake mkoani Pwani ambapo alifanya ukaguzi wa aina hiyo mjini Chalinze na baadaye Msata na kuimalizia ziara yake Bagamoyo.

from Blogger http://ift.tt/2ud1T2B
via IFTTT


Nay Wa Mitego Amjibu Waziri Mwakyembe Kuhusu Kutoimba Siasa

Nay Wa Mitego Amjibu Waziri Mwakyembe Kuhusu Kutoimba Siasa

Rapa Nay wa Mitego amefunguka na kumtaka Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe kutoa ufafanuzi juu ya kauli yake aliyotoa kuwa wasanii wasijihusishe na masuala ya siasa.
Nay wa Mitego akiongea kwenye kipindi cha Planet bongo ya East Africa Radio, amesema kuwa yeye anaamini muziki ni siasa na siasa ni muziki hivyo ni ngumu kutofautisha vitu hivyo viwili, hivyo amemuomba Waziri mwenye dhamana kutoa ufafanuzi juu ya kauli hiyo na kudai yeye hajawahi kuimba wimbo wa siasa bali anaimba mambo yaliyopo kwenye jamii.
“Nachoamini mimi muziki ni siasa na siasa ni kama muziki, siasa ni maisha ya watu ambayo wanaishi kila siku na muziki pia ni maisha ya watu ambayo wanaishi kila siku kwa hiyo anahitaji kutoa ufafanuzi wa kutosha juu ya hili. Siasa ni maisha ya watu na muziki ni maisha ya watu, mimi binafsi naamini sijawahi kuimba wimbo wa siasa hata siku moja bali ninaimba maisha ya watu ambayo yanaendelea kila siku na ndiyo maana wengi wanathubutu kusimama upande wangu endapo linatokea tatizo lolote” alisema Nay wa Mitego.
Mbali na hilo Nay aliendelea kusisitiza kuwa kuna haja Waziri kutoa ufafanuzi wa jambo hilo
“Mh. Waziri anatakiwa kutoa ufafanuzi juu ya jambo hili ili watu wajue kipi hawatakiwi kuimba na kipi wanatakiwa kuimba sababu siasa ni maisha ya watu ya kila siku na muziki wa Hip hop ni maisha ya watu ya kila siku, kwangu mimi muziki wangu hauwezi kubadilika zaidi nitazidi kuongeza vitu ili nisiwaudhi watu na nizidi kuongeza idadi ya mashabiki” alisisitiza Nay wa Mitego

from Blogger http://ift.tt/2qOb2Nt
via IFTTT


Chukua Hii Ikusaidie..Tanzania Yangu Usipumbazwe na Yanayoendelea Mitandaoni..!!!

Chukua Hii Ikusaidie..Tanzania Yangu Usipumbazwe na Yanayoendelea Mitandaoni..!!!

Je Watanzania wenzangu maoni na mitizamo inayoandikwa mitandaoni ndio mtizamo halisi wa Watanzania wote juu ya serikali yetu?
Zile methali zetu za ‘miluzi mingi humpoteza mbwa’ nadhani itaendelea kutuathiri kwa kipindi kirefu sana!
Wakati fulani tunashindwa hata kushtuka kuwa tunatumiwa na magenge yanayopambana na serikali kuiondoa kwenye agenda zake muhimu.
Tumekoswa uzalendo wa kuwatetea viongozi wetu na kuwakosoa kizalendo pale wanapokosea na kusahau mara moja jitihada kubwa na uthubutu wa hatari waliojivika kulitoa taifa hili kule lilikonasa.
Kuna jambo limeibuka la watu kutekwa na kupotea, limekuwa kama maigizo au series ambalo mimi naweza kusema linaweza kuwa linafanywa na yeyote kati ya hawa wafuatao:-
– Serikalikali yenyewe ( upstairs wakiwa wanajua kila kitu)
– Wapinzani wa serikali wakiwa ndani ya serikali ili kuipaka matope serikali.
-Wapinzani wa serikali nje ya serikali, na
-Wahalifu wengine wasio na uhusiano au wakiwa na uhusiano na makundi niliyoyataja hapo juu.
Mojawapo ya kundi lolote kati ya haya linaweza kuendesha tamithiliya za namna hii kwa malengo linayoyajua lenyewe
Si haki kuwashambulia viongozi wa serikali tu bila kuyashuku makundi mengine ambayo ni hatari zaidi hasa katika namna ambayo yanatambua kuwa hatuyawazii km yanaweza kuwa yanaendesha kampeni hatari kama hizi. Viongozi wetu ni binadamu pia, watakata tamaa kisha kesho yetu iwe mbaya zaidi. Mambo mengine tusiyo na uhakika nayo tuziachie mamlaka na Mungu mwenyewe.
Vyombo vyetu vya habari vimekuwa bize kusoma tabia za Watanzania kujua viwauzie habari za namna gani bila kujali vinajenga au vinabomoa ili mradi vimeuza.
Punde tutafaulu kuiangusha serikali yetu wenyewe na wanasiasa watakaofata watageuza siasa kama biashara kichaa ambayo hawana haja ya kujitoa mhanga kwa maswala nyeti yanayorudisha nyuma ustawi wa taifa letu.
Kisha tutarudi kulekule ambako 
Hatutasikia tena gari zimekamatwa bandarini ktk makontena,
Hatutasikia tena habari za makontena elfu kadhaa yamebainika kupita bandarini bila kulipiwa ushuru,
Habari za udhibiti wa wafanyakazi hewa,
Udhibiti wa safari zisizo na tija,
Kufutwa kwa posho za vikao na zinginezo maeneo ya kazi
Kurejeshwa kwa nidham maeneo ya kazi
Vita dhidi ya madawa ya kulevya ambayo kwa watanzania wazalendo tusingesita kutoa ushirikiano wala tusingeona style iliyotumiwa ya kukusanya watuhumiwa wote kuwa ni udhalilishaji bali ni njia ya kuwasafisha wanaotuhumiwa bure na kuwadhibitisha wanaohusika. 
Badala yake tumeamua kuwa bendera….
Wito wangu kwa viongoz wa serikali, mstoke katika ajenda zenu kwa ajili ya Tanzania njema ya kesho, hata Yesu alipata shida znazofanana na hizo.
Kipimo cha idadi ya Watanzania walionyuma yenu mtakiona 2020, MSITISHIKE na kampeni za wauza unga, mafisadi na wenzao waliojificha ktk uanasiasa, uandishi na usanii

from Blogger http://ift.tt/2oe5drg
via IFTTT


Kategori

Kategori