Showing posts with label 2017 at 02:40PM. Show all posts
Showing posts with label 2017 at 02:40PM. Show all posts
Breaking News: Askofu Gwajima Afutiwa Kesi na Mahakama

Breaking News: Askofu Gwajima Afutiwa Kesi na Mahakama

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imemwachia huru Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima katika kesi ya kutoa lugha ya matusi dhidi ya Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo.
Gwajima ameachiwa huru leo baada ya mahakama kuifuta kesi hiyo kwa sababu upande wa Jamhuri umeshindwa kuonesha kujali kwani kwa miezi 14 wameleta shahidi mmoja kutoa ushahidi.
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Cyprian Mkeha, ametoa uamuzi huo leo wakati kesi hiyo ilipokuja kwa kusikilizwa huku upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Joseph Maugo, ukiomba upewe ahirisho lingine kwa kuwa hawakuwa na shahidi.
Mkeha aliamua kuifuta kesi hiyo kwa kutumia kifungu cha 225 cha Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Jinai (CPA) na kumwachia huru Gwajima.
Alisema upande wa Jamhuri umeshindwa kuonesha kujali shauri hilo ambapo ndani ya miezi 14 umeita shahidi mmoja tu.
Gwajima alipandishwa kizimbani mahakamani Aprili 17,2015 akidaiwa kati ya Machi 16 na 25, 2015, katika viwanja vya Tanganyika Packers, vilivyopo Kawe jijini Dar es Salaam, alitoa lugha ya matusi kwa Kardinali Pengo.
Alitamka: “Mimi Askofu Gwajima nasema Askofu Pengo ni mpuuzi mmoja yule, mjinga mmoja, amekula nini yule, sijui amekula nini yule mtoto hana akili yule..”
Chanzo:mtanzania Digital

from Blogger http://ift.tt/2p7uvpB
via IFTTT


Lijualikali apokelewa na sumaye uraiani

Lijualikali apokelewa na sumaye uraiani

Frederick Sumaye, Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani (mwenye suti nyeusi) akiwa Peter Lijualikali, Mbunge wa Kilombero (suti ya kaki) na wanachama wa Chadema wakitoka gerezani Ukonga
FREDERICK Sumaye, Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani, ameongoza viongozi wa Chadema waliofika kwenye gereza la Ukonga kumtoa Mbunge wa Kilombero, Peter Lijualikali, anaandika Pendo Omary.
Lijualikali ametoka gerezani baada ya kushinda rufaa yake jana katika Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam, baada ya kuhukumiwa kifungo cha miezo sita na mahakama ya Hakimu Mkazi Kilombero, Januari 11, 2017.
Sumaye alikuwa miongoni mwa vigogo wa Chadema ambao waliwasili gerezani hapo mapema leo asubuhi na kufuata taratibu za kumtoa mbunge huyo wa Kilombelo aliyekuwa anatumikia kifungo chake.
Viongozi hao wa Chadema wakiwa na mawakili wa Lijualikali waliofanikisha kushinda rufaa yake, walifanikiwa kumtoa mbunge huyo na kuendelea na shughuli nyingine.

from Blogger http://ift.tt/2oGq5F5
via IFTTT


Kategori

Kategori